UHALISI WA MAISHA:
Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni
kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo
yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha
mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na
haya yafuatayo;
UVUMILIVU:
Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa
tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu,
mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au
mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa
inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako
wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko,
manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu
kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila
anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo.
UPENDO WA DHATI:
Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka.
Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi,
pesa, elimu ya juu n.k. wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na
pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo
zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa
ni Upendo wa dhati na uhalisia.
UTII KWA KWA JAMII:
Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka ili kuweza kuyafanyia
kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita
kona yoyote. Utii kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia
kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa.
UAMINIFU KATIKA JAMII:
Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii
inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu
wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na
hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida
ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake
katika sekta zote.
UNYENYEKEVU WA KWELI:
Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka,
unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza,
kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke
shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima.
UWAJIBIKAJI WA DHATI:
Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili
na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa
majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na
uwajibikaji wake.
USHIRIKIANO WA DHATI:
Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa
kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike
kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli
ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi
za kuandaa/ kujenga familia bora.
UTARATIBU WA KAZI/MPANGILIO:
Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo
yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli
zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa.
Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako
bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako.
KUFANYA TATHIMINI:
Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya katika maisha yake ya
kila siku, pengine ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima n.k kama
mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta
faida/hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka. Ukiona faida ni
kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka
katika nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza
wakati.
Wednesday, June 20, 2018
Kanuni Kumi '10' za Kuwa Mke Mwema
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment