Nimatumaini
yangu wapenzi wasomaji ya mahaba ni wazima wa afya na mnaendelea vema
na shughuli zenu za kila siku.Mi nimzima na namshukuru Mungu kwa
kunijaali afya njema. Leo napenda kugusia umuhimu wa Romance.
Kabla
ya yote unaweza kujiuliza nini maana ya Romance, kwa kulitamka neno
Romance nirahisi sana lakini kulijibu ni vigumu, jaribu utaona kama unaweza
kusema nini maana ya Romance. Ni kitu ambacho unaweza kufanya na mpenzi
wako, wakati mkiwa faragha, unaweza kutumia muda mwingi mkitomasana ama kupeana vitu ambavyo vitawafanya kuwa karibu zaidi. Romance ni muhumu sana katika maisha ya mapenzi, bila romance maisha
yako ya mapenzi hayataweza kudumu. Pia romance ni uthibitisho wa kweli
katika mapenzi yenu. Inaonyesha mapenzi yako ya kweli na inakusaidia
kuwa mpenzi mzuri kwa mwandani wako.
Mara
nyingi siku zinavyokwenda watu wengi husahau kuwapa wapenzi wao Romance
nzuri ambayo itawavuta karibu na kuwafanya wajisikie furaha kila
wanapokuwa mbali na wapenzi wao, hivyo Romance wakati mwingine huvuta
hisia za mapenzi hata kama mpo mbali kimwili lakini kifikikra na hisia
zinaweza kuwavuta karibu mkakumbukana kwa yale mliyokutendeana siku moja mlipokuwa faragha.
Kuna
njia ambazo unaweza kuzifanya kuweka mshumaa wa romance ambao utakuwa
ukiwaka moyoni mwako maishani. Ukakufanya usijute kuwa na mwandani wako,
utajiona chaguo lako lilikuwa bora zaidi.
Nini cha kufanya kwa mpenzi wako Kila siku?
1. Mwambie mpenzi wako kiasi gani unavyompenda, sio kukaa kimya, atajuaje kwamba unampenda.
2.
Mwambie 'Nakupenda sana' hata mara saba kwa siku, atajisikia furaha
moyoni na hata kama alikuwa na wasiwasi na wewe sasa utakuwa wakati
wakuamini kiasi gani unavyompenda.
3.
Tumia angalau muda mchache wa kuwa nae sehemu tulivu mkipota vinywaji
baridi na chakula, pia mtalazimika katika sehemu hiyo tulivu mjadili
mipango yenu ya maisha, unaweza kutumia hata saa moja kwa mazungumzo au
hata zaidi ya saa moja, sio unaenda dakika mbili unaondoka. Atakuona
unakuja kumsanifu au unamuwahi mwingine, kama una
kazi ya muhimu mweleze taratibu kwamba una kazi, hatabisha kama ni
muungwana. Atakusikiliza na mtapanga labda kukutana kesho utakapokuwa na
nafasi, tena hakikisha unatafuta muda wa kuwa na mpenzio.
4.
Mfanyie Surprise au kitu ambacho hakikutarajia akilini mwake. Unaweza
kumletea zawadi nzuri sana, labda simu ya mkononi, nguo ya ndani, au
kitu chochote ambacho unajua hakikuwa akilini mwake.
5.
Kama mnaishi pamoja, mnapoamka asubuhi unatakiwa umkumbatie mpenzio,
mkeo au mumeo. Unaweza kumsifu kwa kazi ya jana ambayo kwa kiasi kikubwa
uliifurahia, usimbanie kuhusu suala la kumsifia. Mpe moyo kwamba
anayaweza mashamsham ya gadoro, au vipi? mpenzi msomaji.
Nini cha kumfanyia mpenzio kila wiki?
1.Umanatakiwa
kupeana miadi ya kwenda mahala tulivu kabisa, mkibadilisha na mawazo.
Sio kila siku kuwa chumbani, unachotakiwa ni kubadilisha mazingira.
Wakati unapokuwa mnaelekea labda sehemu ya kubadilishana mawazo,
usipende kutembea eti, mume nyuma mke mbele, kwani unamwogopa nani?
Waonyeshe wale wanaojua kuchukua vya watu kwamba mmejenga ukuta imara wa
penzi lenu. Watashindwa kutupa ndoana za kukuteka wewe ama mpenzio, Shikaneni mikono tena mkionyeshana kiasi gani mnapendana.
2. Mfanyia kitu ambacho wote mnaweza kukifurahia kwa kikifanya kwa pamoja.
3
Kama ni mwanamke unaweza kumpikia chakula kizuri ambacho anapendelae
kukila, hakikisha chakula hicho kuanzia mapishi hadi kukiandaa mezani ni
kazi yako. Sio Umpikie halafu umwambie 'hausigeli' akamwandalie,
haipendezi kabisa na hata jisikia kula chakula chako. Siajabu hata siku
hiyo ya wikiendi unaweza kumlisha chakula hadi akashiba, sio kazi
kumlisha mpenzio, unajua mwanaume ukimnyenyekea hukisikia ni bora na
huongeza mapenzi zaidi.Atakudhamini kuliko chochote, atapenda kukuona
mara kwa mara.
Mimi
binafsi na mlisha mepnzi wangu, kwani nampenda sana. Ninapomlisha
chakula akishiba nae hunilisha kwa furaha. Ninapomtamkia nimeshiba basi
hunitolea tabasamu nono lililoshiba midomoni mwake.
4. Mpe mpenzio zawadi ya kumshangaza, ambayo unahisi ataipenda na kuifurahia.
5.Fikiria
kitu ambacho utamfanyia wiki nyingine, hasa mapenzi. Usifanye mapenzi
kila siku na pia hakikisha unabuni njia nyingine mpya ambazo atazipenda
na kuzifurahia.
Nini cha kufanya kila mwezi?
1.Unaweza kutoka na mpenzio mkaenda kufanya Shopping na ukamnunulia zawadi nzuri, kama nguo, viatu, nk.
2.Mnaweza
kutizama mkanda wa mahaba, angalau mara mbili kwa mwezi. Hakikisha
wakati wa kuangalia mkanda, unamwonyesha staili nzuri uzipendazo. Usione
aibu kumwambia unaipenda staili moja kati ya mbili, tatu ulizochagua.
3.
Unashauriwa kwenda na mpenzio kucheki afya zenu kila baada ya miezi
miwili, hii itasaidia kama kuna magonjwa basi yapatiwe tiba, sio unasema
unampenda mwenzio lakini mumshauri kupima afya zenu.
4.
Muulize kitu ngani labda ambacho umemfanyia bila kujua kama umemuudhi,
kwani wakati mwingin e unaweza kumuudhi mwenzio bila kujua na kukaa
kimya kwako kutamfanya aendelee kuumia.
Hebu
ukiwa na mpenzi wako jaribu kubadilika bwana, sio kukaa kama gogo au
ukimaliza mtanange unakimbilia kufuli, la nini, halina kazi tena ukiwa
na mwandani wako...hebu mpe faraja nzito.....aliwazike hakuna
kubaniana...
No comments:
Post a Comment