Mapenzi ni kitu Fulani tofauti sana kwenye hii dunia na hata
nje ya hii sayari. Mapenzi kwa kiasi kikubwa sana yanasababisha hata mambo
mengine kwenye hii dunia yaende sawa au yaende tofauti hata kama hayahusiani na
mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu
wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida kisa mapenzi.
Ukiachilia mbali PESA, Mapenzi huwa yana nafasi kubwa sana
kwenye kitu chochote ndani yahii dunia tunayoishi. Si masikini wala si tajiri,
wote kwa pamoja wanahitaji mapenzi kutoka kwa wanaowapenda ili dunia iweze
kwenda sawa kwa upande wao. Na ndio sababu hata mimi hapa ninaandika kuhusu
mapenzi kwa sababu yananigusa hata mimi na hata wewe unayesoma hapa sasa.
Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe
ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele
kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo
kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.
Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe
unavyojali basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha
ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo
kikubwa kama mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu bila
kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine
huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi
kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo
kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-
1.
UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye
mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa
sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa
wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni
muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti
maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni
jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua
unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.
2.
USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye
mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo
kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile
vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi
kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila
kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.
Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na
unahisi ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko
aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye
mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi
kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie
kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.
3.
ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama
kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu
yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa
inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa
bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye
mapenzi.
Kamwe
Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako, Usimfanye
Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji
Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya Mapenzi Ipo, Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi
Ya Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.
4.
DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa
kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano
jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata
kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu
mwenye dharau hata awe nani.
Na hii huwa mara nyingi inatokea pale
mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo,
pesa,uzuri au hata akili na mara nyingi
sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo,
ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa
6.
TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Tamaa ni kitu kingine ambacho hufanya
mahusiano mengi kukosa nguvu na mengine kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye
mapenzi na mmeamua kupendana kwa shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa
na tama na kukosa uvumilivu hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika.
Kama mpenzi wako ni wa hali Fulani na
umeamua kuwa naye basi usiwe na tama kwa vitu vingine ambavyo vinaweza
kukusababishia mahusiano yako kukosa nguvu na kufa kabisa. Amini kuwa ipo siku
mtakuwa na vitu kama unavyotamani kwa kuongeza bidii kutafuta na kushauriana
nini cha kufanya lakini si kwa kutafuta ‘’shotcut’’/njia nyepesi nyepesi
zinazoweza kuku-cost hapo baadae.
7.
KUKOSA MSIMAMO.
Hii kitu huwakuta wengi sana kwenye mapenzi
ya siku hizi. Nadhani ni hali halisi ya dunia ya sasa inachangia pia pamoja na
teknolojia tuliyonayo ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona kwenye mitandao
na vyombo mbali mbali vya habari.
Wapenzi wengi siku hizi wamekosa msimamo
kwenye mapenzi/mahusiano yao na unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi zaidi ya
mmoja na wanakuwa hawafahamiani huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo kila kitu
kwa mpenzi wake.
8.
KUTOJALI/KUTOKUWA NA MSAADA.
Hii pia kwa kiasi kikubwa inaumiza sana na
kupelekea kushuka kwa thamani ya mapenzi miongoni mwa mahusiano mengi haa
duniani. Kama kweli unampenda mpenzi wako basi msaidie anapopata matatizo na
umjali na kumchukulia kama mpenzi wako na mtu wako wa karibu na sio kukimbia
majukumu bila sababu zote za msingi.
Kama huwezi kujali na kusaidia basi
usiingie kwenye mahusiano ni bora ukae mwenyewe kuliko kuwepo sehemu
usiyotakiwa.
9.
UBAHILI.
Huna sababu yoyote ya kuwa na pesa na
mpenzi wako akawa anapata tabu kama vile humuoni. Sijasema utoe pesa hata kwa
mambo yasiyo na msingi lakini at least utimize majukumu yako kwa mpenzi wako
kila unapohitajika.
Kuna vitu vingine hata huhitaji kuambiwa
kama unatakiwa kuvishughulikia, ni wewe mwenyewe tu kuwa responsible kumhudumia
mpenzi wako. Na hii huwa ina-apply sana kwa wavulana kutokana na kasumba
iliyojengeka na mila tulizozikuta.
10.
USHOGA/USAGAJI
Hii ipo wazi kabisaaaaaaa…. Hakuna mtu
anayependa mtu wake awe Shoga kama ni mvulana au awe Msagaji kama ni msichana.
Ni aibu kubwa sana kwa mpenzi wako kuwa katika makundi haya mawili na sidhani
kwa akili ya kawaida kama unaweza kufurahia hiki kitu kama utakisikia au kama
utakishuhudia kwa macho yako.
No comments:
Post a Comment