Condom ni nini?
Huu ni mpira uliotetengenezwa kitaalamu na raba inayoitwa
latex mara nyingi..
Hutumika katika tendo la ndoa kuzuia magonjwa ya zinaa
ikiwemo ukimwi pia kuzuia mimba ambazo hazikupangwa.
Kuna condom za kike na za kiume japokua matumizi ya kondom
za kike hua ni adimu sana.
Ikitumika vizuri condom huweza kuzuia kwa zaidi ya 95% ya
maambukizi ya ukimwi ambayo yangeweza kuambukizwa bila kutumia condom.
Lakini kwa sababu watu wengi hawapendi kutumia kondom
wametunga uongo mwingi kushawishi wengine wasitumie, na ufuatao ndio uongo huo.
1.
Condom inapunguza raha ya tendo la ndoa:
Ukweli ni kwamba kondom husaidia sana wanaume ambao wana tatizo la kufika
kileleni kabla wenzi wao hawajaridhika hivyo hufanya tendo hilo kua la raha kwa
wote.
2.
Condom imewekewa virusi vya ukimwi ndani
Ukweli ni kwamba kondom haina virusi hivyo na hata kama vingekuepo
visingeweza kuishi ndani ya condom kwasababu kondom haina chakula cha kulisha
virusi na haiwezekani virusi kuishi kwenye mazingira yale, lakini pia condom kazi yake ni kuzuia virusi hivyo.
3.
Condom huweza kupotea ndani ya mwili wa
mwanamke:
Kitu kama hicho hakipo na hata ikitokea ikabaki bahati mbaya ndani ya uke inaweza kutolewa na kidole
kimoja tu kirahisi.
4.
Condom ni ndogo sana na haiwatoshi wanaume:
Ukweli ni kwamba condom inaweza kuvalishwa kwenye kichwa cha mtu mzima
bila kupasuka ata kidogo.
5.
Condom hupasuka sana:
Condom hufanyiwa vipimo na shirika la viwango TBS kabla ya kuingizwa
sokoni, hivyo ikitumika kwa kufuata maelekezo haiwezi kupasuka.
6.
Condom ina matundu kuruhusu virusi vya ukimwi:
Kama nilivyosema mwanzo condom zinafanyiwa vipimo maalumu kabla
hazijasambazwa na haziwezi kua na matundu hayo,
7.
Condom inawasha na kuchubua sehemu za siri:
Ni watu wachache sana wana shida hii na kama wewe ni mmoja wao unaweza
ukamuona daktari akakupa ushauri au ukatumia aina nyingine ya kondomu yenye
material tofauti.
No comments:
Post a Comment