Miongoni wa makundi ya vijana hasa wenye umri wa kati miaka 15-23
wengi wao huota wakifanya mapenzi ndotoni, lakini mbali na hao kuna watu
wazima pia ambao hukumbwa na tukio hili. Uotaji wa ndoto hii umekuwa
ukitafsiriwa na wengi kwa maana tofauti tofauti, huku wengine
wakiuhusisha na ufanyaji mapenzi na Majini.
Uchunguzi unaonyesha
kuwa uotaji ndoto za kimapenzi huwatokea hata watu ambao hawajawahi
kufanya kitendo hicho kabisa, huku watu wanaofanya nao wakiwa ni wale
wanaowafahamu kwa sura au wasiowafahamu. Wengi wamekuwa wakijiuliza
maswali mengi juu ya nini kinachangia uotaji huu wa ndoto za kimapenzi?
Kitaalamu
ndoto hizi hutokana na mawazo ya mtu husika ambayo yanaweza kugawanywa
katika sehemu mbili ambazo ni MAWAZO YALIYO WAZI au YALIYOJIFICHA.
Mtaalamu wa masuala ya ndoto Daktari Gillian Holloway anaeleza kuwa
ndto hizi hufumbua maamuzi na hisia zilizojificha nyumba ya ubongo.
Pamoja
na tendo hili kuwa baya katika mitazamo ya wengi hasa kiimani, lakini
bado si kitaalamu halina ubaya kwa kiwango hicho kwani mara nyingine
husaidia kutafsiri yale ambayo wahusiaka hawakupata kuyafahamu kabla.
Kwa mfano vijana ambao hawajafanya mapenzi hupata kutambua raha
itokanayo na kitendo hicho na hivyo kuwaamshia hisia za kimapenzi ambazo
pengine hawakuwa nazo hapo awali.
Wachunguzi wa masuala ya ndoto
wanasema ndoto hizi zikitumika vizuri zinaweza kusaidia kumpata mchumba
anayegusa hisia za moyo, aina ya mapenzi yanayokufurahisha, haiba ya
mpenzi umpendaye na wakati mwingine huchangia kuongeza uzalishaji wa
homoni na kupunguza msongo wa mawazo sawa na mtu aliyefanya mapenzi
kihalisia.
Hata hivyo watu wanaotajwa kutokewa na kitendo hicho
mara kwa mara ni wenye tabia ya kuogopa wanaume/wanawake na hivyo
kuzikandamiza hisia zao, wanaochochea hamasa za kingono na kutokuzikata,
(mfano kufanya romance na kuachana bila kuingiliana), wanaotazama picha
za ngono, wanaozungumzia sana mambo ya kimapenzi na wale wanaowaza sana
wapenzi wao walio mbali.
Kwa maana hiyo ili mtu asiweze kutokewa
na ndoto hizo hana budi kujizuia na mambo hayo yanayotokana na uamshaji
na ukandamizaji wa hisia za kingono. Hii ina maana ya utashi wa mtu wa
kutopenda kuota, lakini sia kwamantiki kuwa uotaji huu unauhusiano na
mambo ya kishirikina au kichawi kama ambavyo watu wengine
wanavyoaminishwa.
Mwisho kama kuna wanaodhani kuwa ndoto hizi
zimewadhuru kwa namna moja au nyingine, wafahamu kuwa kilichowadhuru si
kuota ndoto hizo bali ni wasiwasi wao unaotokana na kusikia na wala si
madhara kwa maana ya kuota kwenyewe, kwani ikiwa ni ndoto hata wanyama
kama Mbwa, Paka na Sungura nao huota wakifanya mapenzi, ushahidi ambao
unatosha kutupilia mbali hoja ya ndoto kutokana na majini
No comments:
Post a Comment