"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu
nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba
maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu likawa huru
alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi.
Alinifundisha.
Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya
nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama haikutosha
sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu
mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa
msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi
huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tutumie kinga lakini
aliipinga sana.
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza
kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai.
Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari
amefanya anavyojua. Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini
nikawa na wahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya
lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile.
Alinilawiti!! Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa
mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi.
Mchezo
ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni
mbinu mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu. Miaka
ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu
za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu.
Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo
ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na
atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile. Pesa ikiisha na
mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto.
Sasa akaanza
kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa
kusema neno moja tu. Tuachane!! Nilijuatayari ameniacha!!! Afya yangu
ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi.
Nikapewa ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata mwanaume
mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule
aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulishanyumbani na alitaka
kunioa. Akanioa kweli. Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili
na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana,
hakuwahi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda
hospitali.
Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba
mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga
kabisa.Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu
kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia baruahii mdogo
wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyikanakufanya
mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama
mimi. Wasipokusikiliza usijisikie vibayamaana hata mimi nilikuwa
siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu.
Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe
kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi
siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa.
Lia kwasababu mwanaume mwenzako
AMENITENDA HIVI!!!
No comments:
Post a Comment