Amenorrhea ni nini?
Hii ni hali ya mwanamke aliyepevuka na kukomaa maumbile yake
ya uzazi kushindwa kuziona siku zake.
Mwanamke anatakiwa aanze kuziona siku zake kati ya miaka 12
mpaka 14.
Hali hii ya kutoona siku huweza kutokea kwa mwanamke ambaye
hajawahi kuziona siku zake lakini ameshatimiza vigezo[pimary aminnorhoea] AU
kwa mwanamke ambaye ameshawahi kuziona siku zake lakini zimesimama.{secondary
amenorrhea}
Kwa mwanamke ambaye ameshawahi kuziona siku zake akikaa
miezi mitatu bila kuziona siku zake hiyo ndio itaitwa secondary amenorrhea.
Na mwanamke ambaye hajawahi kuziona siku zake akafikisha
miaka 16 bila kuziona hiyo ndio primary amenorrhea.
Tatizo hili linaweza kuzua hofu ya kisaikolojia kwa mwanamke
aliyelipata.
Chanzo ni nini?
- · Kuchelewa kukomaa kwa viungo vya uzazi mfano kizazi, uke na ovari.
- · Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa chakula. i.e tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika hali nzuri maarufu kama leptin kua katika kiwango cha chini sana.
- · Matumizi ya dawa:
- Dawa zinazotumika kwenye uzazi wa mpango zimeonyesha kusababisha halii hii hasa zile zenye homoni nyingi ya progesterone i.e depo provera
- · Kunyonyesha:Miezi sita ya kwanza ya kunyonyesha mtoto kiwango cha hormone inayohusika kutoa maziwa yaani prolactin hua kwa kiwango cha juu sana na homoni zinazohusika na siku za mwanamke yaani oestrogen na progesterone hua ziko chini sana.
- · Ujauzito:Hii iko wazi kwamba ukishapata mimba ile shughuli ya kusababisha mwanamke kupata siku zake husimama.
- · Magonjwa;Baadhi ya magonjwa ya viungo vya uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kuonekana kwa siku za mwanamke mfano polycystic ovarian syndrome.
- · mgandamizo wa mawazo na kubadilisha mazingira ya kuishi.
- menopause: hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 45 mpaka 60. homoni zinazohusika na na kupata siku za mwanamke hua kwenye kiwango cha chini sana kiasi kwamba haziwezi kufanya kazi yake sawasawa. i.e progesterone na oestrogen
MATIBABABU;
- Kujua chanzo cha hali hii na kukitatua ndio mzizi mkuu wa kuweza kutibu tatizo hili.
Matibabu mengine ni:
- · Kufanya masaji kwenye tumbo la chini kwa kutumia maji ya uvuguvugu ili kuongeza damu nyingi kupita huko.
- · Kula chakula kisichotokana na damu{vegetarian diet} chenye protini nyingi. Mfano karanga, nazi, maharage na korosho.
No comments:
Post a Comment