Kila
siku yule Mama alikuwa akienda kugonga mlango katika ile nyumba, beseni
lake kichwani akiuza mboga za majani na kila siku alikuwa akiambiwa
hawahitaji mboga zamajani. Mama mwenye nyumba alikuwa ni mtu mwenye
uwezo mkubwa na kila kitu walikuwa wakinunulia supper Market na sehemu
safi safi na si mitaani.
Alishamuambia
mfanyakazi wake wa ndani kutokununua mboga au kitu chochote kwa wapita
njia kwani vinaweza kuwa na magonjwa. Lakini yule Mama hakukoma alienda
tu kugonga akisema kuwa anauza mbogamboga, ilifikia hatua wakataka kumpa
pesa tu wakidhani ni ombaomba lakini alikataa, yeye alitaka kuuza
mboga.
Baada
ya kuona hivyo Mama mwenye nyumba alimuambia mfanyakazi wake awe
ananunua fungu moja la mchicha kila siku lakini hawakuupika kila siku
walinunua na kuuutupa. Hali ile iliendelea kwa zaidi ya miaka miwili.
Siku moja mfanyakazi wa ndani ambaye alikuwa mpya alimfuata Mama mwenye
nyumba na kumuuliza.
“Mbona
yule Mama kila siku akishaleta mchicha pale hutembea mbele kidogo na
kukaa pembeni ya Barabara na kulia, kwani ana tatizo gani?” Mama mwenye
nyumba alistuka kwani hakuwa akimfuatilia awali,. aliamua kumsubiri siku
nyingine na kukuta kweli anafanya hivyo, alimuangalia kwa wiki nzima na
kukuta anafanya hivyo hivyo.
Lakini
pia aligundua kuwa ingawa mtaa ule ulikua na nyumba nyingine lakini
alikuwa akigonga pale tu, hakuenda kuuza mboga katika nyumba nyingine,
jambo lile lilimstua na siku moja alipoleta mboga alimuambia aingie
ndani na hapo akaanza kumhoji. Mwanzoni yule Mama alikuwa mzito kuongea
lakini baada ya kubanwa sana huku akitoa machozi alianza kuongea.
“Mimi
siji hapa kuuza mboga, nakuja kumkumbuka mume wangu. Miaka kumi na tano
iliyopita mimi ndiyo nilikuwa mmiliki wa nyumba hii, tuliijenga na mume
wangu kuanzia msingi mpaka hapo ilipo. Mume wangu alikuwa kiongozi
mkubwa serikalini na alikuwa na pesa nyingi, mimi nilikuwa Mama tu wa
nyumbani na kutokana na pesa za mume wangu sikuona umuhimu wa kufanya
kazi.
Lakini
baada ya mume wangu kufariki dunia mamoi yalibdilika. Niliachiwa kulea
watoto watano mimi peke yangu bila kazi yoyote, ndugu wa mume wangu
walinitelekeza ingawa mume wangu aliwasaidia sana, kweli waliniachia
mali zote za marehemu lakini sikujua hata nizifanyie nini. Ndipo
nilianza kufanya biashara lakini kwakuwa nilikuwa sijui chochote kuhusu
biashara nilipoteza kila kitu.
Mafao
ya mume yaliisha yote na nikawa sina hata hela ya chakula, nyumba hii
ndiyo kitega uchumi pekee ambacho kilibaki, nikachukua mkopo benki kwa
dhamana yake na niliposhindwa kulipa nikanyanganywa ikauzwa. nyie ni
watu wa pili kuinunua hii nyumba na kila siku nimekuwa nikija hapa
kujikumbusha tu maisha niliyokuwa nikiishi.
Hii
nyumba niliijenga kwa jasho langu na ndiyo mali pekee ya mume wangu
ambayo naiona na kila mara nikija hapa naangalia na kumkumbuka mume
wangu.” Yule Mama alimaliza kuongea huku akitokwa na machozi, Mama
mwenye nyumba alimuonea huruma pesa kidogo ili amuongezee mtaji wake.
Yule Mama aliaga na kutaka kuondoka lakini kabla ya kufika mbali
aligeuka na kumuuliza.
“Samahani
Dada kwani wewe unafanya kazi?” Alimuuliza yule mwenye nyumba. Yule
mwenye nyumba alitingisha kichwa kushiria kuwa hafanyi chochote. Huku
akimnyooshe mkono alimrudishia kile kiasi cha pesa alichokua amempa na
kumuambia “Chukua hizi zitakusaidia ufungue biashara yoyote, uwe na kitu
cha kufanya, unauhitaji msaada huu zaidi yangu.
Mimi
tayari nina biashara ya mchicha naweza kuwalisha wanangu lakini wewe
huna biashara yoyote unasubiri mume wako awalishe, haipaswi kuwa hivyo,
siku akiondoka watakufa njaa, chukua hizi pesa kafungue biashara
ukifanikiwa kutengeneza pesa za kwako basi utanipa msaada na si hizi za
mumeo. Mimi pesa za mume wangu hazikunisaidia hivyo sidhani kama za mume
wako zitanisaidia hata wewe hazitakusaidia.”
Yule
Mama aliziacha zile pesa na kuondoka. Alimuacha Mama mwenye nyumba
akiwa ameduwaa tu, hakurudi tena kwenye ile nyumba. Mama mwenye nyumba
alizinduka usingizini na kweli alichukua zile fedha na kununua vitenge
akaanza kuuza kwa mashoga zake sasa hivi anaduka kubwa la vitenge ambazo
huchukulia Congo pia ana duka la nguo ambazo hununua China, hamtegemei
tena mume wake kwa kila kitu.
*****MWISHO
#SHARE
huu ujumbe labda utaweza kumuamsha mwanamke mmoja aliyelala akimtegemea
mume wake kwa kila kitu. Inawa siwezi sema labda ipo siku mume wako
anaweza kukuacha na kukutelekeza na watoto lakini nina uhakika kwa
silimia 100 kuwa hawezi kuishi milele, hivyo jiandae sasa kama
akitangulia yeye na si wewe.
No comments:
Post a Comment