Marafiki zangu tunaendelea na mada yetu ambayo kwa hakika imekuwa ndefu
lakini yenye manufaa makubwa kwenye uhusiano wetu. Nilianza kwa kueleza
kwamba yapo mambo mengi sana ambayo husababisha thamani ya mtu kushuka
kwa mpenzi wake.
Nilishazungumza mengi katika matoleo yaliyopita lakini leo nitaendelea
na kukazia zaidi kwenye athari za kuharakisha faragha. Karibu darasani.
ATHARI ZA KUHARAKISHA FARAGHA
Wiki iliyopita nilifafanua zaidi matatizo ya moja kwa moja ambayo mtu
anaweza kuyapata kwa kuharakisha faragha ambapo nilisema kwamba kuna
suala la kuchokwa na kuonekana wa kawaida.
Lingine ni kuonekana mwepesi kwenye suala la mapenzi hivyo mwanaume kuwa
na mashaka kwamba hata kama akifikia uamuzi wa kukuoa unaweza kuwa
mwepesi kutoa penzi kwa wengine kama ulivyofanya kwake. Tuangalie
vipengele vinavyofuata.
(i) Hupunguza thamani
Heshima ya penzi ni kwenye ndoa. Kuna uwezekano mkubwa sana wa kushushwa
thamani baada ya kutoa penzi. Wanaume wengi huanza kuwa wasumbufu (kama
ni kasumba yao) kwa wapenzi wao baada ya kutoka nao kimapenzi.
Pamoja na kwamba ni tendo la furaha lakini kwa mwanamke linampa unyonge
na wakati mwingine huwa mwanzo wa utumwa wa mapenzi kwa kuogopwa kuachwa
wakati tayari ameshatumika!
Hebu jiulize; utatumia/utatumika kwa wangapi? Ukifikiri kwa makini juu
ya jibu la swali hili bila shaka utabadilisha mtazamo wako.
(ii) Hupunguza msisimko
Penzi la kienyeji mara nyingi hata wahusika huwa wanajua kabisa kuwa
wanakosea. Makosa haya husababisha kupoteza msisimko wa ndani. Ni jambo
la kisaikolojia sana na huenda muathirika asigundue tatizo hili kupitia
dalili za kitaalamu atakazozionesha.
Mkishaibana huko nje huwa kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kupoteza
msisimko wa kawaida. Mfano mawasiliano hupungua, hamu ya kuonana
inapungua sana n.k
Hapa nisipoteze muda sana, wengi mnafahamu inavyokuwa; MWANAUME
AKISHATEMBEA NA MWANAMKE, TARATIBU ATAANZA KUJIWEKA PEMBENI. Kama
alikuwa anapiga simu mara nne au tano kwa siku, hupunguza idadi na
wakati mwingine hupitisha siku nzima kabisa.
Mbaya zaidi, unaweza kumpigia wewe na bado asipokee, ukituma ujumbe
mfupi hatajibu au atachelewa. Kesi nyingi sana nilizokutana nazo za
wanawake wanaolalamika wapenzi wao kubadilisha utaratibu wa mawasiliano,
baada ya kuwahoji walisema jambo hilo limejitokeza baada ya kuwapa
penzi.
MUHIMU KWAKO KUJUA
Mwanaume wa aina hii ni yule ambaye hakuwa na mpango wa ndoa baadaye au
hakuwa na uhakika na aina ya uhusiano anaotaka kwa mwanamke wake.
Sasa jiulize, ikiwa alikuwa kwenye majaribio, utajaribiwa na wangapi? Tumia hekima rafiki yangu ili kujinasua katika mtego huu.
(iii) Upungufu
Ukishautoa mwili wako kwa mwanaume, kama ni aina ya wale ambao
huchunguza sana ni rahisi kukutoa kasoro. Utamsikia akisema, aaah! Huyu
mwanamke bwana ana sijui nini...hakuna hoja za maana.
Kikubwa unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba kuutoa mwili wako hovyo
kunakupeleka kwenye kujichoresha na pengine kama umekutana na mwanaume
kicheche ataishia kukutumia na kukuacha kama alivyokukuta!
(iv) Msimamo
Pamoja na kwamba wanaume wengi ndiyo hasa wanaokuwa wa kwanza kushawishi
kupewa mapenzi, ukweli ni kwamba ni wepesi wa kulaumu (vipengele
vilivyopita nilikazia zaidi) na kuwaona wenzi wao hawana msimamo na
maisha yao.
Kukuweka kwenye kundi hilo kutakukosesha nafasi ya uhakika ya kuingia
kwenye ndoa, maana wengi wanapenda kuwa na wenzi wenye msimamo thabiti.
(v) Mimba
Kuna suala la mimba. Nimekutana na kesi nyingi sana za aina hii.
Wanaokutana kimwili na wenzi wao bila mpangilio huwa hawazingatii sana
suala la mimba lakini inapotokea ndiyo huanza kuhangaika kutafuta
ushauri.
(VI) Magonjwa
Kuharakia mapenzi kuna matatizo mengi. Ukiacha kuwa katika hatari ya
kupata magonjwa ya zinaa pia kuna suala la ujauzito. Mathalan utakuta
msichana amepata mimba isiyotarajiwa, anatafuta shotikati na kwenda
kuitoa, hapo kuna matatizo mengine mengi anayoweza kuyapata kutokana na
kitendo hicho.
Thursday, June 21, 2018
Jinsi Ya Kujiweka Wa Thamani Kwa Mpenzi Wako
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment