Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Sunday, April 30, 2017

HAYA NDIO MAGONJWA MATANO YANAYOTIBIWA NA BANGI.

            

Bangi ni nini? 
Huu ni mmea ambao umekua ukitumika kwa miaka mingi kama kiburudisho kwa watu flani, japokua matumizi ya mmea huu yamekua yakiambatana na magonjwa ya akili ambayo yameleta ugumu kidogo kuyatibu.
Utafiti mpya uliofanywa na washngton medical quality assuarance commission umegundua kwamba matumizi ya bangi kwa kiasi kidogo chini ya usimamizi wa daktari bingwa wa magonjwa ya akili,[psychatrist} imeweza kutibu kwa uhakika magonjwa yafuatayo.
  • Insomnia{kukosa usingizi}:
Wagonjwa wengi waliotumia mmea huu wameonyesha kupata nafuu kwa kusinzia kwa mda mrefu masaa machache baada ya kutumia bangi, kupata ndoto nzuri  na kuamka asubuhi wakiwa na nguvu za kutosha.
                                                            

  • Migraine{kipanda uso};
Maumivu haya makali ya kichwa kitaalamu yanasababishwa na kuongezeka kwa msisimko wa mishipa ya fahamu{neural stimulation}, hivyo matumizi ya mmea huu yameonyesha kupunguza msisimuko huu na kuleta nafuu kwa wagonjwa hawa.{inhibition of neural transimitter in the brain}
                                                      


  • Anxiety{wasi wasi}
Mmea huu umeonyesha kupunguza uoga na  mawazo ambayo yanamfanya mtu awe na wasiwasi sana kutokana na matatizo yaliyomsababishia wasiwasi huo. mfano hofu ya kubakwa au kifo.
                                                        
  • Depression{mgandamizo wa mawazo}
Watu wenye mawazo mengi sana wamekombolewa na mmea huu na kuishi kwa furaha wakati huo chanzo cha tatizo lao likitatuliwa na madaktari au ndugu zao ili kupona kabisa.
                                                               

  • Bipolar disorder{mudi ambayo haieleweki}
Huu ni ugonjwa wa akili ambao mgonjwa anakua anabadilika mudi ovyo, yaani anaweza akawa mkimya kabisa na mwenye huzuni asubuhi lakini jioni ukamkuta anaongea sana na anafurahi.
Mmea huu unafanya kazi ya kutuliza mudi hiyo na mgonjwa kua kwenye hali nzuri na furaha mda wote.{ acts as mood stabilizer}
                                                   

Onyo: uvutaji na matumizi ya bangi kwa nchini kwetu Tanzania haujaruhusiwa.
Sijaandika makala hii kuruhusu bangi itumike kwa aina yeyote ile na sitawajibika kwa mtu yeyote atakayeanza kuitumia ovyo. ila nimeandika kuwaambia watu tafiti hizi zilipofikia na, ni  nchi chache sana duniani ambazo zimeruhusu matumizi ya mmea huu kwa starehe binafsi au matibabu.

No comments:

Post a Comment