Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama
wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini
kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe
kushiriki kwenye mapenzi hayo.
Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa,
wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa in return. Na siku zote
ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine
hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi
yanapokuwa machungu kwao.
Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli
kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila
siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa
pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina
yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini
ukakosa njia za kutatua.
Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya ukae na
mpenzi wako kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia mapenzi yenu popote
pale mtakapokuwa na mtakapoishi.
1.
KUWA NA MUONEKANO CHANYA (POSITIVE IMAGE) KWA
MPENZI WAKO.
Ukiwa Ni Mtu Wa Kuangalia Mabaya/Kasoro
Sana Kwa Mpenzi Wako Kuliko Mazuri Yake Hautakuja Kukaa Kwenye Relationship Kwa
Muda Mrefu Hata Siku Moja...Utaendelea Kubadilisha Wanaume/Wanawake Kila Siku
Na Mwisho Wa Siku Utajiona Huna Bahati Kwenye Mapenzi Na Wakati Unayeyaharibu
Mapenzi Yako Ni Wewe Mwenyewe...Hakuna Asiye Na Kasoro (Ukiwemo Wewe Mwenyewe).
Kwa Hiyo Muonyeshe Mpenzi Wako Mapenzi Bora Na Umrekebishe Pale Anapokosea Bila
Kuwa Na Lawama Mara Kwa Mara, Kuna Makosa Mengine Ni Madogo Sana Na Unaweza
Kuyarekebisha Kwa Kukaa Chini Na Mpenzi Wako Mkayamaliza Kwa Dakika 5 Tu Lakini
Wengine Huwa Issue Kubwa Kwao Na Kusababisha Mwisho Mbaya.
2.
SAMEHE NA KUSAHAU.
Unapomsamehe mpenzi wako kwa kosa lolote
alilokosa basi hakikisha umemsamehe kiukweli na ujitahidi kusahau kosa
alilotenda itasaidia uwe na amani ya moyo zaidi kuliko kumsamehe kwa usoni tu
lakini moyoni ukawa na Donge bado, hii hupelekea kupunguza mapenzi kwa kiasi Fulani
kwake na kujikosesha furaha ya mapenzi.Anapokosea siku nyingine usimkumbushe
kosa lake la nyuma kwa sababu itamfanya ajione mwenye huzuni na ajione kuwa
hakusamehewa.
3.
MPE NAFASI/UHURU MPENZI WAKO.
Mnapokuwa kwenye mahusiano jitahidini kwa
hali na mali kupeana nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa yale ya kitaaluma
zaidi na kimaisha.anapokwambia yupo kwenye kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na
umpe support ya kutosha kwenye kazi zake au biashara zake au hata masomo
yake.usipende sana kulalamika pale anapochelewa kurudi kazini au kutoka kwenye
biashara zake bali mpokee kwa upole na baada ya kupumzika ndipo muulize kwa
upole na kimahaba zaidi kwanini siku hizi anachelewa sana kurudi au kwenye
biashara zake au shuleni tofauti na zamani.Hii itajenga zaidi kuliko kubomoa
kwa kulalamika na kupayuka mbele yake na huku yeye akiwa hata hajapumzika na
itamfanya siku nyingine aione nyumba chungu kitu ambacho si kizuri kwenu wote
wawili.
4.
KUWA MBUNIFU KWENYE MAPENZI.
Napozungumzia ubunifu hapa nakuwa
simaanishi kwenye upande mmoja tu wa kwenye yale mambo yetu ya chumbani,
hapana. Hapa namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ndani na nje ya nyumba,
jitahidi mara kwa mara kubuni vitu vipya vitakavyofanya azidi kukupenda na
kukuona kama mpya kwake kila siku. Kama amezoea kupata zawadi za aina Fulani kutoka
kwako basi jitahidi siku moja kumbadilishia zawadi kutegemea na unavyomfahamu
mpenzi wako anapenda nini na nini. Hakuna anayemjua mpenzi wako zaidi kuliko
wewe kwa hiyo lazima ujue ukifanya nini kwake na kwa wakati gani atafurahia na
kujivunia kuwa nawe.
5.
WHAT GOES AROUND COMES AROUND.
Unapokuwa kwenye mapenzi hakikisha kwa
khali yoyote humfanyi mpenzi wako awe na huzuni kila mara. Hapa ninamaanisha
kuwa USIPENDE KUMFANYIA KITU UNACHOONA AKIKUFANYIA WEWE UTAKOSA FURAHA. Hakuna
kitu kibaya kwenye mapenzi kama kukosa mapenzi uliyoyategemea kutoka kwa mpenzi
wako. Kama unaona mpenzi wako aki-cheat utaumia sana basi hata yeye siku
uki-cheat ataumia tena inawezekana kuliko wewe utakavyoumia. Usimfanyie kitu
amabacho wewe hupendi kufanyiwa hata siku moja.
6.
MFANYE AJIVUNIE KUWA NAWE.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku unamfanya
mpenzi wako ajivunie kuwa nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa kukuchagua wewe
miongoni mwa wote aliowaona. Usijidanganye hata siku moja kuwa kwa kumpata tu
na kwa yeye kukupenda basi hajaona mwingine wa kuweza kuwa naye. Wapo wengi
sana anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua wewe katika hao wote, kwa hiyo
usimfanye aanze kuwafikiria wale wengine wanaomfuatilia kila siku na kumsumbua.Ukianza
kumwacha aanze kuwafikiria wengine aidha kwa wewe kuwa unamkosesha amani ya
mapenzi kila mara au kwa mengine mabaya ndani ya mapenzi basi ipo siku utaishia
pabaya.
7.
MSAIDIE KWA KHALI NA MALI.
Kwenye mahusiano huwa kuna kupanda na
kushuka miongoni mwa wapenzi na hasa kiuchumi na hata kisaikolojia. Hakuna kitu
kizuri kwenye mapenzi kama mtu kupata tatizo na akasaidiwa na mpenzi wake katika
hali ambayo hakuitegemea, namaanisha mpenzi wako akipata tatizo lolote
hakikisha wewe ndo unakuwa wa kwanza kulifahamu na kulifanyia kazi. Sio
matatizo yote yanamalizwa kwa pesa so hata ushauri na kumpa mawazo chanya
inasaidia sana na kumfanya awe na furaha kuwa nawe.Kama unampenda usione tabu
kumsaidia kwa kuogopa kuonekana eti unahonga, huyo ni mpenzi wako kwa hiyo
jiamini na umpe kile anachostahili kusaidiwa na mpenzi wake.
Yapo mambo mengi sana ambayo kama
mkiyafanya kwenye mapenzi basi uhusiano wenu utakuwa wa kudumu na wenye furaha
sana ingawa hapa nimezungumzia kwa uchache sana lakini nina imani itasaidia
sana kwa wote walio kwenye mahusiano .
Mapenzi hayana ndumba au limbwata hata siku
moja, unapoona wapenzi wengi wana furaha kwenye mapenzi yao ni kwa sababu
wanavumiliana kwa mengi na kusameheana kwa mengi.
No comments:
Post a Comment