Dysminorrhea ni nini?
Haya mi maumivu makali anayoyapata mwanamke siku chache kabla ya kuingia na kipindi ambacho yupo kwenye siku
zake.
Kuna aina kuu mbili za maumivu hayo kutokana na chanzo
chake.
Primary dysmenorhea…
Haya ni maumivu ambayo hayana sababu maalumu lakini
wataalamu wanadhani yanasababishwa na homoni inayoitwa kitaalamu kama prostaglandins
kutoka kutoka kwenye mfuko wa uzazi.{endometrium}
Secondary dysminorrhea..
Hii ni aina ya
maumivu ambayo hutokea kutokana na ugonjwa flani hasa unaoathiri umfuko wa
uzazi mfano pelvic inflammatory diseases, underdeveloped genital organs,
cervical stenosis, asherman syndrome.
Vipimo vinavyofanyika
hospitali.
Utrasound scan:
Hichi ni kipimo cha ambacho hupiga picha kuangalia mfuko wa
uzazi kama una tatizo lolote ambalo linalohusiana na maumivu hayo.
Mgonjwa hutakiwa kunywa maji mengi kujaza kibofu cha mkojo
kabla ya picha hiyo.
Matibabu:
- Kutibu ugonjwa unaosababisha maumivu hayo ni njia nzuri zaidi.{secondary dysminorrhea}
- Matibabu huweza kua antibayotiki kulingana na ugonjwa husika hadi upasuaji wakati mwingine.
Matibabu kwa maumivu ambayo hayasababishwi na ugonjwa
wowote.{primary dysiminorrhea}
· Fanya massage kwa nusu saa kila siku{kipindi cha maumivu} kwenye tumbo la chini ili kuongeza mzunguko wa damu.{dry massage}
· Fanya massage kwa nusu saa kila siku{kipindi cha maumivu} kwenye tumbo la chini ili kuongeza mzunguko wa damu.{dry massage}
·
Tumbukia kwenye sinki la maji ya moto kwa nusu
saa au saa moja kipindi cha maumivu au weka maji ya moto kwenye mpira maalumu
kisha weka juu ya tumbo.
·
Tumia dawa za maumivu kama diclopa, ibuprofen,
meloxicam pale maumivu yanapokua makali sana.
Kikundi cha dawa za anticholinergic mafano
colirem na hyoscine butylbromide pia ina msaada sana katika shida hii.
Onyo: dawa zote unazozifahamu
zina madhara kwa matumizi ya kibanadamu hivyo usitumie dawa yeyote bila
maelekezo ya kitaalamu.
No comments:
Post a Comment