Wakuu nilikutana na huyu binti miaka kadhaa iliyopita mimi nikiwa
nimepangiwa kazi mkoa fulani katika mihangaiko yangu nikakutana na huyu
binti nilitokea kumpenda, mzuri kisura na kitabia very innocent
niliamini kwake nimefika baada ya kash kash nilizopitia katika mahusiano
ya nyuma.
Wanasema usiusemee moyo ila najua yule binti alinipenda kidhati tena
moyoni kabisa na mimi kwangu she was a queen na niliapa kumuoa baada ya
yeye kumaliza masomo yake. Binti huyu kwao ni familia maskini nikisema
familia maskini ni familia maskini kisawasawa. Baba yake alifariki miaka
kadhaa nyuma kabla sijaonana nae hivyo aliishi na mama yake na wadogo
zake ni story ndefu kuhusu familia yao. Mimi nikawa ndio kama msaada
katika familia yao, sikua na hiyana na nilisaidia niwezavyo kwani binti
yule nilimpenda kutoka moyoni.
Yule binti alimaliza shule na kuhitajika kwenda chuo lakini familia
ikawa haina uwezo wa kumsomesha na mkopo alikosa. Akakosa raha na ikawa
kama jukumu ni langu. Mama yake aliniita tushauriane kwasababu kwao
nilikua nafahamika. Kwakuwa mimi nilisema nitamuoa binti wakashauri
nimsomeshe kama nina nia yakweli. Uwezo wa kumsomesha nilikua nao
nikakubaliana na tukaandikishana kwamba namsomesha mimi lakini mwisho wa
siku yeye atakuja kuwa mke wangu na hata mahari sintolipa kwani itakua
imeingia huko.
Familia ilinishukuru sana kwani waliamini kusoma kwa binti itakua
afadhali katika ukombozi wa maisha yao. Binti alikuwepo wakati
maandikishano yanafanyika na mashahidi walikuwepo nakumbuka binti alilia
yule akiapa kunipenda milele na mapenzi tuliyofanya siku hiyo siwezi
kusahau ilikua best sex ever.
Wakuu nifupishe binti alianza chuo kila kitu nililipa nauli hosteli ada
matumizi kila kitu ilikua mimi,mwaka wa kwanza ukaisha vizuri mapenzi
yanachanua.Likizo naenda likizo zao anakuja, mama mtu alinishukuru sana.
Mwaka. Mwaka wa pili matatizo yakaanza nikipiga simu naambiwa yuko
library mara assignment nikiuliza zaidi anakua mkali nikasema labda
labda kweli shule lakini hata mimi nilisoma muda wa kuongea na mwenzi
wangu nilikua nao nikasema labda shule ya sasa ni ngumu. Binti
akabadilika majibu ya jeuri nikaenda kuongea na mama yake amkanye naona
akajirekebishe na kweli akatulia maisha yakaendelea. Upside zikiwa
chache. Mahusiano yalitawaliwa na migororo
Kufupisha Miezi kadhaa imepita binti kaniandikia meseji eti "NAKUSHAURI UTAFUTE MWANAMKE MWINGINE MIMI SIKO TAYARI KUWA NA WEWE NIKUTAKIE MAISHA MEMA"
Naandika huu uzi wakuu acha nikipiga simu haipokelewi mara haipatikani.
Nikampigia mama yake kumuuliza kama anajua lolote akasema hafahamu.
Nikaomba likizo kazini nifatilie sikuamini siku naambiwa ana mimba na
anaishi na mwanaume mwingine. Nilitamani ardhi ipasuke kumbe ndio maana
niliandikiwa ule ujumbe nikajiuliza maswali bila majibu,basi angefanya
nisijue na mimba juu kapata inauma sana. Kumuuliza mama yake hana
analonijibu, kumbe chuo kapostpone sijui anaishi na huyo mwanaume moja
ya mitaa Dar, yote hiyo nafatilia kwa baadhi ya marafiki zake na kibaya
zaidi huyo mwanaume alishamlipa tena huyo mama pesa nyingine. Na ndio
kamchukua binti yake.
Nimechukia kuuziwa mbuzi kwa gunia.Love is blind inakuwaje sikuona yote
hayo? Why me..Why.. Najiuliza sipati majibu, sikuwahi kupenda kama
nilivyompenda huyo binti. Nilimpenda kutoka moyoni na kujitoa kwake
sijawahi kumfanyia mwanamke yoyote niliyomfanyia leo ameniacha kwenye
mataa na nyodo juu, kuna muda natamani ningekuwa na bastola
nimsambaratishe ila that is not me. Juzi nimeona whatsup kaweka picha
yake tumbo kule na namba yake nikafuta.
NILICHOFANYA;
Nimepeleka hii kesi Mahakamani kwasababu tuliandikishana kama mke
nimekosa basi nilipwe gharama zangu najua haiwezi kuziba pengo kufuta
maumivu naona is the least i can do for my self. Wakuu nifanyaje au
nimekosea kupeleka shtaka polisi tumeshaitwa mara mbili hakuna mtu
aliyetokea upande wao. Nimetokea kuwachukia wanawake sana. Kwanini
mnatufanyia hivi jamani tuwapende vipi. Nimekaa hapa kitandani nimewaza
mawazo mengi moyo wangu kama barafu naishia kusononeka.
Sijui nimfanyie kisasi gani aumie kama mimi nilivyoumia.
Wednesday, September 26, 2018
Nimemsomesha, Nimegharamika, Leo Kaniacha Anaolewa na Mtu Mwingine
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment