Tatizo la wanaume kufika kileleni mapema “early ejaculation” au kufika kileleni gafla na kwa kasi “rapid ejaculation”huwatokea
wengi na kuwa kikwazo na chanzo cha maudhi kwa wapenzi wengi, wapo
wanaoamua kulizungumzia hili katika mahusiano yao na wengine
wanalinyamazia ingawa lina waumiza, tatizo hili limeathiri asilimia 25
hadi 40 ya vijana nchini marekani. Inasemekana, mbali na kukosa nguvu za
kujizuia ili mtu asifike kilele, tatizo hili pia husababishwa na
msongo wa mawazo “stress”, fadhaiko la moyo au sonona “depression”, tabia za kujichua “masturbation”, na matarajio potofu na ya uongo yanayoletwa au kuhamasishwa na vyombo vya habari “media influence”
kuhusu uwezo wa mwanaume kingono. Wanaume wenye matatizo makubwa katika
uwezo wao wa kufanya tendo la ndoa na wanaojiamini sana huweza
kudhalilika kirahisi katika hili. Sababu nyigine inayoweza kumfanya
mwanaume afike kileleni mapema au gafla ni pale anapofikwa na hofu “stage fight”
kwa kuwaza jinsi mwanamke wake alivyo mzuri na kwamba inamlazimu (yeye
mwanaume) kumfurahisha katika tendo hili, na hapo hapo mwanaume akawa
na kiu na shauku kubwa ya kumfikisha kileleni mpenzi wake, viwili hivi
vikigongana vinaleta kitu kiitwacho “performance anxiety” na inaweza kukufanya kushindwa kabisa kufanya chochote. Ndiyo maana wakale wakasema “mkamia maji hayanywi” – Chris Mauki.
No comments:
Post a Comment