Baada ya kumaliza chuo rafiki zake wote
walipata kazi katika kampuni moja binafsI na Jane alibakia nyumbani
akihangaika kuzunguka na Bahasha za kaki kutafuta kazi ofisi moja hadi
nyingine. Hapo ndipo urafiki wao ulipoanza kuingia dosari kwani kila
wakitoka basi mazungumzo ya rafiki zake hao yalikuwa ni kuhusu kazi na
mambo ya ofisini na mara kadhaa walimtenga na kutoka wenyewe na kila
alipouliza kwanini hawakumstua watoke wete walimuambia “Tulikuwa
tunaongea mambo ya ofisini , si unajua siri za ofisi…”
Pamoja na yote hayo Jane alivumilia
akijaribu kujiweka nao karibu kwani urafiki wao ulianzia mbali tangu
wakiwa kidato cha tano mpaka chuo ambapo walisoma kozi moja nakuishi
chumba kimoja wote watatu. Mwaka mmoja baadaye Fatma alichumbiwa na
kuolewa na Boyfriend wake wa kutoka chuo na haikupita miezi mitatu Eva
naye aliolewa na mfanyakazi mwenzake ambaye walianzisha mahusiano baaada
tu ya kupata ajira.
Hicho ndiyo kilikuwa kipindi kigumu
kwake kwani ndiyo wakati ambao mpenzi wake Prosper ambaye walidumu
kwenye mahusiano kwa miaka mitatu tangu wakiwa chuo na kupata
Scholarship ya kwenda kusoma Australia baada ya kumaliza chuo alipunguza
mahusiano na kuanza kupost Facebook mpenzi wake mpya wa kizungu, Jane
alipomuuliza alimuambia kapata mtu mwingine na asimsubirie.
Aliwahitaji sana marafiki zake lakini
nao walimtenga na kumuona kama adui, kwanza hakuwa na kazi na pili
alikuwa hajaolewa. Mara nyingi sasa walikuwa wakitoka na waume zao na
kwakuwa yeye hakua hata na Boyfriend asingeweza kutoka nao kabisa. Mara
chache ambazo alitoka nao walikuwa wakiongea kuhusu ndoa. ile hali tu ya
kumuonea huruma kuwa hajaolewa ilimfanya ajisikia vibaya.
“Wewe mzuri Jane, na shape lako hilo
nakushangaa unakuwa peke yako, si utafute hata mzee wa kupumzika naye
akuondolee mawazo… Kuna Baba mmoja pale ofisini huwa anakuangaliaga
ukija..sema nikuunganishe naye…” Sikumoja Eva alimuambia kiutani utani
lakini alionyesha kumaanisha. Jane alijua wanamchora lakini
hakukasirika, wakati huo alikuwa mpweke na aliwahitaji marafiki sana,
alimjibu tu kwa upole “Wakati Mungu bado, nina hamu sana ya kuolewa
lakinsiwezi lazimisha, wakati wa Mungu ukifika nitaolewa..”
*********
Kule ofisini mambo yalizidi kuwanyookea
rafiki zake, miaka miwili baadaye Eva alipandishwa cheo kuwa mhasibu
Mkuu huku Fatma akihamishiwa Morogoro kuwa meneja wa moja ola tawi la
kampuni hiyo ambayo ilikuwa na matawi katika mikoa ya Morogoro, Mwanza,
Arusha na Mbeya. Habari zile Jane alizisikia siku alipoenda ofisini kwao
kupeleka barua yake ya ajira, alisikia kuna nafasi zilitangazwa pale na
alipofika alitaka kuonana na rafiki zake ili angalau wampigie pande
apate nafasi ya uhudumu.
Pamoja na digrii yake lakini aliamua
kuomba kazi ya uhudumu kwani alishachoka kukaa nyumbani miaka mitatu
bila matumaini ya kupata ajira, alijua kama angeweza tu kuingia
kuajiriwa basi ungekuwa ndiyo mwanzo mzuri kwake katika kupata kazi
anayoitaka. Alipoulizia ndipo alipoambiwa kua Fatma kashahamishwa na Eva
sasa ni bosi, alielekezwa ofisini kwake na alipofika na kukutana na
Secretary wake aliambiwa asubiri kama wageni wengine waliokuwa pale.
Alikaa nakusubiri huku akishangaa kuwa
rafiki yake ambaye walilala chumba kimoja wakitaniana na kushea kila
kitu alikuwa na secretary, alimshukuru Mungu kwa hilo na kumuombea.
Alisubiri sana wageni wote waliingia na kutoka wakiruhusiwa na secretary
ambaye alipiga simu kwanza, alibaki mwenyewe pale na ilipofika zamu
yake kabla ya kuingia alikuja kijana mmoja wa makamo.
“Dada subiri kwanza, karibu bosi..”
Secretary aliongea akimzuia kuingia na kumruhusu yule kijana, yule
kijana alitembea mpaka mlangoni na kuufungua mlango, “Ulikua unaingia
huku?” Aliuliza yule kijana. Bila kuongea kitu akiwa amechoka
alitingisha kichwa kukubali “Basi ingia mimi nitasubiri..” Yule kijana
alimuambia, Jane alikataa kwa heshima akimuambia aingie tu yeye hakua na
haraka lakini yule kijana naye alikataa.
Baada ya kusikia neno Bosi Jane aliogopa
kabisa akijua asipooonyesha nidhamua hata kazi hatapata hivyo
alisisitiza aingie kuwani yeye hakuwa na haraka. Kijana alifunga mlango
na kwa utani alisema “Basi kama na wewe hutaki kuingia tusubiri wote..”
Huku akitabasmau Jane aliingia, alimkuta rafiki yake yuko bize na
alimsalimia kwa bashasha lakini aliitikiwa kwa mkato bila bashasha
yoyote, kabla hata hajasema chochote alimuambia “Naomba ongea
harakaharaka maana nina kazi nyingi si unaona…”
Eva aliongea huku akimuonyesha lundo la
mafaili. Mapokezi yale yalimfanya Jane kupoteza pozi kabisa, alikuwa
akiongea na mtu ambaye akili yake haikuwa pale. Alizuga tu kuwa alienda
pale kusalimia na ili asimsubirishe yule Kaka muda mrefu, aliaga na
kutoka, Eva hata hakumsindikiza alinyanyua tukichwa kidogo akasema poa
siku njema kisha akaendelea na kazi zake. Jane alitoka huku
amenyong’onyea.
Pale nnje yule Kaka aliyeonekana
mchangamfu alikuwa bado anasubiri. “Umeshughulikiwa?” Yule Kaka
alimuuliza, “Ndiyo kaka ahsante…” Alijibu huku akilazimisha tabasamu.
Alitoka taratibu, alipofika mapokezi aliwaaga vizuri, alitembea mpaka
getini lakini kabla hajatoka mlinzi, alimuambia subiri kwanza. Jane
alishangaa kwani hakua maefanya kitu kibaya, alisimama kusubiri na
alipogeuka ndipo alipokutana na yule Kaka akija akitembea kwa mwendo wa
kasi, sasa alikuwa na wasiwasi zaidi akihisi labda kuna kitu kibaya
kafanya.
**********
“Samahani kwa usumbufu…” Yule Kaka
alianza kuongea, kumbe baada tu ya yeye kutoka yule kaka alimfuata nyuma
na alipomuona anaagana na dada wa mapokezi alienda moja kwa moja
kumuuliza yule ni nani ndipo aliambiwa alileta barua ya maombi ya kazi
na hapohapo alichukua simu ya mapokezi na kumpigia mlinzi akiamuambia
asimruhusu yule jane kutoka, alimuita na kumuaomba arudi ofisini kwake.
Yule Kaka alikuwa ni Samwel, mtoto wa
mmiliki wa ile kampuni ambaye alikuwa Uingereza kimasomo, ni miezi sita
tu alikuwa amerejea na Baba yake ambaye alikuwa na makampuni mengine
akimuachia kuendesha ile kampuni kama Mkurugenzi mkuu lengo lake likiwa
ni kumuandaa ili kuendesha makampuni yake yote kwani alikuwa ndiye mtoto
wake wapekee wakiume akaiwa na mdogo wake mmoja wakike ambaya bado
alikuwa chuo.
Jane hakusita alirudi kwa wasiwasi na
alipoingia Samweli liagiza kueltewa faili lake na akuanza kulipitia.
“Mbona CV yako nzuri namna hii, hii GPA…halafu unaomba kazi ya uhudumu…”
Aliongea kama utani, Jane alimuelezea namna kupata kazi ilivyokuwa
ngumu, taratibu walianza kuongea mambo kadhaaa, Sam ambaye alikua
muongeaji sana alipiga klila story na akujikuta wamezoeana, muda
ulikimbia mpaka jioni iliwakuta pale.
Jane alipotaka kuondoka Sam alimuomba
ampe lift kwakuwa hakuwa na usafiri akifikiria kusukumana katika
daladala alikubali. Kilichofuatia hapo ni historia, Sam alivutiwa na
Jane mara ya kwanza tu alipomuona na alipogundua kua si mke wa mtu
hakupoteza muda, walijikuta wanaingia katika mahusiano, alimtambulisha
nyumbani kwao ambao walitaka aoe harakaharaka. Kama mtoto wa wakwanza
kila siku walikuwa wakimpigia kelele kuoa mama yake akitaka wajukuu.
Miezi sita baadaye walikuwa ni mke na
mume, Sam alipanda cheo kusimamia makampuni yote ya Baba yake akisaidiwa
na mkewe ambaye alipewa kusimamia kampuni ile ile waliyokuwa wakifanya
rafiki zake Eva na Fatma. Hii ikimaanisha kuwa mbali nakuwa sehemu ya
umiliki alikuwa bosi wao na walikuwa wanalazimika kuriporti kwake.
Pamoja na yote waliyomfanyia lakini Jane hakubadilika aliendelea
kuwachukulia kama marafiki zake ingawa walikuwa wanajitenga kwani
walikuwa wanajisikia vibaya na hawakujiona tena kama watu wa hadhi yake.
Jane alikuwa akiingia mpaka kwenye vikao vya bodi ya wakurugenzi wakati
wao walikuwa ni wafanyakazi wa kawaida tu.
Jane sasa ana ujauzito wa miezi tisa na
anakaribia kujifungua, Familia nzima ni kama imechanganyikiwa kusubiri
mjukuu, Mama mkwe hataki hata anyanyue kikombe, wifi yake kila siku ni
kuchagua majina mapya ya mtoto wa Kaka yake, Baba mkwe anafuraha zaidi
kwani tayari ameshajua kua mjukuu wake wa kwanza ni wakiume anauhakika
mali zake hazitaenda mbali. Fatma na mumewe bado hawajafanikiwa kupata
mtoto, Eva ana mtoto mmoja na nimjamzito wa mtoto wao wapili, huku ndoa
yao ikiwa mashakani kwani ameshamfumania mumewe zaidi yaa mara tatu na
wafanyakazi wenzake lakini hana namna analazimika kuvumilia tu.
*******MWISHO
KILA GUMU, CHANGAMOTO UNAYOPITIA JUA
KUWA KUNA WAKATI WA MUNGU, HUO UKIFIKA HATA SHETANI ATASIMAMA PEMBENI
KUKUSUBIRI UPITE HAKUNA WA KUKUZUIA.
No comments:
Post a Comment