Kwa
sasa kuna wimbi kubwa la watu ambao wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za
kiume, wengi wao matatizo yao yanatumiika kwa kubadili mfumo wa maisha
tu na wachache ambao wamejiharibu kwa kujichua na magonjwa mengine ndio
wanaweza kuhitaji matibabu ya muda fualani.
katika tafiti zangu nimegundua yafuatayo ni chanzo cha kuishiwa nguvu za kiume, changamoto ambayo imeletwa na mfumo wa maisha.
1. Msongo mkubwa wa mawazo; nguvu
za kiume na hamu ya kushiriki tendo hili huanzia kichwani mpaka kwenye
uume wa binadamu, watu wenye misongo ya mawazo sababu ya kushindwa
kutimiza wajibu wao wa kazi waliopewa kwa wakati, misongo ya mawazo
sababu ya majukumu makubwa ya kifamilia ambayo yanakuja na huenda hakuna
fedha za kukabiliana na hali hizo, msongo wa mawazo wa biashara
zinazoyumba humfanya mwanaume asiweze kushiriki kabisa tendo la
ndoa...omba msaada kama kazi zimekuzidi tafuta msaidizi kama
umeajiajiri, kama waliokuajiri hawakuelewi tafuta kazi nyingine na
uachane na hiyo kazi ya kufanya kazi usiku mpaka usiku lakini pia muda
wa kazi ukiisha undoka kwenda nyumbani haraka kwenda nyumbani hakuna
sifa ya kufanya kazi masaa mengi wakati mahusiano yako yanakufa.watu
wanaofanya kazi benki ni wahanga sana wa matatizo haya.
lakini pia dawa zinazotolewa kutibu msongo wa mawazo huharibu nguvu hizi za kiume pia.
2. Ulevi wa kupindukia; unaweza
kua unapenda kunywa pombe angalau kustarehe na kuonana na ndugu na
jamaa lakini unywaji wa pombe kupitiliza ni hatari sana, humaliza nguvu
za kiume na kukosesha hamu. habari njema ni kwamba pombe kidogo angalau
pia moja mpaka mbili kwa siku ni nzuri kwa nguvu za kiume na afya ya
moyo.
3. Dawa mbalimbali; baadhi
ya dawa zinzotumika kwa shida mbalimbali au magonjwa mbalimbali
zimethibitika kupunguza nguvu za kiume hasa zile zinazomezwa mara kwa
mara au kila siku mfano dawa za presha, dawa za maumivu na dawa za
msongo wa mawazo.
kumbuka
usiache dawa kama una ugonjwa unaohitaji dawa kila siku sababu umesoma
hapa, kwa upande mwingine uhai unaweza kua muhimu kuliko nguvu za
kiume.
4. kufikiria sana; huwezi
kupata nguvu za kiume kama unafikiria mambo mengi yanayokuathiri labda
maumivu ya vifo ya wapendwa, maumivu ya kuachishwa kazi, maumivu ya
kusalitiwa na mpenzi au kuachwa, na uchovu sana wa shughuli za kila
siku. jaribu kurelax, kukubali matokeo, kupata usingizi wa kutosha na
kushiriki mazoezi na kumbuka mazoezi yakiwa makali sana humaliza nguvu
za kiume.
5. Hasira; hasira
juu ya mwenzi wako au mtu yeyote aliyekukwaza hufanya ushindwe
kushiriki tendo la ndoa, hakikisha unamwambia mpenzi wako mambo
yanayokukwaza...kuyaweka moyoni haitakusaidia hata kidogo.
6. Wasiwasi; wanaume
wakishapata matukio kadhaa ya kuadhirika na kushindwa kufanya tendo la
ndoa huanza kuogopa kukutana tena na mwanamke kwa hofu kwamba
wataadhirika tena...tafuta chanzo ni nini na urekibishe, huenda siku
hiyo haukua vizuri au ulikua na njaa...kisha jiamini kwamba sasa
ntafanikisha.
7. Vitambi na unene; vijana
wengi kwanzia miaka 30 mpaka 40 hilo ndio tatizo lao kubwa, yaani
kukosa nidhamu ya kupambana na ungezeko la miili yao na matokeo yake
uume hua mdogo na nguvu kidogo sana lakini pia ulaji wa vyakula vya
haraka kama chips na mikaango mbalimbali wakati wa kazi na kusahau
vyakula asilia kama mihogo,karanga, ugali,wali, matunda na mboga za
majani...asikudanganye mtu kama umeshindwa kupungua uzito nguvu za kiume
utazisikia redioni.
8. kutojiamini; baadhi
ya wanaume hushindwa kujiamini kwa kujikosoa vitu mbalimbali vilivyoko
kwenye miili yao ambavyo wakati mwingine hata mwanamke mwenyewe havijali
sana mfano kuhisi ana uume mdogo sana wakati uume wake ni wa kawaida,
kuhisi hana mwili mzuri na kadhalika.
9. Kukosa hamu ya tendo la ndoa; kwa
maisha ya sasa hii husababishwa na kuchoka sana na kazi na kukosa muda
wa kupumzika, kuna watu wanafanya kazi kila siku ya maisha yao kwa madai
wana roho za kichaga...hizo pesa unazotafuta huku unaharibu afya
hazitakusaidia kwa lolote hata ukizipata mwisho wa safari na utaibiwa
mke na walafi wa mtaani.
10. Magonjwa; haya
ni magonjwa mbalimbali ambayo hua hayaponi au huchukua muda sana kupona
kwa namna moja au nyingine huharibu nguvu za kiume moja kwa moja mfano
kisukari, presha, ajali za migongo na magonjwa ya mishipa ya fahamu,
madonda ya tumbo, kifua kikuu, pumu na kadhalika...
Mwisho; unaweza
kua unaona aibu kuongea na daktari kuhusu tatizo lako lakini kimya
chako hakitakusaidia, jaribu mwenyewe kufikiri chanzo ni nini ili uweze
kubadili mfumo wako wa maisha kama kupunguza uzito, kupunguza kazi na
kuishi kwa uwezo wako wa kifedha,kuacha kutumia dawa zinazoharibu nguvu
zako, kupunguza ulevi na hata kupata matibabu kama ikionekana ni muhimu.
Wednesday, August 8, 2018
Ujue Mfumo Unaosababisha Tatizo la Nguvu za Kiume
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment