Kwenye
dunia ya mapenzi ya sasa kuna mambo mengi sana ambayo huwaliza kama sio
kuwakosanisha wapenzi na mwisho wa siku wakaachana na kuacha simanzi
mioyoni mwao, Miongoni mwa mambo makubwa yanayosababisha wapenzi
kuachana ni pamoja na USALITI.
Kwa leo
tujaribu kuangalia kwa upande wa wanawake, ni kitu gani/ni dalili gani
ukiziona basi ufahamu kuwa mwanamke uliyenaye anakusaliti na kuna
uwezekano usiwe na maisha marefu ya kimapenzi naye.
Hizi ni
baadhi ya dalili kuwa mwanamke uliyenaye amechoka aina ya mapenzi
unayompa na anataka kuondoka na anakusaliti ikiwa ni njia mojawapo ya
kutimiza nia yake;
1.
Kama akianza ghafla kujijali kupita kiasi kwa
muonekano wake basi unatakiwa kuanza kumtilia shaka, kwa kipindi chote mmekuwa
pamoja amekuwa ni mtu wa muonekano unaoendana nawe lakini ameanza kutafuta
muonekano mpya na tofauti kabisa na ule ambao umeuzoea na unaoupenda, anaweza
kuwa ameanza kuwa na muonekano tofauti kwa sababu amepata mtu ambaye angependa
awe vile, anaweza kuwa mfanyakazi mwenzake, mwanafunzi mwenzake, mfanyabiashara
mwenzake na hata bosi wake.
Ameanza na kwenda gym ili kuweka mwili
kwenye shape tofauti na ile uliyoizoea na unayoipenda wewe, amekuwa ni mtu wa
make up hata kama anataka kwenda kununua vocha tu dukani nje, anza kuwa makini na
mienendo hii, inaweza kuwa ni mabadiliko ya kawaida na pia inaweza kuwa
mabadiliko yasiyo ya kawaida.
2.
Mwanzoni alikuwa ni mtu wa kuwapenda watu wako
wa karibu wakiwemo ndugu zako na marafiki zako lakini kwa sasa
amepunguza
kabisa kuwa nao karibu kama sio kuacha kabisa, anakuwa anaogopa na kuwa
na
wasiwasi kwa kuwa nao karibu tena atashtukiwa kuwa anakusaliti kwa hiyo
anaona
njia nzuri Zaidi ni kuwa na excuse kila mara marafiki zako au ndugu zako
wanapomhitaji kuwa naye siku za kawaida au weekend au hata kuwasaidia
kwenye baadhi ya vitu ambavyo mwanzoni ilikuwa ni rahisi kutoa msaada
kwao.
3.
Mabadiliko mengine utayaona kwenye kufanya
mapenzi, mlishazoea kufanya mapenzi mara mbili kama si mara tatu kwa wiki na
amekuwa ni mtu muwazi na anafurahia sana mapenzi lakini ghafla anaanza kuwa ni
mtu wa kukimbiakimbia linapokuja suala la kufanya mapenzi, anakuwa hayupo
comfortable na haonyeshi kuyafurahia tena mapenzi yenu,
Kwa manaume kama
anaenda nje ya mahusiano na msichana huwa anapenda Zaidi kufanya mapenzi na
huyo mpya aliyempata lakini pia haoni aibu kufanya na wewe mwanamke wake wa
zamani kiasi kwamba unaweza kutokufahamu upesi kama anakusaliti/Inachukua muda, lakini kwa
mwanamke hali ni tofauti, akianza kukusaliti hata akiwa kwako anakuwa
anajisikia vibaya na kama umemzoea kupita kiasi utamshtukia kuwa hayupo sawa.
Kutokutaka kufanya mapenzi nawe ni dalili
tosha kuwa hayafurahii tena mapenzi yenu na haridhiki nayo,anaona kama
unamghasi tu na anatamani aondoke.
4.
Mwanamke aliyekuchoka ana anayetamani kuondoka
kwako kwa kuwa amepata mtu mwingine ataacha kukujali kama zamani, vile
vitu ulivyozoea
akufanyie vitapungua sana kama sio kuisha kabisa, ataanza kuwa na sababu
ukimwambia akusaidie kitu, kama alizoea kuja kwako na kufanya usafi wa
nyumba basi itapungua kama sio kuisha na hutakumbushwa vitu muhimu
vya kimaisha vya kufanya na kuna wakati unaweza kumkosea na akakuacha tu
bila
kuhangaika kukurekebisha kama zamani.
5.
Mwanamke anayekusaliti ataanza kupunguza ule
uwazi aliokuwa nao kwako, kuna baadhi ya mambo ambayo alikuwa anayafanya kwa
uwazi sana mbele yako lakini kwa sasa ataanza kuyafanya bila uwazi na kuna
wakati asikushirikishe kabisa, mwanzoni alikuwa anaweza kuacha simu au laptop
mbele yako na asiwe na wasiwasi lakini kwa sasa anakuwa ni mtu wa
kujifichaficha na anaziwekea password simu na laptop na hata uongeaji wake wa
simu unakuwa tofauti na zamani na anakuwa ni mtu wa kuwa bussy muda mwingi na
simu kuliko zamani akiwa mbele yako/mkiwa wote.
6.
Zamani ilikuwa rahisi sana kumpata pale
unapomhitaji iwe face to face au hata kwa simu, lakini hali kwa sasa imekuwa
tofauti. Amekuwa ni mtu wa kuwa bussy kila wakati na kuna wakati unapiga simu
haipokelewi na unaweza kukaa masaa nane ndo unajibiwa meseji yako na hali hii
inatokea mara kwa mara na kila ukimuuliza alikuwa wapi kujibu simu au kujibu
meseji anakujibu hakuisikia ikilia au iliisha chaji. Fahamu hapo kuna mtu
mwingine amechukua nafasi yako na unatakiwa kuanza kujiandaa kwa safari mpya.
7.
Kuna jina jipya la mwanaume limekuwa halikauki
mdomoni kwake na ukimuuliza maswali kumuhusu huyo mtu amekuwa ni mtu wa
kumponda kwa sababu hataki umjue vizuri na hataki uendelee kumuulizia akijua
utamshtukia, unatakiwa kuanza kufuatilia nyendo zake kwa huyo mtu kwani ni
dalili tosha kuwa ameanza kutoka nae au yupo njiani kutoka nae, ukimuuliza Zaidi
atakwambia ‘’ni rafiki tu’’ na usiwe na mashaka naye.
8.
Zamani ilikuwa ukimkosea anakuwa ni mwelewa na
anachukua muda mfupi kukusamehe na kuendelea na furaha yenu ya mahusiano,
lakini kwa sasa amekuwa ni mtu wa kukutafutia makosa kila wakati na ikitokea
umekosea kidogo tu ataufanya ugomvi wenu kuwa mkubwa kuliko maelezo na anakuwa
ni mtu wa lawama tu bila kutafuta suluhisho la ugomvi wenu, ukianza kuona
dalili hizo hakikisha unaanza uchunguzi mapema ili usije kulia mwenyewe.
9.
Kuna wakati mwanamke akitaka kukusaliti anaanza
kuwa interested sana na ratiba zako za kila siku kiasi kwamba unaweza kudhani
anakujali kupita kiasi kumbe anataka kufahamu muda Fulani utakuwa wapi ili
aweze kukusaliti vizuri, njia nzuri ya kumkamata ni kumwambia utakuwa sehemu Fulani
na utachelewa lakini ukafanya kitu tofauti na ulichomwambia, unaweza kukuta
unaliwa chakula chako na ulikipika mwenyewe, kuwa makini.
10.
Zaidi ya yote, dalili mojawapo kuwa mwanamke
wako anakusaliti ni pale Unapoanza kuhisi ndani ya nafsi yako kuwa mambo
hayaendi sawa kwenye mahusiano yenu kama zamani, hisia zako zinakuambia kuwa
inawezekana mwanamke wako akawa anakusaliti, hii ni dalili nyingine kuwa kuna
kitu unatakiwa kukifanya kwenye mapenzi yako, kuna wakati hisia huwa
zinasababishwa na mienendo tofauti ya mtu wako na mara nyingi hisia hukupeleka
kwenye ukweli.
No comments:
Post a Comment