Fikiri hili, wewe ni mwanamke mrembo wa wastani, mwenye hofu ya Mungu.
Kila siku jioni huwa unakwenda kufanya mazoezi baada ya shughuli za siku
na hii hukufanya uchelewe kufika nyumbani mara kwa mara.
Una kazi nzuri na mshahara mzuri wenye tarakimu nyingi kama namba ya
simu. Umeona gari zuri na ukaamua kulinunu tena kwa fedha zako mwenyewe
na Mungu akakujali kupata mume mtanashati na baraka ya watoto wawili.
Lakini kutokana na wingi wa majukumu unaona utafute dada wa kazi ambaye
atakusaidia shughuli za nyumbani. Dada huyo unamtoa huko kijijini
Sitimbi na wakati mwingine hata jina la ulipomtoa hukumbuki kwa jinsi
lilivyogumu.
Mumeo, kama walivyo wanaume wengi wa mjini, wao huwa hawahusiki na
kuchagua dada wa kazi. Lakini akija unamuuliza mumeo, umependa huyu dada
wa kazi? unamiini atakuwa msaada kwetu.
Msichana huyu huyu uliemtoa huko kijijini pengine hajui kushika hata
kalamu aandike jina lake. Pengine anamiliki mkoba wake mdogo aliotoka
nao kijijini na sura yake ya kuvutia ambayo hajajua kuitunza lakini
itaanza kuonekana akishaizoea nyumba.
Ili kumuonyesha wewe ndio mama mwenye nyumba, utakuwa ukigomba na
kumuelekeza namna ya kuvaa hasa wakati baba nani hii yupo. Utaenda
sokoni kumnunulia nguo ambazo zitamfanya onekane kama mzee. Hii ikiwa ni
njia ya kutaka kumlinda mumeo asiangukie kwenye mtego.
Lakini wewe upo busy kuvaa sketi fupi na vinguo vya kuacha maungo wazi
kuonyesha wewe ndio mwenye mamlaka katika nyumba. Kitu ambacho hujui ni
kuwa huyu msichana wa kijijini na yeye anajua namna ya kumpeti peti
mwanaume kama wa mama wa vijijini.
Msichana atakuja wakati mumeo yupo sebuleni na kukunja goti kwa heshima
akimuuliza kama anataka kuandaliwa maji ya kuoga. Sasa kwa mwanamke wa
mjini hadi akunje goti labda wakati anatafuta remote ya Tv aangalie
tamthiliya za kifilipino.
Mara ya mwisho mke wake kumuuliza kama anataka kuandaliwa maji ya kuoga,
Tanzania ilikuwa chini ya mfumo wa chama kimoja. Mumeo atakunja gazeti
lake, na kukubali kuwa aandaliwe maji.
Dada wa kazi ataandaa maji na kuhakikisha yapo katika joto linalotakiwa,
asijeunguza ngozi ya bosi wake. Wakati huo mke wa mtu anachati na
marafiki zake kwenye mitandao ya kijamii bila kujua upande wa pili
anampoteza mume.
Unaona kuwa ni vitu vidogo sana ambavyo wanawake huwa hawavifanyi na
kuviacha kwa wasaidizi wao wa nyumbani wafanye kwa ajili ya waume zao
bila kujua kuwa kwa kufanya hivyo wanajitengenezea njia ya kuwapoteza
waume zao kwa dada wa kazi.
No comments:
Post a Comment