Katika moja ya makala zilizopita tuliwahi kuongelea dalili
muhimu za kifo ambazo ukiziona kwa binadamu yeyote kuna uwezekano mkubwa wa kua
amepoteza maisha tayari..
Lakini pia kabla binadamu yeyote ambaye alikua anaumwa
hajafa kuna hatua kadhaa za kisaikolojia ambazo lazima azipitie kabla ya
kupoteza maisha kabisa..
Zifuatazo ni hatua hizo muhimu…
Rejection: hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo mgonjwa
mfano anasumbuliwa na kansa labda ya damu akiambiwa kwamba atakufa, hukataa
kabisa na hatakubaliana na kauli za madaktari au ukweli halisi kwani anaamini
bado atapona japokua ugonjwa wake hautibiki..
Anger: hii ni hatua ya pili ambayo mgonjwa ameshagundua
kabisa kwamba atakufa lakini matokeo yake hua na hasira sana, kujutia nafsi
yake hata kumlaani mungu na baadhi ya watu ambao binafsi anahisi wamehusika
na kifo chake.
Depression; hatua hii
ya nne mgonjwa hukata tamaa kabisa na kua na mgandamizo mkubwa wa mawazo, mara
nyingi hua haongei tena huku akitumia mda mwingi kutafakari labda huko kaburini
kukoje, itakuaje ndugu zake na familia kwa ujumla siku kifo kikifika, kama kuna
maisha mengine baada ya kifo na kadhalika.
Acceptance: hii ni hatua ya mwisho ambayo mgonjwa
hukubaliana na ukweli wa mambo kwamba lazima afe hata iweje. Kipindi hiki
mgonjwa hua na furaha kama kawaida na mara nyingi hupenda kuomba aletewe
viongozi wa kiroho ili wamuombee huku aendako, pia huanza kuandika urithi na
kuweka mambo yake sawa kabla ya kifo.
No comments:
Post a Comment