Habari za zenu ndugu wasomaji, natumaini mnaendelea na
shughuli zenu za kila siku kama kawaida.
Katika mtiririko wetu wa makala za uzazi wa mpango, leo
tutaongelea uzazi wa mpango kwa mwanaume.
Watu wengi hua hawajui kama mwanaume pia anahusika pia
kufungwa mirija kama ilivyo mwanamke ili asiweze kumpa mimba mwanamke tena na
baada ya hapo kuishi maisha ya kawaida kabisa..
Njia hii ni imekua ngumu kidogo kupokelewa kwa tamaduni za
kiafrika labda kwa sababu ya imani zilizopo na wanaume kutoathirika moja kwa
moja na tatizo la kubeba mimba nyingi..
Jinsi ya kufanya upasuaji..
Upasuaji huu hufanyika kwenye korodani na mirija inayopeleka
mbegu za kiume kutoka kwenye korodani kwenda kwenye uume kitaalamu kama vas deferens
hukatwa kabisa kuzuia mfumo huo wa uzazi..
Mwanaume huweza kuendelea na shughuli zake za kawaida baada
ya wiki moja tu.
Madhara ya njia hii ya uzazi wa mpango..
Yapo madhara madogo madogo ya njia hii ya uzazi wa mpango
kama kutokwa na damu, maumivu, na kidonda kuchelewa kupona kwasababu ya
kuingiliwa na bacteria{ infection}.
Lakini madhara haya haya huweza kutibika kirahisi sana..
Baada ya upasuaji
Upasuaji huu ni wa moja kwa moja yaani hautaweza kumpa
kwanamke mimba tena hivyo ni vizuri kua na uhakika kabla hujaamua kushiriki
njia hii,
Ni nchi chache zilizoendelea zilizofanikiwa kurudisha mirija
hiyo tena lakini bado uwezekano wa kumpa mwanamke mimba unakua chini yaasilimia
55.
Mwisho; hii ni moja ya njia bora za uzazi wa mpango ambazo
hazina madhara kabisa kiafya na huweza kutumika mda na wakati wowote muhusika
anapokua tayari.
No comments:
Post a Comment