Nguvu za kiume ni nini? Huu ni uwezo wa mwanaume
kusimamaisha uume wake na kustahimili kwa mda mrefu wakati wa faragha bila
wasiwasi wowote…
Kama nilivyoongelea kipindi cha nyuma wanaume wengi
wanasumbuliwa na tatizo hili kadri miaka inavyozidi kusonga mbele.
Idadi kubwa ya watu wamaekua wakihangaika sana na
kudanganywa na waganga wa kienyeji kwamba watapona kabisa.
Lakini kuna sababu kadhaa za kibinadamu ambazo uchunguzi wa
kitaalamu unaonyesha zinasababisha tatizo hilo kama ifuatavyo…
·
Uvutaji wa sigara:
Hii ina kimelea cha kemikali kwa jina la
nicotin ambacho huharibu mishipa ya damu na ile ya fahamu na kukufanya kua
mlegevu kabisa wakati wa tendo la ndoa…
·
Ulevi uliopitiliza:
Unywaji wa pombe sana huharibu mishipa ya
fahamu yote ya binadamu, ndio maana mtu akishalewa hata akiumia hasikii
kwasababu kwa kipindi kile mishipa hiyo ya fahamu haifanyi kazi sawasawa.
·
Kutokufanya mazoezi:
Mwili untegemewa kua safi sana pale damu
inapozunguka kila sehemu na kusafisha kila kitu ikiwemo na sumu za vyakula
tunavyokula. Usafi huu hufanya mwili kua safi kila Nyanja ikiwemo na nguvu za
kiume hivyo kama hufanyi mazoezi huwezi kupata faida hizi.
·
Uzito uliopitiliza:
Kwa jamii zetu za kiafrika kitambi ni kama
sifa, lakini naomba nikwambie mtu mwenye kitambi ni mgonjwa na husumbuliwa sana
na tatizo la nguvu za kiume kwani uzito alionao humchosha sana na kulala akiwa
hoi.
·
Kufanya ngono mara kwa mara na upigaji wa
punyeto:
Hamu ya kulala na mwanamke ni kama ulaji wa
chakula, tunaamini mtu mwenye njaa kali ndio atakula sana. Hivyo ukifanya ngono
na kupiga punyeto mara kwa mara hutakua na hamu ya ngono na nguvu za kiume hutaziona
kabisa.
·
Maumivu makali ya mwili na mgandamizo wa mawazo:
tendo la ndoa ni la starehe hivyo linaenda
vizuri mwili ukiwa safi kabisa bila shida yeyote . kama unasumbuliwa na maumivu
ya mwili ya aina yeyote ile au maumivu ya kisaikolojia kama kuachwa, kufiwa au
kukosa kazi basi hautakua na nguvu za kiume za kutosha.
·
Njaa wakati wa tendo la ndoa:
Najua watu wengi watashangazwa na hii
pointi, lakini napenda ujue kwamba mwili wa binadamu unajua kutoa vipaumbele. Kama
una njaa sana mwili hautahangaika na nguvu zako za kiume kwasababu kuna mambo
mengi muhimu ya kufanyika kwenye ubongo.
·
Kulala na mwanamke mchafu na ambaye humpendi:
Naomba utambue kwamba nguvu za kiume si
mwili tu, bali hata saikolojia..
Nguvu za kiume huambatana na mapenzi kutoka
moyoni kwenda kwa mwanamke husika na usafi wake binafsi. Usitegemee kulala na
mwanamke huku umeshika pua kuzuia harufu kali afu upate nguvu za kiume.
·
Ugomvi wa mara kwa mara na mwenza wako:
Kama mahusiano yako na mwenza wako yana
matatizo kimsingi mtakua mnaingia faragha na vinyongo moyoni , hali hii
hupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa na kuendelea kuishiwa nguvu za kiume.
·
Kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume hovyo:
Dawa za kuongeza nguvu za kiume kama Viagra
zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya watu flani na humezwa chini ya usimamizi wa
daktari. Wewe unayezimeza hovyo unakosa imani na nguvu zako kiasi kwamba
ukizikosa dawa hizo hufanyi kitu kabisa.
No comments:
Post a Comment