Miaka inavyozidi kwenda mbele uhuru wa binadamu unaongezeka
sana kutokana na sera za demokrasia na kudidimia kwa maadili ya kidini, hivyo
kuwapa watu nafasi kubwa ya kuingia kwenye mahusiano mapema.
Hali hii pia imechangia kwa ongezeko la kuumizwa kimapenzi
kwa watu wengi sana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo tamaa za fedha,
usaliti,umbali kati ya wapenzi, shinikizo la wazazi, utofauti wa dini, mitazamo tofauti kati ya
wapenzi na kadhalika.
Madhara makubwa sana yamekua yakisababishwa na hali hii ya
kuachana ikiwemo watu kujiua hasa vijana, kuathirika kisaikolojia, kufeli
mitihani, kuacha kazi na kupoteza muelekeo wa kimaisha kabisa.
Leo naenda kuongelea jinsi ya kumsahau mpenzi wako uliye
achana naye na kuanza maisha mapya yenye furaha na amani kama zamani..
Usiyazuie machozi yako:
Usiyazuie machozi yako:
Maumivu haya yatakufanya ulie sana na kujilaumu kwanini
ulipenda lakini ni vizuri kulia sana kadri unavyoweza kwani hii itakupa ahueni
na kupunguza maumivu makali unayoyapata.
Futa namba zake:
Kuendelea kua na namba zakekutakufanya uendelee kumpigia ili
abadilishe mawazo yake hii itakufanya uumie zaidi hasa kama hakutaki tena na
huenda ana mtu mwingine badala yako. Hata kama umezikariri kichwani usiziandike
tena kwenye simu yako.
Kua bize na mambo mengine;
Fanya mazoezi, katembelee sehemu ambazo hujawahi kwenda na
rafiki zako, angalia filamu za mapigano, sikiliza miziki isiyohusiana na
mapenzi. Hii itakufanya usahau mapema kuliko kukaa nyumbani peke yako na kuwaza
sana kuhusu mpenzi wako.
Usifiche hisia zako:
Kama umeachwa usione aibu, ongea na ndugu na jamaa zako na
uwambie ukweli kuhusu yaliyokutokea, hii itakufanya upunguze mzigo wa nawazo
kichwani kwako na utahisi hali ya wepesi moyoni mwako hasa kwa ushauri
utakaopata. Pia unaweza kuwaona wataalamu wa ushauri kwa ushauri zaidi.
Usitafute mpenzi mwingine kuziba pengo lake haraka.:
Watu wengi huchukua wapenzi wapya haraka ili kuzuia maumivu
lakini hii sio njia sahihi kwani siku maumivu yako yakiisha utagundua
kwamba hauna
mapenzi ya kweli juu ya huyu mpenzi wako mpya na utaishia kumuumiza tena
huyo uliyemchukua.(mwanamke anaweza kujifunza kumpenda mtu lakini
mwanaume asipokupenda mwanzoni hawezi kujifunza kukupenda hata iweje)
Andika mapungufu yake kwenye karatasi:
Jaribu kukumbuka matatizo na mapungufu ya huyo mpenzi wako
hii itakufanya uone kwamba hakuna madhara uliyoyapata ila faida na
itakupunguzia machungu yako.
Msamehe mpenzi wako ata kama hajakuomba msamaha:
Njia pekee ya kua huru kihisia ni kusamehe, visasi moyoni
havitakusaidia kabisa kuondokana na maumivu na utajikuta unawaza kufanya mambo
ya ajabu ambayo yanaweza kukuletea matatizo ikiwemo kumuua au kumjeruhi.
Kaa mbali na vitu vinavyokukumbushia kuhusu mpenzi wako:
Sikiliza nyimbo mpya, weka mbali picha zake na zawadi zote
alizokupa, usitembelee sehemu ambazo zinakukumbusha kuhusu yeye. Kua na
marafiki wapya ambao hawakumfahamu mpenzi wako.(simaanishi uwaache marafiki wa
zamani), pia usijaribu kua rafiki wa mpenzi uliyeachana nae kwani utajikuta unaumia zaidi labda baadae sana ukishasahau.
Usiseme mabaya kuhusu mpenzi wako au familia yake:
Hii ni hali ya mpito tu, ukianza kupost vitu vya ajabu
kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano yako haitakusaidia kitu bali
kujiabisha kwa jamii na siku maumivu yakiisha utajuta sana kwanini uliandika
mambo hayo. Hili ni tatizo sugu kwa watu wengi walioachana kupost vitu kama
kumkomesha mpenzi wake wa zamani. Naomba nikwambie mapenzi hayana kisasi kama
umeachwa, umeachwa tu. kumbuka silence is the best weapon..
Fikiria faida za kuishi bila mpenzi:
Kua peke yako kuna faida nyingi ikiwemo kua huru na maamuzi
yako, kuchagua marafiki unaotaka, kujikinga na magonjwa ya zinaa,kuishi maisha unayotaka bila kuhofia
kukosolewa, unaweza kuzima simu yako ata wiki nzima bila hofu, kulala peke yako
bila bugudha, kupunguza msongo wa mawazo ambao hutokana na ugomvi wa mara kwa
mara.
tumia dawa za kupunguza mawazo; wakati mwingine maumivu ya kuachana na mpenzi yanaweza kua makali sana, mtu akshindwa kupata usingizi, kufanya kazi zake, kukosa furaha kabisa na kulia kila siku. hii huathiri sana mfumo wa maisha husika na huweza kusababisha mtu kuamua kujiua kabisa kama mnavyosikia watu waliojiua sababu ya mapenzi. ndio maana kuna dawa maalumu za watu wenye msongo wa mawazo. ukitumia dawa hii mwili unatulia na ubongo unapumzika sana. itakupa usingizi na kila ukiamka unakua na furaha upya na unaendelea na maisha yako kama kawaida. dawa hizi zinaharakisha sana kusahau na kuendelea na maisha yako haraka kuliko kujaribu kupambana mwenyewe.mfano wa dawa hizo ni bupropion,clomipramine na doxepin. zinapatikana maduka makubwa ya madawa kwa gharama kubwa kidogo lakini ni bora kuliko kuendelea kupoteza muda kumuwaza mtu ambaye hakutaki tena kwani hiyo ni gharama kubwa zaidi.
tumia dawa za kupunguza mawazo; wakati mwingine maumivu ya kuachana na mpenzi yanaweza kua makali sana, mtu akshindwa kupata usingizi, kufanya kazi zake, kukosa furaha kabisa na kulia kila siku. hii huathiri sana mfumo wa maisha husika na huweza kusababisha mtu kuamua kujiua kabisa kama mnavyosikia watu waliojiua sababu ya mapenzi. ndio maana kuna dawa maalumu za watu wenye msongo wa mawazo. ukitumia dawa hii mwili unatulia na ubongo unapumzika sana. itakupa usingizi na kila ukiamka unakua na furaha upya na unaendelea na maisha yako kama kawaida. dawa hizi zinaharakisha sana kusahau na kuendelea na maisha yako haraka kuliko kujaribu kupambana mwenyewe.mfano wa dawa hizo ni bupropion,clomipramine na doxepin. zinapatikana maduka makubwa ya madawa kwa gharama kubwa kidogo lakini ni bora kuliko kuendelea kupoteza muda kumuwaza mtu ambaye hakutaki tena kwani hiyo ni gharama kubwa zaidi.
Amini utapata mwingine;
Katika dunia hii hakuna mtu alizaliwa kwa ajili ya mtu fulani..kila
mtu anaweza kutengeneza mahusiano na mtu yeyote Yule na yakawa mazuri..jipe mda
wa kutosha usiwe na haraka fanya mambo yako.. BELIVE ME, ANOTHER TIME WIL
COME..NEW LIFE, NEW LOVE AND NEW HAPPYNESS.
No comments:
Post a Comment