Kitendo cha kutongoza kina ufundi wake,
na wanaume walivyo wajanja (kwa wale wenye uelewa) wana maarifa yao ya
kutongoza. Maarifa hayo hutofautiana tegemeana na aina ya mwanamke
ambaye wananiya ya kumtongoza. Licha ya kuwa maarifa haya
yametofautiana, mwisho wa siku sababu za yeye kutongoza mwanamke huwa
mle mle – sababu za msingi hufanana na moja ambayo ni kubwa kuliko zote
ni tamaa.
Katika ulimwengu wa utongozaji mambo
yamebadilika sasa to the extent hata akina dada/mama huwa tunajilipua
once in a while. Ila ukweli unabaki bado kwa kiasi kikubwa wanao ongoza
kutongoza ni akina kaka/baba. Na katika kutongoza huko wengi huwa na
sababu mbali mbali za kumtongoza huyo mtongozwaji.
Zinazofuata ni sababu hizo zinazomfanya
huyo kaka/baba afanye maamuzi na kufanyia kazi malengo yake ya kumpata
huyo anae kuwa kadaka jicho lake. Hizi ni sababu tokana na mtazamo wangu
ambazo huwa vigezo vya sababu ya kutongoza mwanamke:-
Anakujaribu
Ni mara nyingi nimesikia kaka/baba zetu
wakiweka wazi kukubaliwa na mwanamke aliye mtongoza na kukubaliwa bila
kutarajia. Ni kuwa just for the sake of it, mazingira yanakuwa
yanaruhusu anajikuta kutongoza kwa kujifurahisha na kujaribu alafu
anajikuta mwanamke kakubali. Kama hajajipanga anatahamaki na hata
kushindwa kuendeleza azma ya kukutana naye kimwili hasa kwa vinajana
ambao hawana makazi badala yake hulelewa na familia hivyo kuwa na sehemu
ya kukutania na mwanamke kwa ghafla ni mtihani kwake. Mwingine
akikujaribu ukakubali atalala na wewe na hali mwingine atakupotezea na
mwanamke akibaki akishangaa inakuwa kakubali na hatafutwi.
Kakutamani
Hii ndio sababu inayo ongoza kwa sababu
zote za akina baba/kaka kutogoza. Uzuri, Urembo, Mvuto wa dada/mama
husika hucheza nafasi kubwa ya mtongozaji kuvutiwa hadi akataka kuwa na
wewe. Hii hutokana na ukweli kuwa kiasi kikubwa cha wanaume anapotongoza
malengo yake inakuwa kukupata na kuweza kufanya sex na mwanamke huyo.
Hata hivyo vivutio vimetofautiana, kuna wale wanafutiwa na miguu,
wengine sura, wengine midomo na wengine weengi makalio (kwa kaka/baba
zetu hawa wa kibongo).
Kakupenda
Hii ni mara chache, mara nyingi kigezo
cha kwanza mwanaume kutongoza huwa kuvutiwa na huyo mwanamke then
kupenda kunakuja baadae. Hata hivyo kuna exceptions; mfano kama vile
huyo mwanaume anapokuwa yupo mahala ambapo anakutana na huyo dada mara
kwa mara. Siku ya kwanza alipo muona hakuwa na wazo kabisa la
kumtongoza, ila with time kwa kuendelea kumuona pengine hata kwa
kuendelea kuwasiliana kama wana mazoea anajikuta kampenda tokana na
tabia or sababu zozote zile alizonazo hivyo kuamua kutongoza. Hii sababu
ina probability kubwa ya kuishia kwenye ndoa.
Ana ngunge (Horny) Anahitaji pa kupooza haraka
Ana hitaji kwenda kupoza hamu ya ngune
alilo nalo. Pengine anakuwa hajakutana na mwanamke muda mrefu au tu ni
aina ya mtu ambaye ana hamu kila mara au kila akiona aina ya mwanamke
ambae kamtamani. Hivyo mwanaume kutongoza kwa kigezo hiki ina maana huyo
mtongozwaji ndiyo akaonekana chaguo zuri la kuweza kuubali haraka bila
uchelewefu wa kwenda kukutana kimwili. Mara nyingi hii hutokea kwa
mwanamke ambae ni kazi yake hio (yaani dada poa) au yule anayejulikana
mtaani kama mama Huruma.
Wa ku beep/Hamaanishi
Huyu ni aina ya yule mwanaume ambae
hayupo committed. Yeye siku zote anakuhitaji wewe siku akitaka kukutana
kimwili. Yaani mara nyingi anacheza na hisia zako.. Anakuwa anakujua
vema… Namna ya kukuweka sawa, namna ya kuahakikisha huna wasi wasi juu
yake na namna ambavyo kukutana na wewe ni lazima siku ambayo anataka
kufanya na wewe uone kawaida. Anaweza akawa hata na galfriend/mke huko
but akawa na mwingine kwa ajili ya sex tu.
Kukuoa
Hii utokea pale mwanaume anapokuta
mwanamke katimiza vigezo anavyotaka kwa mke wake, kama vile utulivu,
upole, usafi, aina ya kazi n. k. Inakuwa kamjua tabia yake (iwe kwa muda
mrefu ama mfupi) na zikamvutia kutaka kuwa nae kwa muda mrefu zaidi
tena kama mke na mume kabisa. Hii ni mara chache, mwanaume huja mpole
sana, sex inakuwa si priority sana. Yupo haraka kutaka kukufahamu zaidi
wewe na familia yako na anakuwa na bidii ya kutaka kuhakikisha hata
upate mimba mara moja.
Mahusiano
Huyu anapenda kuwa safe. Anataka mwanamke
wa kuwa nae pamoja kama partner, awe rafiki, waweze kukutana kimwili na
wawe waaminifu. Mara nyingi anakuwa kalenga wewe ndio uwe the special
lady. Hata ikitokea ana wengine mwisho wa siku huyo mwanamke wa kujenga
nae mahusiano anakuwa makini zaidi na invest zaidi katika huo uhusiano..
Mara nyingi ikienda vizuri hata huishia katika ndoa.
Kukuchuna/Kukutumia
Huyu mwanaume anataka mwanamke anae
onekana una uwezo wa kujikimu kila kitu. Unaonekana independent na huoni
taabu kum support mwanaume. Hivyo hutaka wepesi… Haoni taabu siku ya
kwanza mmetoka ama siku zingine zote wewe ukitop up the bill ziku zote.
Kwake anakuwa so set on enjoying bila kujali partnership ya kweli katika
mahusiano hayo.
Kukuzalisha
Hii ni nadra.. Siku hizi kaka/baba zetu
anakutamkia kabisa… Hasa hawa ambao hawataki ku commit na kuoa. Ma
senior bachelors. Inafika wakati anajua kabisa mke sitaki, but nataka
niwe na mtoto so the shortcut anatafuta mwanamke mwenye mwelekeo wa kuwa
mama mzuri, tena kwa kiasi kikubwa awe anajiweza kuweza kulea mtoto na
anakushawishi ubebe mimba. Pengine hata kwa uongo wa nitakuoa. Ingawa
hii ni wachache sana.
Wa kuzugia
Mwanaume wa namna hii ni yule anataka
mwanamke kwa sababu si ya dhati. Kwa kiasi kikubwa anakuwa na huyo mtu
kwa sababu maalum. Mfano; anaweza kuwa yupo gay, hayupo tayari sexuality
yake ijulikane hivyo anatongoza mwanamke wa kuwa nae (wengine hata kuoa
kabisa) ili nae aonekana ana mwanamke na hivyo mwanaume wa kawaida
katika macho ya watu.
Ujumbe kwa akina dada/mama wenzangu:-
Kuna wakati ni mtihani kujua mwanaume
anakutongoza kwa ajili gani. Ila siku zote tunacheza na insticts na
pengine kuingia katika mahusiano kana kwamba wacheza kamali. All in all
kuna wale ambao wapo so obvious na ni rahsi kujua sababu ya yeye
kukutongoza. Faida ya kujua hilo ni wewe kutoa maamuzi kama upo tayari
uwe nae kwa vigezo ambavyo vimemfanya aje kwako.
Usikose kukutana namimi katka makala ijayo….
No comments:
Post a Comment