1. Kwanza mdomo wa mbu haupo kama sindano za kawaida
zinazotumika, mlija wa mbu ambao hutumika kuingizia mate yenye vimelea
vya malaria ni tofauti na ule unaotumika kufyonza damu kutoka kwa
binadamu, kutokana na hili kwaiyo damu tu ndio huingia
kwenye mwili wa mbu kutoka kwa binadamu alieng`atwa na mbu, na mate tu
ya mbu ndio huingizwa kwenye mwili wa binadamu.
2. Pili magonjwa yote ambayo huambukizwa na insekta kama,
matende na malaria aya magonjwa yanaweza kusambazwa na mbu kwa sababu
vimelea vya aya magonjwa huweza kujizalisha(multiply) katika mwili wa
mbu, ambapo hivi vimelea huweza kusambaa hadi kwenye mate ya mbu baada
ya hapo huweza kuingizwa kwa kung`atwa binadamu. Tofauti ni kwamba
vimelea yani virusi vya ukimwi(vvu) vinapoingia kwenye mfumo mzima wa
mmeng`enyo wa mbu humeng`enywa kama chakula cha kawaida kisha hutoka
kama uchafu, ili virusi vya ukimwi viweze kujizalisha(multiply) ni
lazima viingie kwenye seli maalumu za binadamu.
3. Tatu, virusi vinavyosabisha ukimwi huzunguka taratibu
kwenye damu ukilingansha na vimelea vinavyosababisha magonjwa yatokanayo
na insekta(mbu), hii inamaanisha ata mbu anaponyonya damu kwa binadamu
ambaye tayari virusi vya ukimwi hawezi kunyonya idadi kubwa ya virusi.
Tafiti zaidi zinaonyesha kwamba ili mbu aweze kueneza virusi vya ukimwi
kwa binadamu mtu huyo ina bidi ang`atwe na mbu million kumi(10) idadi
hii ya mbu ndio inaweza kutengeneza uniti moja(1) ya kirusi apo ndipo
huenda kikasababisha kueneza vvu, hii inamaanisha ata ikatokea kwa
bahati mbaya uka mmeza mbu aliye mng`ata binadamu ambaye ana virusi
vinavyosabisha ukimwi huwezi kupata maambukizi.
UHIMU
Achana na ngono zembe kwani
huchangia kwa asilimia kubwa maambukizi
ya VVU ambavyo usababisha UKIMWI…
Achana na ngono zembe kwani
huchangia kwa asilimia kubwa maambukizi
ya VVU ambavyo usababisha UKIMWI…
No comments:
Post a Comment