Pamoja
na ukweli wa tafiti kwamba jinsi tunavyozielezea na kuzionyesha na
kuzidhihirisha hisia zetu baina ya wanaume na wanawake au mke na mume
hutegemea na utofauti tulionao katika maeneo ya ubongo wetu, ni kweli
pia kwamba malezi na makuzi yetu yanachangia sana. Unapoona mtu
anahasira za karibu, au haoni aibu kabisa, au analia kwa kitu kidogo, au
ni mtu wakulaumu sana, au mtu wa kutafuta visingizio, au mtu wa
kususa, au mtu wa kunyamaza na tabia nyingine nyingi, ujue malezi na
makuzi yake yanamchango mkubwa sana katika kumfanya yeye kuwa hivyo
alivyo. Usisahau au kutosisitiza kufahamu malezi na makuzi ya mwenzako
kabla hamjaanza kuishi pamoja, yasije yakakutokea puani mengine
usiyoyajua, ni bora hufahamu kuwa unaishi na chui kuanzia mwanzo kuliko
kudhani unaishi na paka na baadae ukagundua kumbe ni chui – Chris Mauki
Wednesday, May 17, 2017
JE UNALIJUA CHIMBUKO LA HIZO TABIA UNAZOZICHUKIA ZA MPENZI WAKO??
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment