1.
Kila Mara Ukiwa nae ndani na mnafanya
mapenzi au anakubusu , anajisahau na kukuita jina lisilo lako, huyo bado
hajatulia na hajakuweka kwenye mipango yake bado, MUACHE, ukilazimisha sana
utapotea.
NB; Kumbuka Kuwa Kuna Mtu Maalum Kapangwa Kwa Ajili Yako, Muda Utafika Tu Na Utapata Furaha Unayoitafuta, Usiogope Kuanza Upya Kama Ulipo Hapakufai.
2.
Upo nae lakini kila mara unapowaza
mipango yako ya baadae humuweki kwenye mipango yako na hata unapokuwa unapokuwa
naye mawazo yako muda mwingi yanakuwa mbali, HUYO SI CHAGUO LAKO, Muache
uendelee na safari.
3.
Kila unapokuwa naye, Simu yake inakuwa
yake na simu yako inakuwa yake pia, anasoma sms na kuwa mkali sana kwenye simu
yako ilhali yako wake huruhusiwi hata kuigusa, HAKUFAI huyo ni Player, Trust
Me.
4.
Kila unapokuwa na ugomvi nae kila siku
wewe ndio wa kumuomba msamaha hata kama yeye ndio amekukosea, huyo hawezi kuwa
na upendo wa kweli, mapenzi ni kusikilizana pande zote mbili na si kwa upande
mmoja kuonewa kwa kila kitu.
5.
Kuvaa ni njia mojawapo ya kujiamini kwa
mwanamke, lakini inapotokea anakupangia kila vazi unalotakiwa kuvaa na
usilotakiwa kuvaa hapo inakuwa sio sawa, huwezi kutoka kwenda shule, kazini,
outing, na kwingineko mpaka aone ulichovaa.
6.
Anakuchagulia watu wa kuwa nao ikiwa ni
pamoja na marafiki, hii sio dalili nzuri, wanaume wanaotenda ‘’madhambi’’
pembeni ndo huwa na tabia hii kwa wingi, wewe unakuwa ni mtu wa kubadili
marafiki kila kukicha.
7.
Linapokuja suala la pesa mara nyingi huwa
hakuna undugu, mara nyingi amekuwa ni mtu wa kukukopa pesa lakini anajifanya
‘’Kusahau’’ inapokuja muda wa kulipa deni, sio dalili nzuri ya mwanaume
anayekufaa, una mipango yako binafsi ukiachilia mbali mapenzi na yeyote
atakayesababisha mipango yako kutosogea mbele hatakiwi kuvumiliwa.
8.
Mapenzi yake kwako huongezeka pale tu
anapokuhitaji kwa ajili ya kutimiza haja zake za Ngono na anapomaliza hukusahau
na kukupotezea, hakufai kabisa huyo mtu.
9.
Kila unachomwambia hukusikiliza na
kukubaliana nawe lakini inapokuja wakati wa kutekeleza kwa vitendo
mlichokubaliana mambo huwa tofauti, ANAKUDHARAU na anajisemea moyoni ‘’Bora
Liende’’, Hakufai.
10. Hawezi
kila kitu cha jikoni, hawezi kuosha vyombo hata kikombe cha chai, hawezi kupika
hata chai, hawezi hata kufua nguo zake za ndani na anaona kama kazi hizo zote
ni za wanawake tu, umejaribu sana kumuelekeza na haonyeshi mabadiliko, Kimbia.
NB; Kumbuka Kuwa Kuna Mtu Maalum Kapangwa Kwa Ajili Yako, Muda Utafika Tu Na Utapata Furaha Unayoitafuta, Usiogope Kuanza Upya Kama Ulipo Hapakufai.
No comments:
Post a Comment