Naitwa Patrick Bundala niko mailimoja Kibaha ni mwajiriwa wa serikali ni
Askari ila nyumbani ni Tabora na huku niko kikazi tu, nina mke na
watoto 4.
Kuna kitu kibaya kilinitokea nikiwa kozi ya uongozi huko Zanzibar mwaka
2009, tukiwa kozi tulikua tunapata mapumziko siku za weekend hivyo
kutumia nafasi hiyo kwenda kutembea beach na siku hiyo ya tukio baya.
Ilikua jumamosi ambapo tuliondoka tukiwa wengi tu kama 50 na kwenda
maeneo ya kilimani karibu na migombani ambako kuna beach nzuri sana na
siku ya jumamosi jioni beach huwa inajaa watu wa kila aina na siku hiyo
haikua mara ya kwanza mimi kwenda huko beach kwani kila weekend lazima
niende huko beach ili kuburudisha macho na kuangalia mazingira na watu
maana mimi kwa Zanzibar ilikua mara ya kwanza kwenda hivyo kwa umaarufu
wa Zanzibar nilitaka hadi natoka huko niwe na cha kuwasimulia huku
nyumbani kumbe ilikua bahati mbaya sana kwangu siku hiyo,
Wakati siku hiyo tumefika beach tulitawanyika kila mtu eneo analotaka na
wengine walienda kuogelea na mimi licha ya kufahamu kuogelea lakini
siku hiyo sikutaka kuogelea lakini nilitaka kutafuta binti mzuri ili
nimtongoze na tuwe wapenzi na nilienda pembeni kidogo eneo ambalo watu
walikua wachache na kukaa mkao wa kuangalia watu na baada kama ya dakika
40 alipita dada mmoja aliyevaa ninja akiwa ni nusu mwaarabu na nusu
mwafrika na nikajikuta namtamani sana alinipita kidogo na kugeuka na
kuniangalia na mimi nikaona hiyo ndio nafasi ya kumwogelesha na
kikamwita akaja na ajabu sikumwambia chochote lakini sijui aligundua
kuwa natafuta mwanamke maana alisogea na kunisalimia na akakaa pembeni
yangu na kunichangamkia sana,
na kwa sababu nilitaka mpenzi nilidhani kuwa huyo ni changudoa ambaye huwa anaenda kutafuta wanaume beach,
Baada ya kukaa tuliendelea na story na ajabu yule dada akaniambia
mwenyewe kuwa amenipenda sana maana nimemjali na mimi nikaona kuwa hiyo
nafasi ya kumpata mrembo yule siwezi kuipoteza na muda huo huo nikaanza
kumwambia mambo ya mapenzi maana nilidhani ni kahaba na nilipomwambia
hivyo alicheka na kusema amekubali ila anataka ajue kwanza jina langu,
kwa sababu ya kuepusha maswali ya kuulizwa zaidi na ili asije akakataa
kwa sababu ya majina yangu ya kikristo japokua hata kanisani sijawahi
kwenda nilimwambia kuwa mimi naitwa Saleh Juma na yeye akasema anaitwa
Munira, akafurahi sana na kusema kuwa nafaa sana na amefurahi sana
kukutana na mimi.
Sikutaka kuopoteza nafasi hiyo nilimwambia kuwa tunaweza kuwa wote usiku
ule? akasema mbona mapema sana nikasema kwa sababu amenivutia sana,
akaongea kwa madaha na kusema amekubali na kwa sababu ya binti yule
nilisahau yote na kumwambia tuondoke twende tukaongelee guest house
akakubali na tukaondoka saa ile ilie na kupanda gari za airport na
tukashukia mkunazini na kutafuta gest tulipata na nikaalipia na
tukaingia chumbani na lengo langu japokua nililipia chumba hadi asubuhi
lakini nilitaka tu tufanye mapenzi na niondoke kuwahi foleni ya usiku
kule kozi,
Tukiwa chumbani tulianza michezo ya kimapenzi na akanivulisha nguo zote
na mimi nikamvulisha nguo zote isipokua nguo ya ndani na baadae kidogo
akashuka kitandani na kusimama huku akinitazama kwa macho makali sana
nikaanza kushtuka na ghafla kibanio chake cha nywele kikaachia ghafla na
tukio la ajabu sana likatokea nywele zake zikalefuka na kuongezeka
zikajaa chumba chote,
Nikiwa nimejilaza kitandani nilikaa ghafla na baada ya muda kidogo zile
nywele zilisinyaa na kuwa za kawaida na kile kibanio kijiweka mahali
pake na kubana nywele,
Munira akasema kuwa yeye ni jini na anataka tu damu yangu kwani ana njaa
sana nilikimbilia mlangoni ghafla huku nikiwa uchi na kujaribu kufungua
mlango lakini haukufunguka japokua hatukufunga, akasema siwezi
kumtoroka hata siku moja na kwa sababu mimi nimempenda na yeye amependa
nyama yangu na damu yangu,
Nilijikaza lakini nilikua hoi karibu na kuzimia na nikaona njia
iliyobaki ni kupiga kele ili watu waje kunisaidia na nilipopiga kele
sauti haikwenda kokote maana nilipanua mdogo kwa nguvu zangu zote lakini
sauti iliyotoka ni kama namng'ong'eza mtu kiukweli nilikua kama
nimechanganyikiwa na niliposhidwa zoezi hilo niliwaza kuwa njia
iliyobaki ni kulibembeleza tu lile jini na nilipoliangalia nilikuta
linakwato miguuni na miguu ina manyoya kama mbuzi na meno limetoa na
kuwa marefu zaidi ya rula ya kupigia mistari,
Hakuwa tena yule msichana mrembo munira ambaye nilimpenda sana kwa muda
mfupi, Nilimwambia yule jini anibadilishie adhabu akakataa na nilijikuta
naomba maombi kwa MUNGU anihurumie na ajabu kama dakika 5 zilizofuata
mlango uligogwa na ghafla lile jini likawa Munira yule wa beach na kwa
sababu ya mlango kuendelea kugongwa yule jini alienda kufungua na mimi
muda huo nikaanza kuvaa nguo kiaskari yaani nusu dakika nimeshavaa zote,
Alikua ni dada wa mapokezi akileta chakula chipsi mayai na na soda na
munira kwa ujanja akasimama katikati ya mlango na kuanza kusema sisi
hatukuagiza chochote na muda huo huo nikamwambia yule dada aingie ndani
maana kuna kitu nataka kumtuma akaja na alipokaribia tu nikatoka ghafla
na kumwaga kile chakula chote huku nikisema kuwa yule dada sio mtu ni
jini yule dada mhudumu naye akaakimbia na sikujua kilichoendelea ila
nadhani yule jini alipotea muda huohuo maana nilipofika tu nje nilimkuta
akinisubiri na kuniambia sina ujanja wa kumtoroka na kwasababu ilikua
ni barabarani na watu wengi wanapita nilipiga kelele na kusema jamani
niokoeni na vijana fulani waliokua wanapita mmoja wao akasema wewe
umekua chizi yaani unaongea peke yako niliondoka kwa kukimbia kama mita
100 na kupanda gari ambayo ilinipekeka hado kambini.
Nilipofika tu kambini nilimwona tena yule jini na akaniambia kuwa kuniua
lazima anaiue tu tena usiku uleule nilipiga tena kele na askari
wenzangu wakaanza kucheka sana wakisema nimepandisha mashetani na
nikawaelezea kuwa sijapandisha chochote ila ni hali halisi na
nikawasimulia mwanzo wa tukio hadi mwisho na usiku huo sikulala maana
usiku wa saa 7 nilimwona tena yule munira jini na nikapiga kelele na
wenzangu kwa hasira wakasema nisiwasumbue lakini mmoja wao ambaye
ameokoka akaniambia namhitaji YESU ili niwe huru
No comments:
Post a Comment