Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Thursday, April 13, 2017

Jinsi Ya Kutongoza Wanawake Waliokuzidi Umri ( Majimama )



Wanawake wakubwa huwa wanakuwa na ladha tofauti ikija kwa maswala ya mapenzi – ile ambayo wanaonyesha kupenda wanaume wadogo kiumri. Na kwa sababu wanaume wengi huwa wanavutiwa na aina hii ya wanawake, bila shaka wanaume hawa hutaka kujua jinsi ya kuwavutia wanawake wakubwa kiumri. Uzuri ni kuwa uhusiano na mwanamke aliyekushinda umri siku hizi inaonekana jambo la kawaida.


So, kama unataka kujua jinsi ya kuwatongoza wanawake wakubwa basi hizi mbinu saba zitakusaidia vizuri.

#1 Thamini kile ambacho anakupatia
Kama unataka kujua jinsi ya kutongoza wanawake wakubwa kiumri, basi unapaswa uthamini  kile ambacho anacho. Kwa lugha nyingine ni kuwa unapaswa kusimamisha fikra zako za kuangalia miaka yake au mikunjano ya uso wake, na uanze kufikiria mambo ambayo anaweza kugawa na wewe ikiwemo mapenzi. Wanaume wengi hudhania kuwa wanawake wadogo ndio huwa na ujuzi ikija na maswala ya mapenzi lakini huwa si ukweli.

Ijapokuwa ni kweli kuwa kujua jinsi ya kutongoza wanawake wakubwa kunahitaji mmoja kuzoea, yaani utahitajika kuthamini na kutambua umri wake, kiujumla; utakuja kujua baadaemkuwa utakuwa umechukua hatua kubwa katika kudeti wanawake wadogo na wale wa wasiwasi. Kwa mfano hutapata mwanamke aliyekomaa akikimbia kwenda msalani ili kuongea na mashoga zake kuhusu deti aliyoko. Hii bila shaka itakuwa ni mwamko mpya wa kutongoza na pia utaboresha uwezo wako wa kutumia mistari kiurahisi na haraka.

#2 Mnyeshee heshima
Wakati unapojifundisha jinsi ya kumtongoza mwanamke mkubwa, weka kwa akili yako kuwa atataka kupewa heshima  zake zaidi ya vile wanawake wadogo utakavyowapatia. Hii ni kwa sababu ana experience ya juu zaidi ya maisha. Na kwa sababu ambazo zitategemeana na yeye, mwanamke aina hii anaweza kuwa asiwe huru kufunguka na kukueleza maisha yake ya zamani ama kukufungukia kuhusu maisha yake. La muhimu zaidi ni kuwa usimwonyeshe kuwa lengo lako kuu kwake ni kumuonyesha kuwa unatoka deti na yeye ama una uhusiano wa kimapenzi na yeye kwa sababu huna jingine la kufanya au umelazimika. Michezo kama hii haiwezi kufanya kazi kwa mwanamke aina hii – kumbuka hilo.

#3 Muonyeshe kuwa wewe ni classy, mjanja na usiyesomeka
Kama unataka kujua jinsi ya kuwatongoza wanawake wakubwa waliokupita umri, basi ni jambo la muhimu kabisa kuhakikisha kuwa unakuwa mjanja na kuwa na tabia za kukomaa. Wanawake wakubwa tayari wanaexprerience ya kuwa na deti ambazo zilikuwa mbaya awali, so kama unataka kumshawishi mwanamke ambaye ni mkubwa wako kiumri vizuri, basi utahitajika kupandisha gemu yako iwe ya juu.
Kimsingi, wanawake wakubwa hawatakuwa interested na wanaume wenye nyege ambao wanashindwa kumaintain gumzo la kawaida mara kwa mara. Badala yake watatafuta mwanaume ambaye ni gentleman ambaye anaweza kuongea kuhusu mambo ya kisiasa na yule ambaye anaweza kutofautisha aina aina za duvai ama angalau yule ambaye anaweza kuchagua sehemu nzuri ya kutoka dinner. So, kadri unapozidi kuwa mjanja, ndipo inazidi kuwa rahisi kumtongoza mwanamke aliyekupita kiumri kuweza kuwa na wewe.

#4 Usijionyeshe
Kuonyesha vitu unavyomiliki ama kuonyesha ujuba wako hakutakusaidia kutongoza wanawake waliokupita umri. Siku hizi wanawake wanapenda kupata nafasi ya kuonekana kuwa wana madaraka flani, so mwanamke atapoteza interest na wewe haraka sana kama  utaanza kujidai na kuringa kuhusu idadi ya wanawake ambao umefanya nao mapenzi ama idadi ya magari unayomiliki. Kama umevalia suti ya kushonesha ama una Mercedes ya gharama si lazima umwambie kuvihusu kwani atajionea yeye mwenyewe.  Badala yake msifu na kumpongeza kwa mambo aliyofanikiwa kufanya. Hii ni njia rahisi ya kuweza kuwatongoza wanawake waliokupita kiumri na wakakukubali kirahisi.

#5 Jiamini
Njia nyingine rahisi ya kutongoza mwanamke aliyekupita umri ni kwa kuonyesha kuwa unajiamini kwa kila kitu unafanya au kuzungumza. Wanawake aina hii huwa kwa kawaida wanapenda wanaume ambao wanauwezo wa kutatua tatizo lolote ambalo watarushiwa usoni mwao. So, kama wewe ni mwanaume ambaye hujafikia kiwango cha kujiamini , basi ni wakati wako wa kuchukua hatua ya kuhakikisha ya kuwa unajenga ujiaminifu wa kuweza kuongea na wanawake. Unaweza kujifundisha kuhusu biashara, sanaa na mambo ya kisasa, silaha ambayo unaweza kuitumia iwapo mwanamke aina hii atazua mjadala akiongea kuhusu swala kama hili. Wanaume ambao wanaelewa kile ambacho wanaongea huwa wanakuwa na confidence zaidi mbele ya wanawake.  Pia wanaonyesha utawala ikija kwa maswala ya mahusiano. Kama unataka kuwa bingwa katika kutongoza wanawake waliokupita umri, basi confidence itakuwa ni silaha kubwa katika mpango mzima.

#6 Yaweke mapenzi yawe ya hali ya juu
Kama unataka kumshawishi mwanamke aliyekushinda kimiaka vizuri, unafaa kuhakikisha kuwa unaweka mapenzi yawe juu. Hii inamaanisha kuwa, ijapokuwa hatakuwa na tabia za kama wanawake walio wadogo, unapaswa humchukulia kama mwanamke mdogo. Mnunulie chokoleti, maua na zawadi ndogo ndogo mara moja au nyingine. Msifu wakati amevalia nguo nzuri ama anapopendeza mnapotoka out. Mambo haya madogo madogo ambayo unamsifia mwanamke yatamfanya mwanamke kuwa na furaha na atapendezwa na wewe.

#7 Usitaje kuhusu utofauti wa miaka yenu
Na lile jambo muhimu la kuzingatia wakati wa kujifunza kutongoza wanawake waliokupita umri ni: kutotaja tofauti ya miaka yenu. Hata kama haujiskii huru na kuwa na yeye mara ya kwanza, hupaswi kuzungumzia swala hili. Ama unaweza kuharibu nafasi yako ya kumtongoza. Badala yake makinika na mambo ambayo yanahusiana nyote wawili, kama vile kuongea kuhusu mambo mnayopenda au kuongea kuhusu filamu. Pia unaweza kuingiza ucheshi katika mazungumzo yenu; hii hufanya kazi nzuri kwa mwanamke.
So hizi ndizo mbinu unapaswa kuzijua ikija na maswala ya kutongoza mwanamke ambaye amekushinda kiumri.

No comments:

Post a Comment