Ujauzito ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kubeba kiumbe
kwenye mfuko wake wa uzazi, dalili za ujauzito wakati mwingine huweza
kuchanganya watu na magonjwa mengine kama malaria na magonjwa ya njia za mkojo
hasa mwanzoni mwa ujauzito, lakini pia kuna watu hawazipati dalili hizi na
kushtuka mimba ikishakua kubwa kabisa.
Mimi kwa uzoefu wangu nimeshakutana na wanawake watatu
katika vipindi tofauti wakiwa na ujazito wa miezi sita bila wao kujua wakihisi
ni unene tu..
Dalili za ujauzito husababishwa na kuongezeka kwa kwa
hormone za uzazi ndani ya mfumo wa damu wa mwanamke..lakini kabla ya kwenda
kuhakikisha ujauzito na vipimo vitu vifuatavyo huonekana kwanza kwa mwanamke
husika..
·
Kukojoa mara kwa mara
·
Kutoona siku za hedhi
·
Kichefuchefu na kutapika
·
Matiti kuuma na kuvimba
·
Kuchoka sana bila kazi
·
Kupoteza hamu ya kula
·
Kupata hasira au furaha ndani yam da mfupi.{mood
swings}
·
Kizunguzungu
·
Kuongezeka joto la mwili.
·
Kuongezeka kwa uwezo wa kunusa harufu.
No comments:
Post a Comment