Namshukuru
Mungu kunifanikisha hadi kuona jua la leo, na namshirikisha kila jambo
nifanyalo. Karibuni tukumbushane machache juu ya mapenzi ambayo kila
siku tumekuwa tukikumbana nayo, iwe asubuhi, mchana, jioni na usiku.
Katika sekunde, dakika ama saa yeyote popote pale duniani.
Naweza kutafsiri mapenzi kama hisia nzito zimuingiazo mtu pale moyo wake unapozama katika ulimwengu wa huba kwa yule ampendae, akajikuta kwa lazima isiyoweza kuvumilika ama kukwepeka akampenda mwenzake.
Nadhani
hakuna mtu asiyejua kupenda, ni wazi hata wewe unajua kupenda na
ulishawahi kupenda na kupendwa, kama bado ipo siku mungu atakujaalia
utampata umpendaye na akupendaye. Usikate tamaa mwombe mungu atakusaidi
yeye ndiye anayejua mume gani au mke gani atakupa.
Na
kama yupo asiyeweza kupenda basi huenda ana matatizo kisaikolojia na
namshauri aende kwa wataamu wa mambo ya saikolojia waliopo karibu nae
waweze kumshauri cha kufanya juu ya tatizo lake.
Wiki
iliyopita nilizungumzia jinsi mtu anapojikuta akiwa mtumwa wa mapenzi
kwa kulazimisha mapenzi kwa yule aliyempenda bila yeye kupendwa. Leo
basi na penda kuongelea suala la mwanamke anapokuwa anatoa jibu la
haraka kwa mtu anayemtongoza.
Kwanza
unapomtongoza mwenzako unategemea kupata majibu mawili, eidha
kukubaliwa ama kukataliwa. Na unapotongozwa unatarajia kutoa jibu moja
la uhakika lisilo na kejeli, kumkubali ama kumkataa. Hii itategemeana
kiasi mwanaume huyo atakavyo kukonga moyo wako na kukufanya uwe na msisimko
wa kumtamkia hisia zako. Tatizo linakuja pale mwanaume anaposhituka na
kuhofu kukubaliwa kwa muda mfupi na mwanamke aliyemweleza ukweli kutoka
moyoni mwake.
Mpe
wenzio uhuru wa kusema, mbona wewe ulimweleza bila kujali ni muda gani
umekutana naye?. Kwanini tusibadilike, tukaenda na wakati?. Lazima
tujiulize kulikoni inafikia hatua ya kumfikiria mtu uliyemtamkia
anapokutamkia ukamuhukumu bila kosa.
Naomba
ufahamu kitu kimoja, sisi wote ni binadamu, mwanaume anavyo penda hata
mwanamke naye ana hulka ya kupenda na kumwonyeshe mwenza wake kiasi
alivyo mpenda.
Pengine
katika mila na desturi za sisi waafrika tulizoeshwa kwamba mwanaume
ndiye mwenye kumrubuni mwanamke hadi kuwa naye katika ndoa, Inapofikia
hatua ya mwanamke kutoa maamuzi itategemeana na mtu aliyemrubuni.
Lakini sidhani kwamba kuna ubaya mwanamke unapomtongoza ukategemea kupata jibu baada ya mwaka au mwiezi sita baadaye.
Kufanya
hivyo si ishara kwamba huyo unayetegemea kupata jibu kwake atakuwa
mwanamke mwaminifu sana, na atakuwa na tabia nzuri kupita yule atakaye
kukubalia siku chache baada ya kumweleza bayana kile kilicho moyoni
mwako.
Mwanamke
ana haki ya kutoa msisimko wake juu ya yule aliyemtamkia ikiwa moyo
wake nao umeridhia na kupendezwa na mwanaume aliyemtamkia kwa uwazi
kwamba anampenda. lAkini hata hivyo nawashauri, kuwa makini sana na
majibu ya watu wanau watamkia kuwa wanawapenda, usidanganyike na mali ya
mtu ama cheo cha mtu, utakuwa unajiangamiza. Angalia utu na upendo wa
mtu, usitizame pesa ambazo hata wewe waweza kuzipata, kumbuka pesa
inaisha lakini utu wa mtu hauishi.
Kutamkiwa haraka na mwenzio uliyempenda si tiketi ya kumdhania mwanamke yule ni mdhaifu na malaya, wengine kuhofia huenda akawa akimkubali
kila mwanaume atakaye mweleza anampenda. Naweza kukuhakikishia wanawake
wengi hivi sasa wanajaribu kuwa wagumu kuwakubalia wanaume wanauwapenda
kwa dhati kwa sababu wanaume wengi wamekuwa na hulka ya kizamani. Kama
ulikuwa hutaki jibu mapema basi usingemtamkia mwenzako kwamba unampenda
na una subiri jibu kutoka kwake.
Darubini yangu ya mitaani inaonyesha wanawake
wengine wanajifanya wagumu kuwakubalia wanaume ilhali wanawapenda, kwa
kuogopa kutoswa. Inapofikia hatua ya kuwazungusha wenzao muda mrefu waliowapenda wakajikuta kupoteza bahati zao. Kwani wanaume wengine wamekuwa wakiudhiwa na tabia ya wanawake wanaojifanya wagumu
kama reli kumbe si waaminifu hata kidogo lengo lao waonekane wagumu
kushawishika kwa wanaume wengine. Unaweza kumkuta mwanaume anatamba wazi
wazi bila aibu, “Mimi namwamini sana demu wangu, alinizungusha mwaka
mzima bwana. Inaonekana ni mwaminifu sana” Hicho sio kipimo cha uaminifu
katika mapenzi, ndugu yangu. Tena anaweza akawa mgumu kwako pengine uchochoro kwa wengine.
Jaribu
kuupa moyo wako uhuru, uchangue upendavyo, Usiudhulumu nafsi yako kwa
sababu zisizo na msingi, kama unataka kumchunguza tabia zake ni jambo
ambalo utafanya siri kabla ya kufikia hatua lengwa. Ukiubania moyo wake
nisawa na kulinyima tumbo chakula, utateseka na hata amani ya moyo
itatoweka. Usiunyime moyo wako uhuru.
NB:
Ushauri wangu; Tunapaswa kubadilika, mwanamke anapomtamkia mwanaume
aliyemtongoza kwa haraka si tiketi ya umalaya. Tuwe waaminifu katika
ndoa zetu, uchumba na urafiki wetu, tusiwaudhi wandani wetu na kuwalaumu
pasina sababu. Kufanya hivyo nikupunguza upendo wa dhati.
No comments:
Post a Comment