utangulizi
Kwa miaka mingi wanaume wengi wamekua wakijihisi wana nyeti
ndogo kulingana hadithi wanazosikia
mtaani kuhusu wanaume wengine wenye maumbile makubwa, video za phonograph,na
tabia za kuoga pamoja hasa shule za bweni kipindi cha masomo ya sekondari.
Kampuni zizodai zinaweza kuongeza maumbile ya kiume
zimetengeneza pesa nyingi sana kwa kudai zina vidonge, sindano, na dawa za asili kwa ajili ya kazi hii.
Uchunguzi wa kisayansi uliofanyika india umegundua zaidi ya 60% ya wanaume wana wasiwasi na maumbile ya nyeti zao.
Leo naomba nikutoe dukuduku la mawazo yako wewe msomaji wa kiume ambaye na
wewe unadhani una maumbile madogo na unatafuta suluhisho.
Je ni kweli una maumbile madogo?
Jibu ni hapana, kwani ukijiangalia mwenyewe angle unayotumia kujiangalia inakufanya
ujihisi una maumbile madogo, lakini mwanaume unayelingana nae maumbile
akisimama mbele yako utaona anakuzidi mbali sana kulingana angle uliyosimama
kumuangalia yeye.
Je maumbile ya kawaida yanalinganaje?
Kosa kubwa linalofanywa na wanaume ni kujipima urefu wa
maumbile yao wakati yakiwa yamesinyaa.
lakini naomba nikwambie kipimo halali
cha uume ni pale uume unapokua umesimama tu.
Nyeti mbili zilizosinyaa zinaweza kuonekana zinatofautiana
urefu, mfano moja ikawa na sentimita sita na nyingine tisa lakini zikisimama
zote zikafika sentimita 15.
Utafiti umeonyesha mwanaume wa kawaida ana uume wenye urefu sentimita 12 mpaka 15 na unene{circumference}
wa sentimita 12 akiwa amesimamisha.
zaidi ya asilimia 95%
ya wanaume wamo kwenye hicho kiwango hicho.
Japokua kuna wanaume wanakua na uume mkubwa kidogo kuliko
vipimo nilivotaja hapo juu lakini uume ni sawa na viungo vingine vya binadamu
kama mguu na mikono na haviwezi kua sawa
kabisa.
Lazima kuna watu wana miguu au viganja vya mikono vikubwa kidogo kuliko wengine.
Ni 0.6% ya wanaume wanaoupatwa na hali inayoitwa kitaalamu
kama micro penis ambayo uume husimama kwa sentimita saba tu.
Hali hii husababishwa mara nyingi na kuepo kwa kiwango
kidogo sana cha hormone inayoitwa growth
hormone kipindi cha ukuaji.
Hali huweza kutibiwa na wataalamu wa nyeti{urologist} bila madhara yeyote.
Mahusiano kati ya tendo la ndoa na ukubwa wa maumbile ya
kiume.
Utafiti uliofanyika na mtafiti wa kimarekani kwa jina la
jonson uligundua wanawake wengi hua swala la ukubwa au udogo wa maumbile halipo
vichwani mwao na sio kesi kubwa kama wanaume wengi wanavyolichukulia.
Swala la kumridhisha mwanamke halina mahusiano na urefu wa
uume japokua baadhi ya wanawake walikiri kuridhishwa kirahisi na wanaume wenye
uume mnene na sio mrefu kama watu wengi wanavyofikiria.
Lakini point yangu hapo juu haimaanishi wanaume wenye uume
mwembamba hawawezi kuwaridhisha wanawake. La hasha.
Lakini pia naomba nikuonye wewe mwanamke unayesoma hapa usije
ukamwambia mpenzi wako ana maumbile madogo ata kama unatania.
Kauli hyo ataichukulia uzito mkubwa na itamuumiza sana kichwa
kuliko unavyofikiria.
Je kuna dawa ya kuongeza nyeti za kiume?
Mpaka sasa hivi,
Hakuna dawa yeyote ambayo imethibitishwa kuongeza nyeti za kiume kama makampuni
mengi yanavyodai.
Ni operation na mazoezi tu ndio yamefanikiwa kuongeza maumbile kwa
sentimita tatu mpaka tano na zimekua zikiambatana na madhara makubwa kama
kubadilika kwa shape za nyeti, kupungukiwa nguvu za kiume, kuchelewa kupona na
maumivu ya mda mrefu hasa kawa oparesheni.{chronic pain}
hata hivyo mazoezi ya kuongeza uume yameonekana hayana madhara kabisa.
hata hivyo mazoezi ya kuongeza uume yameonekana hayana madhara kabisa.
Zaidi ya 75% ya wanaume waliofanyiwa operation hzo
hawakuridhika na matokeo yake hivyo sikushauri na wewe uingie huko labda kama
una ugonjwa wa micropenis nilioutaja hapo juu.
Mwisho nakuomba wewe mwanaume ufahamu kwanzia leo kwamba
hayo maumbile yako hayana matatizo yeyote na wewe ni dume la mbegu.
No comments:
Post a Comment