Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Saturday, April 29, 2017

HII NDILO SULUHISHO PEKEE LA KUNUKA MDOMO { BAD BREATH}



                
Watu wengi hawawezi kujua harufu zao za mdomo. lakini harufu za midomo yao ziko wazi kwa watu wengine wanaowazunguka..
Sio rahisi muhusika kufahamu kama ana tatizo hili mpaka aambiwe na wanao mzunguka.
Mtu akishafahamu ana tatizo hili hupata hofu sana na huathirika sana kisaikolojia kwa kuwaza kwamba jamii inamchukuliaje..
Sababu zifuatazo zinaweza kumfanya mtu awe na harufu kali ya mdomo..
  • ·         Vyakula na vinywaji:
Pombe na  vileo vingine huacha mabaki mdomoni ambayo huleta harufu kali ya mdomoni pia vyakula vyenye wingi mkubwa wa madini ya sulphur kama nyama, samaki vinapomeng’enywa sulphur hyo husafiri kwenye damu mpaka kwenye mapafu na kutoa harufu ambayo si ya kawaida. Harufu hiyo huweza kudumu kwa masaa 12 mpaka 24.
  • ·         Kitu chochote kinachokausha mate mdomoni:
Mzunguko wa mate mdomoni huzuia bacteria wa mdomoni kukua .
Mdomo unapokauka mfano wakati wa kulala bacteria hao huazaliana haraka kula mabaki mdomoni na na kuacha harufu kali inayopatikana wakati wa kuamka.{morning breath}
Dawa pia zinazokausha mate mdomoni kama furasamide, amitripline na piriton huweza kuleta hali hiyo.
Pia mtu anavyozidi kua mkubwa kiumri uzalishaji wa matemdomoni  unapungua na ii ndo sababu watu wengi wazee wananuka midomo.
  • ·         Magonjwa:
Magonjwa kama kisukari, kifua kikuu,baadhi ya kansa, na magonjwa ya ini huleta harufu kali ya mdomoni.
  • ·         Uvutaji wa sigara na kutopiga mswaki:
Kawaida mtu anatakiwa apige mswaki kila anapomaliza kula yaani kama asubuhi mtu anatakiwa anywe chai kwanza ndio apige mswaki na milo mingine ivoivo.
Pia sigara huacha mabaki yanayofanya mdomo ue na harufu mbaya.
VIPIMO VINAVYOFANYIKA HOSPITALI:
Historia ya mgonjwa inaweza  ikamfanya daktari akatambua chanzo cha harufu ya mgonjwa kama nilivyotaja hapo juu.
Pia kuna baadhi ya vipimo huweza kupimwa kugundua magonjwa flani. Mfano
  • ·         Kupima kikohozi kuangalia wadudu wa kifua kikuu.
  • ·         Kupima damu kama mgonjwa ana kisukari.
  • ·         Uwezo wa figo na maini.{liver and kidney function test}
Wakati mwingine vipimo vinaweza kushindwa kugundua chanzo cha ugonjwa husika.
MATIBABU:
Daktari akishafahamu chanzo cha ugonjwa ni rahisi kuutibu kirahisi.
Mgonjwa anaweza kusafishwa kinywa na daktari wa meno na kuanzishiwa matibabu mengine kulingana na ugonjwa husika.{scaling}
Matibabu mengine:
·          Usafi wa kinywa ni muhimu kwa ajili ya afya ya meno na kinywa kwa ujumla, ni vizuri kupiga mswaki kila baada ya mlo na kumuona daktari wa meno kila baada ya miezi sita.
Kama huwez kupiga mswaki kama hivyo ni bora ata kuosha mdomo tu na maji baada ya kula.
·         Ulimi unaweza kusababisha harufu kali mdomoni, hivyo usiusahau wakati wa kupiga mswaki.
·         Tumia viosha mdomo mara chache kuua bacteria hatari mdomoni.{ mouth washes}
·         Kunywa maji mengi kama glasi nane kwa siku, juice au tafuna jojo kuongeza mzunguko wa mate mdomoni.
                      Nakutakia afya njema wewe na familia yako..

No comments:

Post a Comment