''Mjuzi wa kutongoza ni mtanashati, mtaalam wa kutongoza ni msafi na tofauti na unavyofikiri, mara nyingi mjuzi wa kutongoza
sio sharobaro na wala sio kwamba anamistari mikali saana, sema ni
mcheshi na anajua kusifia pale panapohitajiwa kusifiwa na anajua kuongea
pale neno linapotakiwa kuongelewa!''
Kila mtu anauwezo wa kumtongoza msichana tatizo lazima ujue nini unafanya, kipi kinatakiwa kutangulia
na kipi kinatakiwa kufuatia, kumtokea msichana ni jambo ambalo limekuwa
gumu kwa watu wengi, mtu anaweza kumpenda msichana na inawezekana
anaishi nae karibu tu na kila siku anaonana nae ila hafanyi chochote!.
Wanawake hawapendi wanaume hambao hawana maamuzi, kuwa na maamuzi, jikakamue na onyesha hisia zako, penye nia pana njia. Tatizo wanaume wengi wanaogopa kutoswa tena hamna anaeongoza kutoswa kama
mkufunzi wa mapenzi, ila tatizo la mkufunzi wa mapenzi anajifunza
kutokana na makosa, kumbuka hata wewe darasa la pili kipindi kile hesabu
za kujumlisha ulikua unakosa, ila sasa hivi hesabu ya 1+1 unaiona ya
kitoto sababu ulijifunza kutokana na makosa uliokua unafanya. Unaanza na
uwanafunzi kwanza ndo unaenda kwenye ualimu.
Kiumeni.com tunakunyambulia vitu unavyotakiwa kuvijua ukitaka kuwa mtu
unaejua mchezo wa kutongoza. Nifuatilie vizuri, na hakikisha unafanya
majaribio na utaona mabadiliko. Na ukitoswa usivunjike moyo ndo mwanzo
na hata hivyo kisicho riziki hakiliki, hii ni hesabu ya kujumlisha, kuwa
na moyo utaijua tu!.
Unatakiwa uwe unajiamini, hamna kitu ambacho hawa viumbe wenye jinsia
tofauti na sisi wanachokijua zaidi kukiona kama kumuona mwanaume ambae
hajiamini, na ndio sababu kubwa ya kutoswa, kutojiamini. Maana mwanaume asie jiamini mwanamke
atampeleka wapi... mwanamke anahitaji baba wa familia!, sasa yeye na
wewe mtu usiojiamini wapi na wapi!, maana kwa vyovyote atakuona kuwa
hauna maamuzi madhubuti, na yeye anataka mtu wa kumuongoza, kwahio
ukimfata hakikisha upo unajiamini na aone unajiamini.
- NAMBA MBILI; PANGA SWAGA ZAKO USIKURUPUKE....
Msichana hafatwi moja kwa moja, ukitaka kuharibu pozi na kumfata kichwa kichwa utachoambulia ni ''Unikome, tena usinizoee kaka...'',
kuwa mtulivu soma mazingira kama simba muwindaji. Panga swaga zako,
mwangalie machoni kwa mbali akigeuka akakuona unamwangalia tabasamu
kidogo endelea na mambo yako huku unamtupia jicho mara kwa mara, usiogope wala usionyeshe hujiamini kila mtu na mtu wake kwa jinsi ulivyo na wewe una uzuri wako hambao hujioni.
- NAMBA TATU; KABLA HUJAMSOGELEA HAKIKISHA UMEMSOMA...
Siku zote ukienda kichwa kichwa pozi la kufanya mazungumzo yaendelee hua linaisha haraka sana, utajikuta umetupa maneno mawili matatu, la nne huna la kusema!, mtoto kumbe anaendelea kukusikiliza wewe betri imeisha!, unamkosa kijinga tu!, hakikisha umemsoma toka mbali na cha muhimu zaidi angalia lugha yake ya mwili kama
yupo na wewe, alipokushitukia unamwangalia mapokeo yake yalikuaje?,
maana kama kaanza kuuma kucha toka mbali, au kuangalia chini anakuonea
aibu au ulipotabasamu nae katabasamu, jua kaka hio ni mali yako..!, cha
kufanya sogea karibu na usaini mkataba!. Kumuangalia toka mbali na kumsoma ni vizuri tena sana,
maana unaweza kuta mtoto yuko kwenye mudi mbaya, wewe ukapata gia ya
kumuingia kwa kumpa pole na kumpoza!, sasa kama hajamchunguza toka mbali
si unaweza kuta unamchekea kumbe mtu anamajonzi au hasira ukaishia
MATUSI!. Kwa hio kumsoma kwa mbali na kumtupia jicho moja mbili... mpaka
yeye akagundua unamwangalia nakutabasamu inatayarisha mazingira zaidi
nakuyafanya yawe murua na ukiona anakurudishia jicho kali mpotezee
utamtafuta siku nyingine akiwa vizuri zaidi.
- NAMBA NNE; USIWE NA HARAKA...
Ukitaka mambo yaende vizuri zaidi usiwe na haraka, chukua muda wako
onyesha unamtaka kihisia, unaweza hata kumpa siku kadhaa huku
unamwonyesha unavyopendezwa nae, hii inampa muda na yeye akuone wewe ni
mtu wa namna gani, wasichana wanapenda sana mtu mwenye subira na inamfanya msichana akuzoee hata kabla hamjaaanza kuongea na pia ina mto hofu kuhusu wewe na inakupa manufaa ya kutengeneza mazingira ya maongezi yawe ya kelewana na kueleweka zaidi.
- NAMBA TANO; UNAKAZI ZA KUFANYA....
Msichana anampenda mtu wa maendeleo, mtu anaethamini kazi na mtu aliebize na shughuri zake, kwa hio usikosee ukafanya akuone kama mtu mzembe usie na kazi ya kufanya, itakushushia heshima na usijue kipi ulichovuruga. Kuwa bize na mambo yako ila ukimwona mwonyeshe kwa macho na tabasamu kuwa yupo akilini mwako, sio siku nzima unamzinga kama mwizi unataka umtaimu umuibie.
Kwa hiyo umempata huyu msichana
ambae unataka umtongoze uongee nae, umeshamwangalia jinsi lugha yake ya
mwili ilivyo, unacheza nae kwa macho na tabasamu nae anamapokeo mazuri
tu na kuna ka asilimia kadogo kwamba anaweza kukataa na hujali hilo kwa
sababu kwa prea kutoswa kutakua ni sehemu ya mchezo, ukitoswa usichukulie moyoni sana ni sehemu ya kujifunza ili ukirudi ujue wapi ulikosea.
No comments:
Post a Comment