Katika safari ya mapenzi wanandoa huwa wanakutana katika maeneo
mbalimbali, wapo wanaokutana vyuoni,shuleni, kwenye nyumba za ibada,
sokoni, kwenye daladala, kuunganishwa na mtu mwingine, au baada ya
kusikia sauti kwenye simu, redioni, hotelini na sasa wengine kupitia
mitandao ya kijamii kama facebook
Ukweli ni kwamba katika mitandao unapoanzisha uhusiano na mtu
usiyemfahamu inawezekana ameona picha yako tu nakukuambia kuwa
anakupenda na wewe ukiona picha yake ukaridhika naye mkaamua kuanzisha
uhusino ni vyema kuonana kabisa ili kuwa na uhakika na uhusiano mnaotaka
kuanzisha kwani unahitaji kumfahamu zaidi na ndipo utakapoweza
kufanya maamuzi ya kukubali au kukataa.
Anaweza kuwa rafiki yako wa kawaida lakini uhusiano ukaja baada ya
kuonana mkafahamiana zaidi, kwani ukikurupuka na kutaka kuoana haraka
haraka na yule ambaye mna chat tu kwenye mitandao unaweza kujikuta
unajuta baadaye kwa maamuzi yako ni vyema kufahamiana zaidi ya kuchat
ili kuwa na uhakika na maamuzi yako.
Thursday, June 21, 2018
Inawezekana Kupata Mume au mke Mzuri Kupitia Facebook?
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment