Makala zilizopita zimetaja njia nyingi za uzazi wa mpango
ambazo zinaweza kutumika kupanga uzazi kwa mwanamke ikiwemo faida zake na
hasara zake.
Leo katika mtiririko wa njia za uzazi wa mpango tutaongelea
njia ya kuzuia mimba kwa kunyonyesha mtoto
mdogo baada ya kujifungua.
Njia hii inafanyaje
kazi?
Tafiti zinaonyesha kwamba mama baada ya kujifungua huchelewa
kupata siku zake za mwezi na kipindi hiki kunakua na homoni nyingi kitaalamu
kama prolactin hormone ambazo hufanya
kazi kinyume na homoni za uzazi yaani progesterone na oestrogen ambazo ndizo
chanzo kikuu cha kuruhusu yai kwa ajili ya kutunga mimba.
Homoni hii ya prolactin kazi yake kubwa ni kuruhusu
utengenezwaji na kuruhusu maziwa ya mama kutoka ili mtoto anyonye..
Uhakika wa njia hii..
Njia hii ina uhakika wa kufanya kazi kwa asilimia 98 bila
kusababisha ujauzito kwa mtu anayeitumia ila tu afuate masharti yote
yanayohusika na njia hii ya uzazi wa mpango.
- · Mtoto awe ananyonya maziwa ya mama tu: kunyonya huku ndo kutafanya homoni hii ya prolactin kuendelea kuzuia hizi homoni zingine za uzazi kufanya kazi, hivyo mama anashauriwa amnyonyeshe mtoto wake angalau kila baada ya masaa manne.
- · Mama awe hajaona siku zake kabisa baada ya kujifungua: kama mama ameshaona siku zake ni dalili ya wazi kwamba homoni za uzazi zimeanza kazi hivyo asitumie kabisa njia hii.
- · Miezi sita iwe haijapita baada ya kujifungua: baada ya miezi sita kuna uwezekano mkubwa wa homoni za uzazi kuanza kazi hivyo kama miezi sita imepita mama anashauriwa atumie njia zingine za uzazi wa mpango kama kondomu.
Madhara ya njia hii…
·
Njia hii haina madhara yeyote kiafya ila
hutegemea sana unyonyeshwaji wa mtoto hivyo mama akizembea kunyonyesha kama alivyoelekezwa
anaweza kubeba mimba nyingine..
No comments:
Post a Comment