Kutoka katika misuli ya mwili,kifua,unavyocheka hakili yako au kwa maana
nyingine kujitambua,wasichana wanaelezea mambo ambayo wanapenda sana
kutoka katika mwili wa mwanamme.
Kama ukimuangalia msichana machoni unapokuwa mtaani kwako,au kama
mmetoka na msichana wako kwenda kwenye matembezi ya kimapenzi(out),au
ukiwa umekaa na msichana au mpenzi ambaye mmeoana kwa muda mrefu,najua
umekuwa ukijiuliza kwa muda mrefu sana kwamba mpenzi wako amekupendea
nini na umemvutia kwa kitu gani kimuonekano mpaka akakubali kuwa mpenzi
wako? Kutoka kwenye mwili wako mzima mpaka ndani ya suruali yako umekuwa
ukijiuliza ni sehemu zipi wasichana hata kabla ya kuwa mpenzi wako huwa
anapenda sehemu zipi? sehemu gani ambayo mwanamke au msichana wako huwa
anachanganyikiwa sana mnapokuwa uso kwa uso,kifua kwa kifua au mkiwa
kwenye mashuka? Haya ni maswali ambayo wanaume na wakaka wengi huwa
wanajiuliza sana linapokuja swala la kumpenda msichana.
Tuliwauliza wasichana 25 kutoka katika historia tofauti ya maisha
yao,sehemu walipozaliwa,na tofauti ya mitindo ya maisha yao kuelezea ni
sehemu gani ambazo wasichana wanapenda sana kutoka kwa mwanaume.
Kwa mujibu wa mwanamke au msichana yeyote yule sehemu inayomvutia sana
kwake inaweza kutokana na sehemu mbili ambazo ni moja ni;kuzaliwa na ya
pili ni ile ambayo inatokana na mazoezi kama "Gym nk".Ndio unaweza
ukashangaa lakini ndio hivyo wasichana walitupa maoni yao kulingana na
kile wanachokipenda kutoka katika mwili wa mwanaume.
MSICHANA 1:
" Ninapenda sana muonekano wa TUMBO la mkaka hasa linapokuwa "FLAT " na sio kitambi"-Pilietta
MSICHANA 2:
"Ninapenda mwili wote wa mwanaume,lakini ukiniambia nichague sehemu
ninayoipenda zaidi ni mi ninapenda MIKONO ILIYOJAA VIZURI na inapokuwa
mizuri basi mimi nasikia raha"-Christina
MSICHANA WA 3:
"Mimi ninapenda mwanaume ALIYEJAA MIKONO vizuri,hasa hasa anapokuwa na
mgongo mpana kwangu mimi nachanganyikiwa kabisa,huwa najihisi kuwa na
amani na furaha sana ninapokuwa na mkaka mwenye mgongo mkubwa"-Sarah G
MSICNA WA 4:
"Mimi napenda mkaka mwenye VIGANJA VIKUBWA hali hii hunifanya nifikile
kwamba mkaka huyu anaweza kufanya mambo vizuri kwa sababu ya kuwa na
viganja imara na nguvu za kutosha."-Julia
MSICHANA WA 5:
"Mimi napenda mkaka mwenye TABASAMU ZURItabasamu huwa linanifanya moyo
wangu unayeyuka kabisa kama barafu ndani ya maji ya moto"-Mariamu
MSICHANA WA 6:
"Mimi napenda mwanaume mwenye nguvu yaani aliyejaa mikono vizuri na
mwenye mabega mapana na yaliyojaa vizuri,ili aweze kunibeba si unajua
tena mambo ya mapenzi"-Lydia
MSICHANA WA 7:
"Mimi napenda mwanaume mwenye MACHO MAZURI macho mazuri hunifanya nichanganyikiwe kwa kumuangalia tu"-Anna
MSICHANA WA 8:
"Mimi napenda mwanaume mwenye MAKALIO MAKUBWA KIASI asiwe mwembamba
sana,ninapenda makalio na sijui ni kwa nini nimejikuta ninapenda
tu"-Sarah
MSICHANA WA 9:
"Mimi ninapenda wavulana wenye umbo la "V" katika matumbo yao na lazima
mwanaume ninaye mpenda mimi awe ni mtu wa mazoezi"-Elizabeth
MSICHANA WA 10:
"Mimi napenda mkaka mwenye TABASAMU ZURI basi"-Recho
MSICHAN WA 11:
"Mimi ninapenda mwanaume mwenye Kifua kipana na kilicho jaa vizuri"-Fatumah
MSICHANA WA 12:
"Kwa upande wangu mimi ninapenda mwanaume mwenye mikono mikubwa ya
kuweza kunibeba huku na kule kunapokuwa kwenye mambo yetu yale"-Mwajumah
MSICHANA WA 13:
"Mimi napenda mwanaume mwenye misuli imara sana na yenye nguvu kuanzia chini mpaka juu ila asikomae sana jamani"-Brigite
MSICHANA WA 14:
Msichana wa kumi na nne naye alisema kwamba anapenda sana wakaka wenye mikono mizuri
MSICHANA WA 15:
Msichana wa kumi na sita naye pia alisema kuwa anapenda wakaka wenye vifua vikubwa.
MSICHANA WA 16:
"Hahaha swali lahisi sana kwangu hilo,mimi napenda mkaka mwenye mikono mikubwa na iliyo jaa zuri na tumbo lililokaza vizuri".-Tunuh
MSICHANA WA 17:
"Mimi ninapenda sana wakaka wenye makalio makubwa kama vile wakaka wanavyopenda wasichana wenye makalio makubwa"-Vanessa.
MSICHANA WA 18:
"Mimi ninapenda wakaka wenye tabasamu zuri hasahasa anapokuwa na meno maeupee! yananivutia sana jamani"-Eliza J.B
MSICHANA WA 19:
"Mimi ninapenda sana mwanaume mrefu kwa sababu mimi ni msichana mrefu kidogo kwa hiyo huwa sipendi kumzidi urefu mpenzi wangu ndio maana napenda wakaka warefu"-Paulinah
MSICHANA WA 20:
"Mimi napenda mkaka awe na mwili msafi siangaliii kifua wala mikono wala nini,ila mimi napenda awe mtanashati"-Mwavua.
"Hahaha swali lahisi sana kwangu hilo,mimi napenda mkaka mwenye mikono mikubwa na iliyo jaa zuri na tumbo lililokaza vizuri".-Tunuh
MSICHANA WA 17:
"Mimi ninapenda sana wakaka wenye makalio makubwa kama vile wakaka wanavyopenda wasichana wenye makalio makubwa"-Vanessa.
MSICHANA WA 18:
"Mimi ninapenda wakaka wenye tabasamu zuri hasahasa anapokuwa na meno maeupee! yananivutia sana jamani"-Eliza J.B
MSICHANA WA 19:
"Mimi ninapenda sana mwanaume mrefu kwa sababu mimi ni msichana mrefu kidogo kwa hiyo huwa sipendi kumzidi urefu mpenzi wangu ndio maana napenda wakaka warefu"-Paulinah
MSICHANA WA 20:
"Mimi napenda mkaka awe na mwili msafi siangaliii kifua wala mikono wala nini,ila mimi napenda awe mtanashati"-Mwavua.
No comments:
Post a Comment