KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha
yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata
wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa
kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa kuendana nae
au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi
na mambo mengine mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana.
Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla
kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji
na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza.
Ndio ukweli wenyewe
Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata
kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume
anajikanyaga namna ya kuongea.
Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha
au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika
mapenzi.
Maneno ya kusikia kutoka kwa wanawake
Wakati wa kumtongoza mwanamke tarajia maneno kama;
1. Nina mume au mchumba
Inakuwa kuwa ni kweli au njia ya kukataa
2. Niko bize na kazi`
Hii humaanisha kwamba hana muda wa kuzungumza au hata kuonana, ni dalili pia ya kukataa au kuvuta muda ili aendelea kukutafiti
3. Nimeokoka nampenda Mungu
Hii huwa na maana kwamba yeye ni mtu asiyependa uchafu hasa kama unamtongoza kwa lengo la kufanya ngono tu
4.Mimi nasoma, sitaki hayo hadi nimalize
Sitaki! Ni kwamba anaweza kujisemea kwamba hataki uhusiano uwepo. Anaweza kueleza sababu au kutoeleza.
5. Wewe sio mwanaume wa aina yangu;
Hapo huwa mwanamke anamaanisha labda una sifa tofauti na anazotaka,
huenda wewe mwanaume ni mfupi, mweusi au tabia zingine zozote ambazo
haziendani nae.
Msingi wa kuomba urafiki
Kwa mwanamume mwenye umakini, huwa hakosi kupata anachotaka. Jiwe lake
lazima litapiga anachokitaka, hasa kama atakuwa mwenye kufanya utafiti
wa kina kabla ya kuamua kufanya kitu. Msingi sahihi wa kutongoza ni
kufanya utafiti na kuongea kwa mitego, kabla ya kumfikia msichana
unayemuhitaji.
Kwa mfano badala ya kusema twende tukale chakula cha mchana, sema
utakuwa na muda kweli tukale, au uko bize? Maana yake ni kwamba huenda
ni kweli akawa bize au la, lakini kama hataki atakwambia niko bize kama
ndivyo unaweza kumuuliza nikuletee nini ninapotoka kula. Kwa namna
anavyojibu vibaya au vizuri unaweza kupata mwelekeo wa nini unaweza
kujibiwa kama unaongea wazi unachokitaka kwake.
Wanawake wanajua fika nini ambacho mwanaume anakitaka anapoanza kuongea
hiki na kile, mara nyingi huwa wanafanya kana kwamba hawajui.
Mambo ya kuzingatia katika hatua ya uchumba
Ukweli ni kuwa uchumba ni wakati mzuri sana wa kuangaliana tabia ili
hatimaye kuwa na chaguo jema. Hata hivyo ili kuwa na uhusiano mzuri ni
lazima kufahamu kuwa wanadamu wanatofautiana, aidha kitabia au
kimuonekano. Ni lazima kujifunza namna gani unaweza kuishi na watu
wengine wenye hali tofauti.
Unaweza kuona watu wanatofautiana kitabia, huyo ni mzunguzaji sana,
mwingine ni mpole, kiasi kwamba hata ukiwa nae ni kama uko peke yako.
Kumlazimisha asiye na uwezo wa kuzungumza sana, awe mzungumzaji, sio
sahihi sana, wala kumzuia mzungumzaji asifanye hivyo, pia sio sahihi
Wachumba wanaweza kutofautiana kwa kiwango cha elimu, uchumi, ufahamu
juu ya mambo mbalimbali, kikabila, umri na hata kwa rangi pia. Kufahamu
hili ni suala la msingi sana ili kuhakikisha.
Ingawa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakilazimisha kwamba wawe wanaoana
na wale ambao ni wa kutoka kwenye madhehebu yao tu, wachumba wanaweza
wakatoka katika madhehebu/makanisa tofauti na hili ni kwa kuzingatia
madhehebu/makanisa mengi yaliyopo.
Thursday, June 21, 2018
Zifahamu Mbinu Mbalimbali za Kumpata Mpenzi Bora Katika Mapenzi
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment