Huyu dada nimemfahamu miaka mitatu iliyopita.
Ni mwanasheria kwenye firm fulani jijini Dar, nilikuwa nina mpango wa
kumuoa haraka, ila mmoja wa marafiki zake wa karibu aliniambia
nijitahidi kumfahamu kwanza kabla sijaamua kumuoa nadhani alihisi kitu.
Kufahamiana naye kwa muda tukaishia kupata mtoto mmoja wa kike ambaye sasa ana miaka miwili.
Ni mwanamke mzuri sana, ni gumzo kila anapopita au kufanya kazi, hata nilitaka nitoane macho na patina mmoja wa firm yake.
Kwa kweli anaita kila jicho ana mengi mazuri, lakini pia ana mapungufu yaliyonipigisha breki kali juu ya tope.
Kwa sasa anaishi na wazazi wake, lakini mara nyingi saba tunalala
kwangu. Nafahamika kwao kama mzazi mwenza, kwetu pia kaskazini
wanamtambua.
Amekuwa ni mwepesi sana wa kupata marafiki wa kiume, ana hasira za
karibu, kujiachiachia sana kwa wanaume imekuwa sehemu ya maisha yake,
yeye anadai si wapenzi wake. Wanataniana tu hii ni moja ya sababu
iliyonizuia kumuoa.
Nilihisi kama hajiheshimu.hayuko tayari kuishi kama mke wa mtu nikadhani
nimwache kwanza ale maisha wakati nami nakula taratibu ingawa nahofu ya
magonjwa.
Simu zake sijawahi ziona hata mara moja zikiita kwa sauti toka nimfahamu.anashinda watsapp 24/7.
Facebook kwake ni kama oxgen, kila siku anaongeza wanaume, viber
anatumiwa mioyo na mikisi ya wanaume, linkedin pia hayuko mbali.
Nahisi kweli atakuwa ananipenda, lakini kwa hayo nashindwa kuji commit,
ila bahati mbaya nashindwa hata kumuacha, hasa ukizingatia nina mtoto
naye.
Yaani sijui nifanyeje, nimbwage.
Naona sio waifu matirio.
Ataniua jamani.
By Kelly
Wednesday, July 25, 2018
Anashinda Whatsapp Masaa Yote, Ila Nashindwa Kumbwaga
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment