1. CHOKOCHOKO
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye
kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume
wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa
hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.
Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba
vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake
kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake,
yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.
Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda
chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake
kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na
marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na
muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.
2. KUTORIDHIKA
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya
wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao
kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi
wake, haridhiki tu.
Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake.
Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi
mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye
awaze atapigwa mzinga.
Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi.
Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na
mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi
wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.
Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za
kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba
wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake
hamtimizii.
Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi
shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza
kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa
anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.
3. KULINGANISHA
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi
maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia
mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’
Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama
yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke
anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa
tatizo kubwa.
Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu
mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni
nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika
kumfuata yule anayemvutia.
Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna
kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije
kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume
uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.
4. KUWA TEGEMEZI
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa
kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume
wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka
kwa mwanaume.
Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya
biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa
fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini
inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.
Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na
mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha
hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia
nyumbani.
Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni,
ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau
atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa
wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.
5. KUTOKUA MUELEWA
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani
kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya
pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha
wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.
Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa
kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.
6. KUJITAPA KWA KUWA NACHO
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi
wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye
kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba
anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.
Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana
wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye.
Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia
watashindwana katika suala la kumtawala.
7. KUWA BIZE SANA
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao
wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona
mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho
kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.
Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize
na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa
kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke
mwingine ambaye hayupo bize.
Wednesday, June 20, 2018
Ukiwa na Tabia hizi 7, Lazima Mwanaume Akukimbie
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment