Ndugu msomaji wa Muungwana Blog, karibu kwenye makala hii maalumu,
nimeamua kuandika habari hii ili kujaribu kupunguza mifarakano kwenye
familia zetu especially familia zenye wafanyakazi wa ndani wanaojulikana
kama house girl.
Katika mada hii nimekuwa nikikutana na maswali mengi sana ambayo mda
mwingine yalikuwa yakituchanganya hata sisi wenyewe katika kuwajibu
wahusika, maswali haya malanyingi yalikuwa yakiulizwa na akina mama.
Na kwa upande wa akina baba maswali yao sio mengi ukilinganisha na akina
mama, sasa napenda nianze kwa kusema mambo yafuatayo ili wote twende
sawa.
WAJIBU WA MWANAUME KATIKA FAMILIA:
Mwanaume anawajibu wa kutimiza mahitaji yote ya msingi katika familia
yake, moja ya majukumu hayo ni pamoja na kutoa pesa za matunzo ya
familia yake kadri ipasavyo, kuonyesha upendo wa dhati kwa mama pamoja
na watoto wake, na mambo mengineyo nk.
WAJIBU WA MWANAMKE KATIKA FAMILIA:
Mwanamke ndiye mtendaji mkuu wa familia kwa upande wa nyumbani
ukiachilia mbali ya kwamba baba ndiye kichwa cha familia, mwanamke
anamajukumu mengi kwa upande wa nyumbani moja ya majukumu yake ni pamoja
na kupika chakula cha familia, kufua nguo za mumewe pamoja na nguo za
watoto, kuakikisha nyumba pamoja na eneo linaloizunguka nyumba ni safi,
kuonyesha upendo wa dhati kwa mumewe pamoja na watoto wake, nk.
Ndugu msomaji wa makala hii, nadhani mpaka hapo tayari umeisha anza
kupata mwanga kuhusu jibu la swali la makala yetu, sasa twende kuona
wajibu wa mfanya kazi wa ndani kama house girl.
House girl wajibu wake ni kuakikisha anafanya usafi wa kuizunguka eneo
la nyumba kwa nje na kufanya usafi huo kwa upande wa ndani kwa baadhi
tu ya maeneo ya nyumba hiyo pamoja na kuwaogesha watoto, kufua nguo za
watoto, na kufanya kazi ndogo ndogo za nyumbani.
House girl hatakiwi kufanya usafi chumbani kwa mume wa mama mwenye
nyumba, house girl hatakiwi kufua au kupiga pasi nguo za mume wa mama
mwenye nyumba, house girl hatakiwi kumuandalia chakula au chai mume wa
mama mwenye nyumba, nk.
Sasa ukiona house girl anafanya kazi zote nilizosema kuwa hatakiwi
kuzifanya pindi awapo nyumbani kwako, ukiwa kama mama mwenye akili
timamu jua kabisa tayari umeamua kumuletea mumeo mke mdogo na pia
usipige kelele wala kulaumu maana jitihada zote za kumuandaa mke mwenzio
umezifanya wewe mwenyewe.
Ushauri wangu kwenu akina mama na akina dada nikwamba, hatukatai kuwa
wafanyakazi wa ndani hawafai, ila jitaidi mfanyakazi wako awe na mipaka
ya kazi, mwanaume anaamua kumuoa house girl kwa sababu yeye amechukua
majukumu yote ya mama mwenye nyumba, sasa wewe mama usianze kumtupia
maneno mtoto wa watu pamoja na mumeo maana yote hayo umeyataka wewe
mwenyewe.
Wednesday, June 20, 2018
Mama kuwa makini House Girl Yaweza Kuwa Mke Mwenzio
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment