Upo kwenye mahusiano ya Kimapenzi? Unahisi unapendwa na mpenzi wako? Haya ni mwaswali ya kujiuliza kuelewa hii Makala.
Katika mahusiano wengi kama si wote hupenda kuelewa mpenzi wake anampenda kiasi kipi, pengine saa ingine hata kutamani angekuwa na uwezo wa kuona nafsi ya mpenzi wake huyo ni kwa kiasi kipi penzi hilo limetawala; bahati mbaya ama nzuri haiwezekani. Hata hivyo kuna dalili katika mahusiano kati ya wawili ambazo uashiria endapo mpenzi wako huyo anakupenda ama lah. Hii huambatana na kutokana na tabia na nyenendo za mpenzi wako huyo dhidi yako.
Katika mahusiano wengi kama si wote hupenda kuelewa mpenzi wake anampenda kiasi kipi, pengine saa ingine hata kutamani angekuwa na uwezo wa kuona nafsi ya mpenzi wake huyo ni kwa kiasi kipi penzi hilo limetawala; bahati mbaya ama nzuri haiwezekani. Hata hivyo kuna dalili katika mahusiano kati ya wawili ambazo uashiria endapo mpenzi wako huyo anakupenda ama lah. Hii huambatana na kutokana na tabia na nyenendo za mpenzi wako huyo dhidi yako.
Baadhi ya viashiria ambavyo vinaweza kukusaidia katika kutafakari ama kutambua endapo Mpenzi wako huyo ni kweli anakupenda.
Mawasiliano egemezi kati yenu (Communication)
Hii ni mawasiliano kwa njia za viwezesha
mawasiliano hasa simu. Sasa hivi mawasiliano yamerahisishwa mno ikiwa na
njia nyingi kama vile kupiga simu, njia za messages hasa kama vile
Whatsapp, Viber, Skype na text messages. Kwa yeyote aliye na simu ya
mkononi ni rahisi kuwasiliana na mpenziwe wakati wowote ule. Mawasiliano
ni njia moja wapo ya muhimu sana katika kujenga na kuboresha
mawasiliano kati ya wapenzi. Inapotokea mawasiliano hayo yame elemea
Zaidi upande mmoja siku zote; hapo kidogo ni tatizo. Kimsingi
mawasiliano hupaswa kuwiana (mtu na mpenzi wake wote watafutane kwa
usawa) ingawa inaweza pishana kidogo tokana na sababu mbali mbali. Ila
inapotokea siku zote mpenzi wako huyo katka mawasiliano hufanya haya;
– Hakutafuti siku zote hadi uanze wewe.
– Kukukatia simu na kukuzimia bila maelezo yoyote ya msingi.
– Kuwa mkali kila ukimtafuta, kukuonyesha kana kwamba simu zako kwake ni kero.
– Kuchukua mda mrefu kujibu jumbe zako ama kutojibu kabisa na hata ukimuuliza hakuna sababu za msingi.
*Kwa baadhi ya tabia hizo katika
mawasiliano ni dalili ambazo zinachangia kuonyesha kuwa mpenzi wako huyo
hakupendi. Na hasa ikiwa tabia hizo zote anazo zote.
Ushirikiano egemezi kati yenu
Ushirikiano ni muhimu baina ya wapenzi
katika masuala yale ambayo ni msingi katika maisha yenu; kila mmoja
anapaswa kushiriki na kujitoa kwa mpenzi wake kwa yale yote ambayo
huitaji ushiriki kwa mpenziwe. Ushirikiano hu upo wa aina mbili.
Kuna ushirikiano wa hali:-
Ushirikiano huu ni
namna ambavyo wewe na mpenzi wako hushirikiana hasa katika mambo ya
kijamii, kijamaa, kifamilia nakadhalika; ya wale na vile
vilivyokuzunguka. Ikiwa pale unapokua na tatizo kama vile
kuugua/kuuguliwa, misiba ama matatizo mengine yoyote yeye siku zote ana
sababu za kushindwa kuwa karibu yako. Na ikitokea akapata nafasi yupo
juu juu akionyesha dalili za kutokua comfortable kua hapo.
Kuna ushirikiano wa Mali:-
Ushirikiano huu ni
namna ambavyo wewe na mpenzi wako hushirikiana linapokuja suala la
kujitoa kwa vitu vihusuvo pesa bila kujalisha kipato cha mwenzako. Ikiwa
una mpenzi wako akawa na shida ama kuhitaji msaada wa kifedha ama
unaohususha matumizi ya fedha (bila kujalisha ni mwanamke ama mwanaume)
huwa ni muhimu kutoa msaada huo; hasa pale ambapo ni wazi kabisa mwenzio
anakuwa amekwama. Kuna baadhi ya wapenzi hawezi toa msaada wa mali
hata kidogo; ingawa naamini kuwa mtu yeyote yule anapokua na mtu
anampenda sana ni lazima atataka kumsaidia mwenzie wakati wa shida.
Taratibu za kuonana (Meetings)
Katika hiki kipengele cha Kuonana kipo katika maeneo mawili pia.
Nafasi yake ya kukuona:-
Mtu yeyote hata kama yupo na majukumu
kiasi kipi, akimpenda mwenzie (iwe kwa mwanamke ama mwanaume) atatafuta
tu muda kwa ajili ya kuwa na mpenzi wake. Haijalishi huo muda utakua
mfupi ama mrefu, dakika chache ama masaa, ila tu lile wazo la kutomuona
mpenzi wake kwa muda mrefu na hali yupo karibu na ana uweo huo
linamkosesha raha. Ikiwa mpenzi wako yupo karibu, na unajua fika
anauwezo wa kukuona na kuwa na wewe mara kwa mara lakini haipo hivyo –
hiyo inaweza kuwa moja ya dalili ya kutopendwa na huyo mtu (labda kuwe
na sababu za msingi na iwe ni kitu cha kupita na si tabia yake).
Maeneo ya kuonana:-
Hii inahusu mpenzi wako kutotaka ufike
kwake (na hali pengine anakaa peke yake ama yeye ndiye mmiliki wa
anapoishi). Siku zote atataka aje kwako ama mkutane sehemu za maficho.
Pia linahusu yeye kutotaka kuonekana na wewe kwa watu ama katika jamii.
Yupo radhi siku zote mkutane mahala na kila mmoja aondoke vyake, ama
kama ana usafiri akuchukue toka utokapo hadi pale mnapoelekea.
Kutokuwa na chembe ya Wivu dhidi yako
Wivu ni kiungo muhimu sana katika
mahusiano, mwanadamu hachagui ni wakati upi awe ama asiwe na wivu, hilo
lipo ndani yetu na ni kitu ambacho hakizuiliki ikiwa kweli mtu wako
wampenda. Kinachotutofautisha wote ni viwango vya wivu na namna/wapi wa
kuonyesha huo wivu. Wivu haimaanishi kuwa mtu hajiamini ama kuwa ndio
hampendi mwenza wake; wivu huja ‘naturally’ mana unapo mpenda mwenzako
kiukweli kwa ni wazi kua mapenzi ya kweli ya viwango vya wivu ndani yake
na kutaka chako kiwe chako peke yako na hivyo kutaka kukilinda chako
kubaki chako siku zote.
Inaptokea mpenzi wako hana habari kabisa,
na wala hashtuki ni wazi kuwa anaweza kuwa asiwe anakupenda vile
ambavyo mhusika ungetaka. Ikiwa yeye haisumbui kabisa ukiwa na wengine,
akikukuta na wengine, akihisi upo na wengine hapo ni wazi kuwa hakuna
mapenzi yale ya dhati.
Hata hivyo ni muhimu sana kutoendekeza
wivu katika mapenzi na kuwa makini kiasi cha wivu dhidi ya mpenzio. Wivu
kwa kiwango ni chachu katika mapenzi, Wivu uliokithiri huwa kero tokana
na tabia ambazo huambatana na wivu huo ambao mwisho wa siku huwa karaha
na kero katika mahusiano.
Kutokutambulisha kwa Ndugu, Jamaa & Rafiki
Kawaida wengi wa wenye wapenzi ambao
haswa wanawapenda, hutaka ndugu, jamaa na marafiki zao wawajue na mara
nyingi hata kutambulisha kabisa kuwa ni mtu wake. Ikiwa upo katika
mahusiano na mtu wako hapendi kukutambulisha kwa watu wake wowote katika
maisha yake hilo nalo linaweza kuwa ni tatizo. Ingawa wengi huwa rahisi
kukutambulisha kwa marafiki maana yeye pamoja na marafiki zake hujuana
kwa viremba.
Sababu za Kukutafuta zinamhusu yeye tu (Selfish reasons of Meetings)
Kila akikutafuta anakutafuta sababu tu anashida toka kwako.
Kwa wanawake mara nyingi inaweza kuwa
anashida toka kwako ya kitu Fulani, ama kufanyiwa kitu Fulani ama shida
ya pesa. Nje ya hapo hahawahi kukutafuta kwa sababu tu kakukumbuka, ama
sababu tu anataka kupumzika na wewe ama sababu yoyoye ile ambayo
haimnufaishi yeye tu. Wapo na wanaume ambao pia wana wapenzi wao
wanawatumia na kila wakiwatafuta inakuwa ni sababu tu wanataka kitu ama
fedha toka kwa wapenzi wao.
Kwa wanaume hii mara nyingi huwa shida
yake kubwa kwako ya kuonana ni kutaka kukutana kimwili. Na akishamaliza
hapo basi kuonana ni tatizo hadi pale tena atakapotaka kukutana na wewe
kimwili.
Anavyokuita hasa majina mbadala (The way they address you)
Hii inahusu namna atakavyo kuita mkiwa
wenyewe ama mbele za watu. Kuna watu wasio na haya na ukimchekea anaweza
hata muita mpenzi wake mbele yake na hata kwa wenzie majina kama demu
(kwa mwanamke) ama buzi langu (kwa wanaume). Hii ni mifano tu, kuna aina
ya majina mengi ambayo si busara kuyatumia, na ambayo naamini mtu
ambaye anampenda na kumthamini mpenzi wake hawezi yatumia iwe yupo na
mpenzi wake ama hayupo na huyo mpenzi wake.
Namna anavyo Kuthamini/Kujali/Kuheshimu
Ikiwa mpenzi wako hakujali, hakuheshimu,
hakusikilizi, hakuweki kipau mblele pale panapostahili ina maana kuwa
hakuthamini. Kuthamini huja tu pale ambapo kuna mapenzi ya kweli dhidi
ya mtu wako. Ni kitu ambacho huwezi kulazimisha, na hata ukilazimisha
kwa siku chache mwisho wa siku mhusika atachoka kujifanya anakuthamini
na hali hakutamini. Thamini inatokana na neon thamani… Kile kilicho na
thamani siku zote mtu kukitunza kwa uangalifu, upendo na kujali kwa hali
ya juu sana. Mtu anaye kuthamini ni lazima atakuheshimu na kukukali,
ila si lazima kuwa mtu anaye kujali na kukuheshimu atakuthamini. Mpenzi
wako akikuthamini, siku zote atakua karibu na wewe, atajali hisia zako,
atajali afya yako na atajali yote yale ambayo ni msingi kwako na wale
wote waliomzunguka.
Tendo la ndoa (Sex)
Hili la tendo la ndoa linaweza kutazamwa kwa namna mbili
*Ikiwa hashirikiani na wewe kwa lolote
lile (hali na mali), hakuthamini na tabia zote ambazo huonyesha
kutofurahia kuwa na wewe wakati wowote ziku zote LAKINI linapokuja suala
la kukutana kimwili ndio hulipa kipaumbele. Hapo ni tatizo. Inakuwa ni
wazi hukuhitaji tu kwa sababu ya kukidhi haja zake za kimwili.
*Ikiwa hashirikiani na wewe kwa lolote
lile (hali na mali), haonyeshi kuthamini na tabia zote ambazo huonyesha
kutofurahia hayo mahusiano hasa kama pia ana tabia ya kukutafuta tu pale
ambapo yeye ana shida; inapotokea ukitaka kukutana nae kimwili
anasita/hapendi/hafurahii ama kutokua na ushirikiano mzuri katika tendo –
hapo ni wazi pia kuwa hakupendi ila anakutumia tu.
MSOMAJI NAOMBA ZINGATIA
Mawazo yangu ya nakala hii ni muhimu sana
na ina nguvu Zaidi kwa wale ambao wapo katka mahusiano kati ya wawili.
Kwa maneno mengine, ikiwa upo katika mahusiano ambayo unajua kabisa kuwa
nyie kama wapenzi wa huyo mpenzi wako mpo Zaidi ya mmoja kuna masuala
ambayo yametajwa hapa na hayawezi tumika kama kigezo cha kuelewa endapo
mpenzi wako huyo ni kweli anakupenda ama lah.
Ikiwa unahisi mpenzi wako hakupendi,
hiyo si lazima ikawa ticket ya maamuzi ya kusonga mbele. Unaweza chukua
baadhi ya hatua ili kuboresha hayo mahusiano na yakaenda kwa mtindo
ambao wote wawili mnaweza yafurahia. Ikumbukwe kuwa kila mmoja anapo
ingia katika mahusiano huingia na mtu mwenye tabia mpya, jamii
iliyomsunguka mpya na kadhalika; na hivyo kuanza upya kuyajenga
mahusiano mengine. Hivyo ni bora ukajitahidi kurekebisha ulipo (hasa
kama kweli unampenda) na pale inaposhindikana yapaswa ukubali na kusonga
mbele.
Ndugu msomaji naona maoni yako, mitazamo
yako, kama kuna mahala hukubaliani, kama kuna mahala pa kuongeza ama
lolote lile ushiriki katika huu mjadala.
No comments:
Post a Comment