Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi-Unguja linawashikilia watu 20,
ambao ni wanawake(12) na wanaume(8) kwa tuhuma za kukutwa wakifundishana
kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharib, Hassan Nassir
amesema watu hao wamekamatwa wakati wakipatiwa mafunzo ya namna ya
kuzitambua haki zao yaliyokuwa yakitolewa na taasisi iliyotambulika kwa
jina la Bridge Initiative.
“Ni kweli tuliweza kuwakamata kwa sababu walikuwa wakishiriki katika
mapenzi ya jinsia moja kitu ambacho ni kinyume na sheria kisiwani
zanzibar na ni ukiukaji wa sheria za Tanzania”, alisema Hassan pia
akaongeza kuwa polisi wataongeza doria zao dhidi ya makundi kama hayo.
Mwezi michache iliopita Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed
alitangaza vita kwa wanaojihushisha na biashara hiyo haramu na alipiga
‘stop’ taasisi zinazofadhiri watu hao.
Wednesday, September 26, 2018
Watu 20 Wanaojihusisha na Mapenzi ya Jinsia Moja Wakamatwa Zanzibar
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment