Ukijifanya fala wa kuchukua hatua ya haraka kumkiss mpenzi wako kwa mara
ya kwanza bila kusoma ishara dhabiti inaweza kukuletea aibu, ama zaidi
kukufanya upungukwe na kujiamini kwako wakati mwingine ambao mtakutana
tena.
So utafanyaje usipate aibu ama kupungukiwa na kujiamini?
Jambo la msingi ni kuwa lazima nyote wawili muwe mumevutiana aidha
kimapenzi ama kuna kemia ya kimahaba ambayo imejijenga kati yenu. [Soma:
Njia tatu za kujenga tenshen ya kimapenzi]
Ok. Kuna wengine wangepinga msimamo wangu wa hapo juu ya kuwa si lazima
kuwe na mvuto wa kimapenzi kati yenu... Jibu langu ni rahisi. "Unless
nyote wawili mumekutana kwa kilabu ama sehemu nyingine na nyote wawili
mumeathirika kwa kubugia bia nyingi, haitakuwa jambo zuri kama utachukua
hatua ya kumkiss yeyote...mwanzo kumkiss mtu ambaye humjui vizuri
kunaweza kuwa matatizo chungu nzima"
So ina haja gani ya wewe kumkiss mtu ambaye humjui? Mbona usimkiss mtu
ambaye tayari umemzoea na ambaye kuna tenshen ya kimapenzi kati yenu?
Hoja hii ndio imenifanya nije na:
Dalili za kuonyesha kama imetimia kumla dende mpenzi wako
1. Kabla siku yenu ya kukiss iwadie lazima muwe mumekumbatiana mara kwa
mara, mumeweza kugusana na kutomasana sehemu tofauti tofauti hasa kwa
mikono, shingo, viganja ama sehemu yeyote ile ambayo nyote wawili
mumeona ni sawa. Iwapo hamjawahi kufanya hatua hata moja kama hii, ni
bora zaidi usijaribu kuchukua hatua ya kukiss kwani itakujeukia wewe
mwenyewe. [Soma: Hatua za kumpapasa mwanamke kiujanja na akukubali papo hapo]
2. Kabla hatua ya kukiss haijawaidia, kwa kawaida inatoa wakati ambapo
nyinyi wawili mnakaribiana kimwili kuliko kawaida yenu. Mara nyingi
wapenzi wawili huanza kugusana mikono, viganja, mgongo au wakati
mwingine miguu.
3. Wakati ukifika nyinyi wawili mtakuwa mkiangaliana sana kwa macho huku
mkipuuzia mazingira ambayo yamewazunguka. Hatua kama hii ikifika
usipoteze muda zaidi. [Soma: Njia za kumshawishi mwanamke kwa kutumia macho]
4. Wakati mwingine ghafla maongezi yenu yanasimama halafu mnaanza
kuangaliana machoni kwa muda mrefu kuliko kawaida. Ijapokuwa maongezi
yenu yatakuwa yamesimama, hamtaona jambo lolote la kutatanisha bali
mtakuwa mnaskia raha na mnavutiana zaidi.
5. Wakati huo mtakuwa mnajiskia mko na raha, na mnaweza kuwa mnacheka
sana ama mnatabasamuiana nyote wawili. Ukiona hatua kama hii mpenzi wako
anatabasabu na wewe unatabasamu, unaweza kuchukua hatua ya pili ambayo
tumeieleza hapo juu.
6. Dalili dhahiri ya kuonyesha kuwa hufai kupoteza hata sekunde moja
zaidi ni pale ambapo mpenzi wako ataanza kuonyesha dalili za wazi za
kuanza kujilamba midomo yake huku akiiweka unyevu. Pia ukiona akianza
kuuma midomo yake huku akiiviringa kwa mitindo flani ni ishara ya
kukuambia: "wapoteza muda wangu, nataka unile dende sasa hivi"
7. Mwisho ni kuwa vichwa vyenu vitapinda upande wa kulia huku
mkisogeleana. Tenshen ya kimapenzi itakuwa imejijenga kati yenu huku
ikikoroga akili na miili yenu. Na mwisho ni ile hatua ya kuyeyusha kiu
ambacho kimekuwa kikikuandama tangu siku ulipoweka nuru ya kumwona
uliyempenda.
Upo!? [Soma: Kutongoza kwa wanaoanza]

No comments:
Post a Comment