Shoga yangu, kabla sijaelezea ‘topiki’ yangu ya leo, napenda kukupa
pole kwa kuondokewa na Kapteni John Komba aliyefariki dunia siku ya
Jumamosi.
Hakika taifa limepata pigo kubwa sana kuondokewa na kada huyo mkongwe
wa CCM aliyekuwa mtunzi na muimbaji mahiri wa nyimbo mbalimbali.Kwa
kuwa kazi ya Mola haina makosa, hatuna budi kumshukuru na kumuomba
ailaze roho ya marehemu Komba mahali pema peponi, amina.
Leo shoga yangu nataka kuzungumza nawe kuhusu suala la kupiga
vigelegele mwenza wako anapokufurahisha mnapokuwa kwenye eneo lenu
tulivu ambalo wengine uliita uwanja wa fundi seremala.
Nimekuandalia mada hii ili kuwaweka sawa wenzetu ambao hata
wakifurahishwa vipi na waume zao wanapokula ‘msosi’ wa usiku, hutulia
tuli kama maji mtungini.
Shoga, kufanya hivyo ni sawa na kupika mboga bila kuweka viungo kwani
ni wazi itapooza na kutowavutia walaji ambao watakula ilimradi washibe
kisha wakaendelee na pilika zao. Mwanamke unapaswa kuwa mahiri wa sanaa
ya malovee na kama ni uzembe ufanye kwenye maeneo mengine lakini
linapokuja suala la wewe kuwa na mkuu wa kaya katika dimbwi la mahabati,
onesha ubunifu wako wote.
Shoga, mtu asikudanganye, hakuna kitu ambacho wanaume wanakipenda
kama wenza wao kutoa mihemko inayochanganyikana na vilio wanapokula
chakula cha usiku.Mwanamke anapofanya hivyo, huongeza ‘spidi’ ya baba
kumlisha chakula ili ashibe wala asiwaze kwenda kudoea kwa watu wengine
au kulalamika kwamba mumewe hampi chakula cha kutosha.
Shoga, kama ulikuwa hulijui hilo na kuishia kununa wakati wa kula
chakula cha usiku, hebu anza kutoa mihemko, mlilie mumeo na mnapofikia
hatua ya kushiba kwa pamoja piga kigelegele kama siyo vigelegele.
Kufanya hivyo utampa raha mumeo na kujiona chakula anachokupatia
unakifurahia, hivyo hatathubutu kwenda kula nje ya nyumba yenu.Hata kama
huna kawaida hiyo kwa sababu mashetani yako yapo mbali, hebu igiza
kutoa mihemko au kuangua kilio wakati mnapata mlo huo wa usiku unaokuwa
maalum kwenu.
Baada ya kila mmoja kushiba, mshukuru mumeo kwa kukupatia chakula
kitamu kisichoisha hamu, nakwambia licha kabla ya kulala kula chakula
chako mara mbili, alfajiri atakuamsha na kuomba mshiriki tena kula
chakula cha asubuhi ambacho huwa kitamu kupita maelezo.
No comments:
Post a Comment