Usaliti hauishii tu katika
kujihusihsa kimapenzi na mtu mwingine hata kufanya mambo ambayo mwenza
wako akiyagundua moja kwa moja atajihisi kuwa anaswalitiwa ni usaliti.
Ni jambo la kawaida siku hizi kukuta mtu mwenye mpenzi anachat katika
mitandao ya kijamii na mtu wa jinsia tofauti. Hapa sizungumzii kuchat
kwa kusalimiana bali kuchat kimapenzi.
Kusalimiana kimapenzi, kuongea
kimahaba na kuchombezana na kufanya mambo ambayo kiuhalisia walipaswa
kufanya na wapenzi wao. Inawezekana unachat na mtu ambaye yuko mbali
labda unamdanganya tu ili akutumie pesa na huna mpango wa kuonana naye
au hata haiwezekani kuonana naye, lakini kama unamfanya mhusika kuhisi
nyinyi ni wapenzi basi unamsaliti mwenza wako.
Lakini chukulia mfano kwa namna
yoyote ile mpenzi wako akaziona zile meseji je atakuelewa ukimuambia
huyu ni rafiki tu? Au je atakuelewa ukimuambia nilikuwa namtania tu?
Tuseme achana na mpenzi wako, vaa viatu vyake na kujiuliza je nikimuona
mwenza wangu anachat namna hii na mtu mwingine nitamchukuliaje?
Usiruhusu mambo ya kijinga namna
hiyo kukuharibia mahusiano yako. Hii ni hasa kwa wanawake, mwanaume
kakusalimia kaanza kukutongoza cha kujilegeza eti umchune kwanza kuwa
mstaarabu kumuambia kuwa nina mtu na kwa heri, akama nasumbua sana
mblock tu au usijibu sms zake. Lakini kumjibu kuacht naye kimahaba hata
kama unatania jua unasaliti kwani mwenzi wako akikufumania hatali kama
unatania au la na kumbuka uaminifu ukishapote ahaurudi tena.
Kuna watu wengi wamaharibu mahusiano
yao kwakuwa tu walikuwa wanataniana huko katika mitandao ya kijamii,
watu wameharibu ndoa zao kwa mitego tu ya kijinga katika mitandao ya
kijamii. Mtu anayejiheshimu huweka mipaka katika matumizi ya mitandao ya
kijamii na kama rafiki yako katika mitandoa ya kijamii akiivuka hiyo
mipaka basi unamuambia kwaheri.
No comments:
Post a Comment