Kubali au usikubali kwamba kila kitu kina uzuri na ubaya hivyo hata kwenye suala la kutokuwa na mpenzi kwa muda mrefu lina ubaya na uzuri wake,leo nitaongelea upande wa mathara yampatayo mtu anayekaa kwa muda mrefu bila kuwa na mpenzi kuna mathara ya kisaikolojia yanayoweza kumpata.
1# kujikuta unajenga tabia ya kujichua(masturbation)
Vijana wengi sana hujikuta wakikubwa na hii tabia ya kujichua ili
kuridhisha hisia na miili yao tabia hii hufikia mahali inakuwa kama
ulevi ambapo kuachana nayo inakuwa vigumu,vilevile ikumbukwe kuwa tabia
hii inamadhara kiafya maana huwa inalegeza misuli ya uume na kusababisha
baadaye unapoingia kwenye ndoa kushindwa kumtimiza haja ya mwenza wako.
2# Msongo wa mawazo
Hili linatokana na kukosa mtu wa karibu unaeweza kumshirikisha jambo
lako la ndani unajikuta unatumia muda mwingi kwenye kuwaza matatizo
yako pia utakuta unashindwa kuwashirikisha marafiki zako kwa kuhofia
kuchekwa hali inayoweza kushusha kiwango chako cha uchapakazi.
3# Kutojijali katika uvaaji na hata simu yako
Mara nyingi mtu akiwa kwenye uhusiano huweza kujiweka vizuri mwili wake
na mavazi inapotokea unaishi pekee yako tu hali hii inaweza kupotea pia
unaweza kujikuta unalalamikiwa kwa kutopokea simu mara kwa mara maana
hakuna mtu anayekuweka busy na simu.
4# Ubinafsi na kufikiria nafsi yako tu siku zote
Mtu anapokuwa kwenye mapenzi huwa anajifunza kuthamini wengine
kuwafikiria kuwafanya wafurahi uwepo wake na kujali hisia za mwenziwe na
kadhalika hivi ndivyo kupenda kulivyo, kwa hiyo mtu anapokuwa hana
mpenzi hujikuta anaanza kujifikiria nafsi yake tu,wakati mwingine
hujikuta anakosa msukumo wa kujiimarisha kiuchumi.
5# Kupendelea kuangalia picha za uchi
Watu wa namna hii hujikuta wakijenga mazoea ya kuangalia picha za uchi
mitandaoni ama kwenye simu zao na kuna wengine hupendelea sana kupiga
chabo yaani kuchungulia watu wakiwa wanafanya mapenzi ama kusikiliza
story za mapenzi.
6# Hukumbwa na tatizo la kusahau sahau na kukakamaa kwa mgongo
Hii ni kutokana na kwamba mfumo wao wa kisaikolojia unakuwa hauko sawa
,wanawake hupendelea kudandia mambo yasiyowahusu pia kutokwa na damu
nyingi waingiapo hedhini pia huweza kuingiliwa kirahisi na jini mahaba
na wanaume hukakamaa migongo.
7# Kutengeneza tabia mbadala za ovyo kama ulevi
Tabia hii inakuwa mbadala wa kujiridhisha unapokuwa unataka faraja baada
ya kukubwa na msongo wa mawazo hivyo ili kujiweka sawa mtu anaamua
kulewa pombe ama kutumia madawa ya kulevya na bangi
8# Kutojiamini (loss of confidence)
Inafikia mahali mtu anapoteza uwezo wa kujiamini hata kuongea na watu wa
jinsia tofauti na yake anaona aibu,wakati mwingine kuanza doubt
mwenyewe labda anakasoro kitu ambacho kinaweza kuharibu mfumo wake wa
kisaikolojia.
9# Kukumbwa na upweke
Hasa inapotokea marafiki zako wote wako kwenye uhusiano wa mapenzi
kasoro wewe unajiona mpweke sana hakuna mtu wakumwelezea siri za moyo
wako na hisia zako kwa kuogopa kuchekwa na marafiki wanaokuzunguka
unafikia mahali unaona kama watu wanakutenga na unawezajikuta unachukia
watu wa jinsia fulani bila sababu.
10# Siku ukipata mpenzi utajikuta huna uwezo wa kutawala suala la mapenzi
Kutokana na kukosa uzoefu wa kutosha katika suala hilo utajikuta
linakuchukulia muda wako mwingi kufikiria na kukufanya urudisha nyuma
mambo yako mengi ya msingi,mapenzi yanaendesha sana watu wengine
wanaharibu kazi sababu ya mapenzi,wengine wanajiua kisa ni hayo mapenzi
hivyo mapenzi ukiyaendesha inakuwa jambo zuri ila omba yasikuendeshe
utageuka kituko mbele za watu.
No comments:
Post a Comment