1# Kukosa siku zako za hedhi
Unaona mwezi mmoja ama zaidi umepita bila kuona siku zako za hedhi
yawezekana utakuwa umenasa ujauzito,maana mtu mjamzito hawezi kupata
hedhi mpaka atakapojifungua,kukosa hedhi pia husababishwa na sababu
zingine kama kubadilisha mazingira,vyakula stress na mengine
2# Kichefuchefu na kutapika
Wakati mimba inapoanza kutunga kuna homoni ambazo huwa zinafanya kazi na
huweza kusababisha kichefuchefu kwa mama mjamzito hali hii humfanya
apate wakati mgumu kula baadhi ya vyakula,hii mara nyingi huanza wiki ya
sita ya ujauzito japo hali hii si kwa kila mjamzito.
3# Kujisikia haja ndogo mara kwa mara
Muda si mrefu baada ya kushika ujauzito homoni hubadilika na huchochea
msukumo wa damu na kupelekea mjamzito kujisikia kwenda haja ndogo za
mara kwa mara
4# kubadilikabadilika kwa mood
Ni ile hali maarufu kwa wajawazito kubadilika hisia mara kwa mara
saikolojia yao hubadilishwa na homoni za ujauzito na hujikuta wanakuwa
na vituko vya kushangaza maana kuna wakati unaweza kuwa unacheka na
mjamzito ila ghafla ananuna ama kulia au kukumbwa na hali ya uoga bila
sababu yakueleweka,kama wewe ni mwanaume inabidi umvumilie tu mwanamke
wako ,maana hali hii hutokea bila wao kupanga
5# Matiti kuvimba na kujaa
Wakati wa ujauzito matiti huweza kujaa hii huwa ni kwa ajili ya kuandaa
chakula cha kiumbe kilicho tumboni kwa mama mjamzito hivyo chuchu huweza
kusimama
6# kusumbuliwa na harufu mbalimbali
Hasa kama unapata mimba kwa mara ya kwanza utachukia harufu za vyakula
na vinywaji au hata marashi ya aina fulani,wakati mwingine hata harufu
za watu wa karibu na wewe
7# Kujaa mate mdomoni
Hii huchochewa na homoni za ujauzito hivyo mama mjamzito hujikuta
anajawa na mate mdomoni yanayompelekea awe anathema mate mara kwa mara
8# Uchovu
Mara nyingi mwili wa mjamzito hupitia mabadiliko mbalimbali ambayo
humfanya awe mchovu mara kwa mara na kujisikia vibaya kama mtu mwenye
dalili za kuugua
9# Kusinzia ovyo
Uchovu anaoupata mjamzito humpelekea kupata usingizi wa mara kwa mara
tofauti na hali yake ya kawaida kabla ya uzito ,anaweza kuwa na usingizi
wa ghafla na mara kwa mara kama mtoto mchanga.
10# Kupata vitone vya damu sehemu za siri(spotting)
Kuna wakati unaweza kupata damu kidogo sana sehemu za siri kitaalamu
hujulikana kama implantation bleeding,haijulikani hasa kwanini damu hii
kidogo huwa inatoka wakati huu,ila mwanamke 1 kati ya 4 huweza kupata
damu hii, wakati mwingine damu ya namna hiyo huweza kuwa dalili ya mimba
iliyotunga nje ya tumbo la uzaziectopic preginancy
11# Joto la mwili hupanda kuliko kawaida
Kama ulikuwa unaweka kumbukumbu ya joto la mwili utaweza kuona joto la
mwili wako linazidi kupanda kila siku kwa siku 18 na zaidi ,yawezakuwa
umenasa umenasa.
12# Chuchu kubadilika na kuwa nyeusi
Chuchu zako zinaonekana tofauti kwa sasa? huwa inatokea mara nyingi
wiki ya 10 ya ujauzito chuchu hubadilika rangi na kuwa nyeusi hali
inayochochewa na homoni za mimba
13# Maumivu kwenye matiti
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini
huongezeka wakati yai linavyopata rutuba jambo ambalo huongeza wingi wa
damu na kufanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kuwa
kawaida
14# Tumbo kujaa gesi
Utaona baadhi ya nguo zinaanza kukubana hasa sehemu ya tumbo manake
homoni za ujauzito tayari zinakuwa zimeanza kutanua tumbo ,hivyo mara
nyingi unakuwa unajisikia tumbo limejaa gesi
15# Kutamani kula vitu mbalimbali
Kutokana na mabadiliko yanayojitokeza ndani ya mwili yanayosababishwa na
homoni za ujauzito mwanamke hujikuta akitamani kula vitu mbalimbali
tofauti na mazoea yake mfano kula udongo,limao na kadhalika ili kukidhi
mahitaji ya mwili wake kutokana na mzigo alionao.
16# kukauka mdomo au kuchanika
Wanawake wengine muda mfupi baada ya mimba kutunga huweza kuona
mabadiliko kama mdomo kukauka sana ama kuchanika hivyo kumpa wakati
mgumu hata kama akipaka mafuta huweza kukauka baada ya muda mfupi tu
17# kuumwa kichwa mara kwa mara
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kuuma kwa kichwa japokuwa si
sana,hususan katika wiki za mwanzo za ujauzito hata hivyo hali hii
hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni zinazotokana na
ujauzito.Ikumbukwe kuwa kila mwili wa mwanamke upo tofauti hivyo si
dalili zote unaweza kuzipata.
No comments:
Post a Comment