Wakati ambapo wanawake hukua, hupenda sana kujikita kuangalia filamu, tamthilia za mahaba ambazo zinajenga dhana ya kuwa mr Right anaweza kutokea siku moja katika maisha ya mwanamke. Dhana hii imekuwa ikiendeshwa na movie nyingi kama vile za Cinderella nk ambapo mhusika anapendwa na mwanaume aliyekutana naye kighalfa na mwishowe wanaishi maisha ya raha mstarehe.
Well, hizo ni ndoto ambazo haziwezi kutimia na unafaa kuamka kutoka katika ndoto uliokuwa ukilala na kuikumbatia ulimwengu wa uhalisia.
So, sababu za wewe kuwa single mpaka sahizi ni zipi?
Kiukweli ni kuwa hakuna mtu anaishi maisha ya cinema. Kama umekuwa
ukitafuta kuwa na uhusiano lakini unashindwa kuwa na mafanikio,
unahitaji kusoma baadhi ya sababu ambazo tumeziorodhesha.
1. Una orodha ulioiandika
Wanawake wote huwa na mawazo ya mr Right kwa akili zao. Kawaida huwa ni
yule ambaye anapatikana katika filamu na sinema. Iwapo una orodha
ambayo umeiandika, orodha hio inafaa iwe kama mwongozo tu.
Kama uko mbioni kutafuta mahusiano na mwanaume mwenye kima cha futi
sita, mhandsome, mwenye uwezo kifedha, macho ya hudhurungi, mjanja,
mzuri, unafaa kufahamu ya kuwa mwanaume huyo anaweza kupatikana ila tu
anaweza kuwa si mwenye kima cha futi 6 ama mwenye macho ya hudhurungi.
Kama atapata wa futi 5 na nchi 9 kumbuka kuwa orodha yako haufai
kuitilia maanani sana.
Kiufupi ni kuwa haufai kuizingatia orodha yako ulioiandika asilimia 100,
si lazima upate mwanaume ambaye ana masharti yote ambayo unataka.
2. Unatext wanaume wengi kupita kiasi
Ni hisia iliyo ya juu kujua kuwa unapendwa, unababaikiwa na
kuhangaikiwa. Lakini kama utaanza kuongea na mwanaume, ukaenda naye deti
mara kadhaa, na kuanza kudhania ya kuwa ni boyfriend wako, basi unafaa
kuwapotezea wale wengine na uache kuongea nao asilani.
Kama hauwezi kujizuia kuzungumza na mtu mmoja, na kila wakati ambapo
utakuwa ukileta gumzo la kuwa huwezi kuacha kuchat na wanaume wengine
fahamu ya kuwa unamsukuma mbali mwanaume ambaye umemzimia.
Haya ni mambo mawili ambayo anaweza kuamua kuchukua: anaweza kukuambia
uachane na kutext hao wanaume wengine ama atachoshwa na kuskia gumzo
lako la kila wakati ambalo unawataja wanaume wengine mara kwa mara.
Hivyo kama unachat na wanaume wengine wengi, jua ya kuwa yule ambaye uko
naye kwa sasa anaweza kuona ya kuwa hauko interested na yeye.
3. Unaongea ubaya kuhusu marafiki zako
Kuongea ubaya kuwahusu marafiki zako kwa mwanaume umemzimia ni jambo
ambalo unafaa kuacha. Hakuna mtu ambaye angependa kuhusishwa na mwanamke
mlalamishi ama malkia wa drama, na iwapo unaongea mabaya kuhusu
marafiki zako huwa unaongea nini kingine?
Baada ya muda ataanza kuingiwa na maswali ya mbona bado uko na marafiki
zako, na pia anaweza kuingiwa na mawazo ya kuwa pindi mtakapokuwa katika
mahusiano utakuwa ungeongea uchafu na ubaya kumhusu na marafiki zako.
Hakuna mwanaume ambaye yuko radhi kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye
ana uhakika wa kuwa ataanza kutoboa siri zake kwa marafiki zake.
4. Unachezewa, na kila mwanaume anachukiza
Ni kweli kuwa kila mtu ashawahi kuwa na mahusiano mabaya na mwanaume
mara moja au nyingine. Ashawahi kufikia hatua ya kuwachukia wanaume
kiasi cha kuwa hautamani kuongea nao kabisa. Kama wewe ni mwanamke
ambaye ushawahi kuwa katika mahusiano ambayo ulichezewa, na umeshindwa
kuvumilia na kuyasongeza maisha yako, inakubalika. Mambo kama haya
huchukua muda hadi yatakapoisha.
Lakini kama uko katika deti na mwanaume, haufai kuongea wakati wote
kuhusu ubaya wa ex wako na jinsi ambavyo alivyokuumiza, jinsi
unavyofikiria kuwa wanaume wote ni waongo na wadanganyifu, na jinsi
ambavyo hutambui iwapo mapenzi ya kweli yanaweza kupatikana dunia hii.
Mwanaume unayetoka naye deti si chanzo cha kwako kukosana na ex wako
hivyo hupaswi kumlalamikia bali unafaa kukubali matokeo yaliyofanyika
awali na kusongea mbele na maisha yako. Kama unaogopa na swala la kuwa
unaweza kudanganywa, basi tatua shida zako ukiwa single.
5. Hautaki kufanya kazi
Kama ndoto yako ni kuwa unatamani kuwa mama wa nyumbani, ni vizuri.
Lakini katika deti ya kwanza na mwanaume hana haja ya kusikia mambo kama
hayo. Wanataka kukutana na wewe, lakini kuona sehemu yako ambayo uko
mchangamfu. Wanataka kuona sehemu yako ya shangwe, ki wewe ambaye una
furaha na mtu wa ashki.
Wanaume hawapendi kujihisi kama unawaangalia wao, kupanga harusi, watoto
wangapi utapata, na chochote kile ambacho kitakuwa kikizulika kwa akili
yako. Kila mtu ana mawazo ya fumba kwa akili yake, hivyo yanafaa kubaki
akilini mwako na si kila mtu anahitaji kujua. Wanaume hawapendi presha,
haswa ile ambayo inajitokeza katika deti ya kwanza. Wanaweza kujua
dalili iwapo mwanamke anataka kuolewa kama kesho! Hivyo acha tabia za
tai.
6. Unapinga kila wakati
Kama unaongea na mwanaume halafu akakuuliza ufanye kitu flani, lakini
kila wakati unapinga, itafika wakati flani ataacha kukuuliza. Kama tu
vile ukiwa na marafiki zako, nadhani ushawahi kukumbwa na kutohusishwa
na jambo fulani, halafu baadae marafiki zako wakakuambia kuwa imetokana
na kuwa unakataa vitu ambavyo unaagizwa kufanya. Iwapo kila wakati
unakuwa mgonjwa, unafanya kazi, unafanya kitu fulani, basi pia utakuwa
single milele.
7. Mitandao ya kijamii umeifanya maisha yako
Ok mitandao ya kijamii ni mizuri kutangamana na wenzako, lakini
usiifanye kama ni sehemu ya kwako kunyatia profile za wengine, haswa kwa
mwanaume ambaye unadeti naye. Ukianza kudeti na mwanaume, utakuwa
ukiyaingia maisha yake, na hii itakufanya mtu mgeni kwa maisha yake.
Ok ni hivi, hufai kuichunguza akaunti yake kabisa sababu unaweza kuona
comments, picha nk ambazo zinaweza kukuchanganya. Usijishughulishe
kuangalia vitu ambavyo hujahusishwa. Hii ni kwa sababu unaweza kuona
comment ama picha iliyotumwa kwakwe na mwanamke flani, jambo ambalo
hutalichukulia vizuri.
8. Kushtushwa na mwanaume ambaye anaonyesha maridhia kwako
Hii ni muhimu sanaa. Kama wewe ni yule ambaye anashtushwa ama
kushangazwa na jinsi mwanaume anaonyesha uzuri na upendo kwako, kama
vile kukusifu, kukufungulia mlango, kulipia gharama zako, ama kimsingi
kukutumikia vile unavyotaka wewe, basi bila shaka wewe ndiwe tatizo lako
mwenyewe.
Relax na utulie, usichukulie kana kwamba yeye anakufanyia hivyo akiwa na
ajenda zake fiche. Kama utaonyesha dalili za kutomwamini basi utamfanya
ahisi ya kuwa huthamini kile ambacho anajaribu kukuonyesha ama
kukufanyia.
9. Kuwa na mtihaji mwingi
Uhitaji ni ile tabia ambayo unajipendekeza kwake mara nyingi. Mwanamke
hafai kuwa masaa 24/7 anataka kuwa kando na mwanaume. Unafaa mara moja
au nyingine kuwa na shughli zako mwenyewe. Ukiwa kila wakati utakuwa na
mwanaume basi anaweza kukuzoea na kukudhalilisha ama kuchukizwa nawe.
Mahusiano yanahitaji muda mpaka yakolee, si eti utapata mpenzi wako
chini ya masaa 48. Mwanzo unafaa umpe nafasi ya yeye kujiskia huru kwa
kumpa nafasi kutangamana na marafiki zake na wewe kuenda kujumuika na
wanawake wenzako.
10. Unapenda kuwa na marafiki zako wa dhati kila wakati
Kama wewe ni yule ambaye kila wakati anakuwa na rafiki yake ukitaka
usaidizi wa kimawazo, maoni, mtizamo wake ikija na maswali ya maisha
yako yakudeti, inamaanisha ya kuwa huna usalama kujihusu wewe mwenyewe
na huna uwezo wa kujiamulia.
Ni vizuri kujumuika na marafiki zako lakini haina haja ya kuwajuza
kuhusu chochote ambacho kinahusiana na maongezi, matatizo ama chochote
kuhusu boyfriend wako. Kuna vitu vingine havina haja kuvieleza hadharani
kwa marafiki zako.

No comments:
Post a Comment