Wabunge nchini Ujerumani wameidhinishwa, kwa wingi wa kura, sheria ya kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Wamefanya hivyos iku chache baada ya Kansela Angela Merkel kuondoa upinzani wake dhidi ya mpango huo.
Chini ya mabadiliko hayo sasa, wapenzi wanaotaka kuoana ambao awali
walikubaliwa tu kuwa na ushirika, hadhi ya ndoa kamili na wana haki ya
kuasili watoto.
Wapinzani wa Bi Merkel kisiasa walikuwa wanaunga mkono sana hatua hiyo.
Lakini kansela huyo, ambaye alionekana kuunga mkono kufanyika kwa kura hiyo Jumatatu, alipiga kura ya kupinga.
Mswada huo uliungwa mkono na wabunge 393, 226 wakaupinga na wanne wakasusia.
Sheria nchini Ujerumani sasa itasoma: "Ndoa inafanikishwa na watu wawili
wa jinsia tofauti au jinsia moja," shirika la habari la AFP limeripoti.
Baada ya kura hiyo ya Ijumaa, Bi Merkel amesema kwamba kwake ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke.
Lakini amesema anatumai kwamba kupitishwa kwa mswada huo kutafanikisha "utangamano zaidi wa kijamii na amani".
Wakati wa kampeni 2013, Bi Merkel alisema kwamba anapinga ndoa za
wapenzi wa jinsia moja, kwa msingi wa "maslahi ya watoto", alkini
akakiri kwamba amekuwa na wakati mgumu kuhusu suala hilo.
Thursday, June 21, 2018
Kuanzia Leo Mashoga na Wasagaji Ruksa Kuoana Katika Nchi Hii
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment