Najua wengi wenu mnahisi au mnadhani mnajua sana kutumia
condom kuliko kawaida lakini leo naomba niwakumbushe kutumia zana hii na
kuwaamsha ambao hawazitumii kabisa.
Pia natoa rai kwamba
condom inazuia magonjwa hatari na mimba ambazo hazikutarajiwa…
Hebu tuone condom ya kiume inavaliwa vipi..
- 1. Hakikisha condom yako haijaisha mda wake wa matumizi yaani expire date, kwan condom iliopitwa na wakati hua inashuka kiwango na uwezo wa kukulinda unakua mdogo sana.
- 2. Fungua taratibu condom yako kwa kuikata sehemu laini ya juu bila kutumia kucha au wembe isije ikaipasuka.
- 3. Toa condom yako na kwa umakini mkubwa jiandae kuivaa.
- 4. Anza kuvaa condom kwa kuweka juu ya kichwa kisha bana chuchu ya condom ili kutoa hewa{kutofanya hivi ndio chanzo cha kupasuka kwa condom nyingi}
- 5. Kisha ivishe juu ya uume uliosimama na ujiandae kuivaa kwa njia ya kuivingirisha kwenda chini. Ishushe condom mpaka chini kabisa ya uume tayari kwa tendo la ndo
- 6. Sasa uko tayari kushiriki tendo la ndoa bila wasiwasi wowote.
- 7. Ukishamaliza kutumia condom vua haraka kabla uume haujalala kisha weka vizuri na kutupa kwenye ndoo ya taka au choo cha shimo..
No comments:
Post a Comment